NJIA MPYA YA KUPIMA SARATANI YA TEZI DUME

Kupima saratani ya tezi dume kwa wanaume wengi limekuwa jambo gumu kutokana na vipimo vyote vilivyopo kwa sasa kuhusisha uchunguzi kufanyika kupitia njia ya haja kubwa. Na kwa wengi hili ni jambo lisilofurahisha ata kidogo.

Habari njema imekuja. Watafiti wa nchini Uingereza wamefanikiwa kuja na kifaa kinachopima mkojo kwa mfumo wa kuunusa na kutoa matokeo kama mtu anatatizo la saratani ya tezi dume au la.

tezi-dume
Aina ya upimaji wa ugonjwa huu kwa miaka mingi unahusisha njia isiyopendwa na wengi
Kipimo hicho kinachotumia mfumo wa kusoma hewa na harufu ya mkojo (gas chromatography sensor) kinaweza pia kutoa majibu ya magonjwa mengine kama vile saratani ya kibofu (bladder cancer) na hematuria (ugonjwa wa kukojoa damu).
Kifaa hicho katika majaribio yake walitumia kuwapimia wanaume 155, katika hao 58 walikutwa na ugonjwa wa tezi dume, 24 na kansa ya kibofu na 73 na hematuria.
Kipimo cha Kupima saratani ya tezi dume
Odoreader – unaweza kukiita ni pua ya elektroniki, kupitia harufu ya mkojo kifaa hichi kitaweza kupima na kutoa majibu
Kumbuka kipimo hichi kitatoa majibu ya chanya (positive) ata kama bado ugonjwa huo upo katika hatua za mwanzo na hivyo kumsaidia mtu husika kuwahi kupata matibabu husika.
Kifaa hicho cha ‘The GC Sensor system’, kimepewa jina la Odoreader na kimetengenezwa na maprofesa wawili wa Uingereza – Bwana Chris Probert wa chuo kikuu cha Liverpool na Bwana Norman Ratcliffe wa chuo kikuu cha West of England Bristol.

Teknolojia hii imesifiwa sana na wengi wanaona itasaidia kurahisisha wanaume wengi kufanya kipimo hicho bila kujisikia vibaya au kuwa na fedhea ukilinganisha na njia zinazotumika kwa sasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post