Kisukari kwa wajawazito

425_2960207
Ugonjwa wa kisukari kitaalam  unaoitwa Diabetes Mellitus hutokea pale tezi kongosho au Pancrease inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin.
Wengine hupata ugonjwa huo pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo cha Insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu au kitaalam Hyperglycemia.

Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti sukari katika damu mwilini.
Lakini kuna baadhi ya wanawake hupatwa na kisukari kutokana na kuwa na ujauzito.
Siyo lazima kuwapima akina mama wote kuchunguza ugonjwa wa kisukari, lakini kwa kuwa vipimo vya kisukari si ghali ni vizuri kuwapima wote wenye ujauzito.
Mara nyingi wajawazito wanaopatwa na kisukari ni wale wanene, wanaoongezeka uzito isivyo kawaida, wenye magonjwa ya kuwashwawashwa na fangasi kwenye sehemu za siri, waliowahi kuzaa mtoto mwenye uzito mkubwa (zaidi ya kilo 4), wenye ugonjwa wa presha na wale walio na mababu na mabibi au wazazi wenye ugonjwa wa kisukari.
Wenye dalili za ugonjwa wa kisukari lazima wapimwe hasa wale wanaojisikia kiu sana, kukojoa mara kwa mara kusikia njaa kali.
Mbali na dalili hizo nilizozitaja, dalili nyingine ni kusikia kuchoka haraka wakati wa kutembea, wakati wa kufanya kazi au wakati kufanya mazoezi, kusinzia, kusikia kichwa kizito na kutoona vizuri (kuona giza).
Dalili nyingine ni matatizo kwenye macho, figo, mishipa ya fahamu, mishipa ya damu, nguvu za kiume, kupoteza fahamu, ni sababu ya kuwa na sukari nyingi mwilini kitaalamu huitwa Hyperglycaemia, mgonjwa kusikia maumivu, kutekenywa au joto kwenye miguu na mikono.
TIBA KWA KISUKARI KWA WAJAWAZITO
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari ni kuhakikisha kiasi cha sukari kinashuka na kuwa katika hali ya kawaida, ili sukari isiingie kwenye damu ya mtoto na kuongeza kiasi cha sukari na mafuta mwilini mwake.
Mama anafuatiliwa kama anakula chakula alichoshauriwa na daktari, kupima damu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa kiasi cha sukari kwenye damu yake hakiongezeki na kumdhuru mtoto atakayezaliwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post