KWA miaka mingi sasa, baadhi ya watu wamegubikwa na dhana potofu ya kwamba, kuwa mweupe ndiyo urembo .
Dhana hii imewafanya wengi waanze kutumia vipodozi vikali, bila kujali madhara ya baadaye.
Kwa mfano, hata baadhi ya wasanii, wake kwa waume, wamekuwa wakijibadili ngozi zao na tumewaona wakibadilika hatua kwa hatua.
Hata hivyo, unapohisi kuna uzuri, mara nyingi kuna kudhurika. Madhara ya awali ya vipodozi hivi, huonekana kwa mtumiaji kubabuka ngozi, kuwa na mabaka meusi au ngozi kuwa nyekundu. Lakini yapo madhara mengine mabaya zaidi ya hayo.
Kemikali hatari
Katika bidhaa hizo zinazotumika za kujichubua, kuna kemikali za aina mbili.
Kwanza ni ‘Hydroquinone’ na ya pili ni ‘Mercury’.
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira.
Hutumika pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele.Mercury nayo ni kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika maduka ya madawa tu tena bila maelekezo ya madaktari
linapokuja swala la afya zetu kwa siku hizi kumekuwa na mlipuko wa magonjwa mengi yasiyo kuwa na tiba na hii inachangiwa na vitu au vipodozi tunavyokua tunavitumia bila kujua nini chanzo chake na vina tengenezwa na nini, imefika wakati watu k lazima tujifunze na tuwe wasikivu sana hasa ujitabua na kuanza kutumia vipodozi asilia
1. Moja kati a viambato vilivyopigwa marufuku kutumika kama kipodozi ni aina ya “steroids” ambazo kimsingi ni dawa, mfano wa viambato hivi ni pamoja na “Clobetasol” na “Betamethosone” zinazopatikana katika dawa aina ya MOVATE, BETACIRT-N, DIPROSON, GENTRISONE, n.k
2. Bidhaa hizi zinaendelea kutumika kama dawa za cheti (prescription only medicine) na lazima kutolewa kwa wagonjwa wa ngozi kwa kufuata maelekezo ya kidaktari na mfamasia. Hata hivyo, haziruhusiwi kutumika kama vipodozi.
3. Dawa nyingine zilizopigwa marufuku kutumika kama vipodozi nizile za kuongeza makalio na maziwa. Hii ni kutokana na kusadikiwa kuwa huleta madhara kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kuhatarisha kupata ugonjwa wa kansa.
4. Kutokana na madhara hayo ya kiafya na kiuchumi yanayoweza kusababishwa na matumizi ya mikorogo na vipodozi vyenye viambato sumu, TFDA imeweka mifumo ya kiuthibiti wa vipodozi ili kuhakikisha kuwa vipodozi vinatumiwa na wananchi ni bora na salama. Hii ni kwa kuhakikisha kuwa vipodozi hivi havina viambato vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya ya mtumiaji.
5. Mifumo ya uthibiti wa vipodozi inajumuisha usajiri wa vipodozi, udhibiti katika uingizaji, ukaguzi na ufuatiliaji na utoaji wa vibali vya biashara ya vipodozi kama ilivyoainishwa.
MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU
1. BITHIONOL
athari zake.
Kupata mzio wa ngozi/allergic na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua.
2. HEXACHLOROPHENE
madhara/ athari
· Inapenya kwenye ngozi na kuingia kwenye ishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu hasa kichwani.
· Pia inasababisha ugonjwa wa ngozi na kuathirika kwa ngozi pindi unapokuwa kwenye mwanga wa jua.
· Kwa watoto wachanga husababisha uhalibifu kwenye ubongo
· Vile vile ngozi inakuwa laini na kusababisha kupata ugonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi.
3. ZEBAKI (MERCURY)
Madhara /Athari
· Husababisha madhara ya ngozi, ubongo, figo na viungo, mbalimbali vya mwili
· Zebaki inapopakwa kwenye ngozi kuweza kupenya taratibu ndani ya mwili na kusababisha sumu yake kuingia kwenye damu na kusababisha madhara mwengi mwilini.
· Mama mjamzito akitumia vipodozi vyenye zebaki mtoto huathirika akiwa akiwa bado tumboni na huzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.
· Husababisha ngozi kwa laini na kuwa na mabaka meusi na meupe
· Husababisha mzio/ allergic wa ngozi na muwasho
· Sumu iingiapo kwenye mishipa ya fahamu husababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu.
· Sumu ya zebaki ikiingia mwilini kwa kiwango kikubwa husababisha madhara maka upofu, uziwi, upotevu wa fahamu wa madhara mara kwa mara.
4. VINYI CHLORIDE
Madhara/ athari
· Inasababisha kansa ya maini, ubongo, mapafu na mfumo wa damu
· Sumu pia husababisha kuumwa kichwa, ksikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
5. ZIRCONIUM
Madahara/ athari
· Husababisha kansa ya mapafu na ngozi
6. HALOGENATED SALICYLANILIDE
Madhara \athari
· Husababisha mzio wa ngozi mara inapopata mwanga wa jua
· Husababisha ugonjwa wa ngozi
7. CHLOROQUINONE
Kundi zima la vipodozi vya CHLOROQUINONE hutumika kutengenezea vipodozi lakini kiambato ambacho kinachotumika ziaid ni kiambato cha Hydroquinone.
8. HYDROQUINONE
Madhara/ athari
Husababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, kansa, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meusi na meupe.
Tags:
MAGONJWA YA NGOZI