Ni kwanini tunapenda kula chakula chenye viungo vinavyotuwasha na kutuumiza?

Man struggling to eat chilliesMwaka jana, madaktari katika chumba cha dharura cha hospitali walikimbia kubaini ni nini lilikuwa ni tatizo alikuwa nalo mwanaume mmoja ambaye alikuwa amewasili akiwa na maumivu makali, akiwa na wasiwasi, maumivu makali ya kichwa na shingo na kupumua kwa kasi.
Baada ya kufanya skani ya CT, vipimo vya mkojo, damu na kufanya uchunguzi wa mwili, walibaini kuwa hakupewa sumu au kukumbwa na ugonjwa wa ajabu, bali alikuwa amekula pilipili kali kuliko pilipili zote duniani.
Aina hii ya pilipili iliyomuathiri ilikua inatwa "Carolina Reaper" (ambayo ni kali mara 275 kuliko pilipili zote) ambayo mwanume huyo wa miaka 34-alikua ameamua kuila katika mashindano.
Bahati yake , mishipa midogo ya kuingia kwneye ubongo iliyokua imeumia iliweza kutibiwa na kupona na kuweza kupona kabisa.

Carolina ReaperHaki miliki ya pichaPUCKERBUTT PEPPER COMPANY
Image captionPilipili hii ya reaper hulimwa South Carolina hinashikilia rekodi ya kwanza kama kwa kua ndio "kali zaidi " duniani

Huu unaweza kuwa ni mfano wa athari kubwa, lakini mamilioni - na huenda bilioni ya watu -kote duniani mara kwa mara huketi na kula chakula vyakula vyenye viungo vinavyowafanya wahisi wanaungua au kuwashwa ulimini na kutufanya wakati mwingine kutufanya tukimbilie kinywaji au kutupatia maumivu ya tumbo- au hata kujihisi vibaya zaidi. Kwanini?
Ni mapenzi ya kiungo hiki ambayo yamekuwepo kwa takriban maelfu ya miaka na hayapungui- wazalishaji wa pilipili mbichi za kijani wameongeza kiwango cha uzalishaji kutoka tani milioni 27 hadi milioni 37 kati ya mwaka 2017 na 2018.
Baadhi ya nchi zina kiu kubwa zaidi ya kuwashwa kuliko nyingine.
Nchini Uturuki , watu hula wastani wa gramu 86.5 kwa siku - kikiwa ni kiwango kikubwa zaidi duniani- kikiwa ni cha juu zaidi ya nchi ya pili kwa mapenzi ya pilipili ambayo ni Mexico ambako gramu 50.95 za pilipili huliwa katika chakula chao. Je ni kwanini tunakula chakula kinachowasha sana ?
Ni hadithi ngumu huu ya namna tunavyopenda kutafuta saikolojia na kuhangaika dhidi ya mageuzi ya hisia zetu.

Farmers with chilliesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUzalishaji wa Dunia wa pilipili ulifikia tani milioni 37 mnwamo mwaka 2018

Siri ya asili

Hata mchakato wa mageuzi ambao huifanya pilipili kuwa capsaicin, kiungo ambacho huwasha bado unaibua mjadala.
Wanasayansi wanafahamu kuwa mimea inaonekana kuwa mikali baada ya muda, na kwamba hutengeneza ladha kali kujaribu kuwazuia wanyama na wadunu kuila.
Lakini ndege huwa hawana tatizo na ulaji wake.

Parrot eating a chilliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTofauti na wanyama na waduni, ndege hawana shida ya kula pilipili

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Arizona, nchini Marekani , wamegundua ni kwanini hii inafanya kazi kwa mimea ya pilipili.
Mfumo wa usagaji chakula wa mamalia hutafuna mbegu zake na kuzizuwia kuota.
Lakini hiyo sio sababu kwa ndege ambazo mbegu hupita bila madhara na kutoka nje kwa njia ya kinyesi tayari kutengeneza mimea mingine .
Kwa hiyo mimea ya pilipili ilitengeneza kinga yake ili kuwazuia wanyama aina ya mamalia kula matunda ya mmea , nkwanini haiwazuwii binadamu?.

Chilli eating contest in HanghzouHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionShindano la kula pilipilikatika mji wa Uchina wa Hanghzou limekua maarufu zaidi na zaidi kote duniani

Inashangaza zaidi hususan ni kwamba kwa kawaida wanadamu huhusisha ladha chungu na sumu- hiyo ndio njia yetu ya kujilinda.
Kuna nadharia kwamba tabia ya binadamu na wanyama kula pilipili nchini Uchina ni ya mababu zao wa kale.
Moja ya nadharia ni kwamba binadamu walipata ladha ya kiungo cha vyakula kwasababu ya kukabiliana na vimeta na bakteria katika vyakula vyao.
Wazo ni kwamba watu walianza kubaini kuwa vyakula vyenye ladha ya kiungo cha pilipili havikua vinaoza - na ukali ilikua ni ishara kuwa chakula hakijaoza
Nadhalia hii iliendelezwa na utafiti wa mwaka 1998 uliofanywa na Wanabaiolojia wa Chuo Kikuu cha Cornell Jennifer Billing na Paul W. Sherman.
TWalitathmini maelfu ya vyakula kuanzia vile vyenye nyama vya nchi 36 na kubaini kuwa viungo vilitumiwa zaidi katika mataifa yenye hali ya hewa ya joto, ambako vyakula vilikua na hatari kubwa ya uwezekano wa kuharibika zaidi.

Plate of tacosHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJe mapenzi yetu ya pilipili yalianza kama hatua ya kulinda chakula chetu dhidi ya kuharibika?

" Katika nchi za joto , karibu kila chakula chenye nyama huwekewa walau kiungo cha aina moja, na vingi huhusisha kiungo cha pilipili, huku katika nchi za baridi vyakula vikiandaliwa vingi bila viungo, au kwa viungo vichache ," walibaini.
Nchi kama vile Thailand, Ufilipino , India na Malaysia ni za kwanza kwa matumizi ya viungo, huku Sweden, Finland na Norway zikiwa za chini.
" Ninaamini kwamba vyakula ni vya pili katika historia ya harakati za mageuzi kati yetu kwa na wadudu wetu. Vimelea vinashindana na binadamu kwa chakula kinachofanana ," Anasema Sherman.

Chilli processing plant in TurkeyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUturuki ni moja ya wazalishaji wakuu wa pilipili dunia, na pia ulaji wake ni mkubwa kwa mwaka.

Anaeleza kuwa,jinsi tu kama ilivyo kwa miwa na viazi, pilipili ni chakula ambacho kwa miongo kilifahamika Ulaya. Lakini baada ya wavumbuzi wa Ulaya kufika Marekani na kuanza kufungua biashara, walisambaa kote dunia .
"Pilipili ilihamishwa kote duniani na wavumbuzi wa Ulaya," O'Connor anasema.
Chaula chao cha kuvutia kiliigwa katika mapishi kote duniani, yakiwemo yale ya India, Uchina na Thailand.
Hata hivyo, kulikua na nadharia ya iliyoshindaniwa ya kuelezea mapenzi yetu kwa pilipili : uhusiano wetu na chakula chenye kiungo ni matokeo ya kile kinachofahamika kama " hatari ".

Chilli plantHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanasayansi wanaamini kwamba pilipili zilijitengenea "ukali" kuwazuia wanyama na wadudu wasiile

Inasema tulianza kula pilipili kwasababu ya kupata kiu kutaka kuzungushwa kwenye mabehewa ya mchezo ya umeme yanayozungushwa kwa leri za kujifurahisha au kuruka kwa parachuti kutoka kwa ndege.

Ladha zinazoumiza

Wazo lilianzishwa na Paul Rozin, profesa wa saikolojia katika Chuo Kiku cha Pennsylvania, ambaye udadisi wake ulitokana na ukweli kwamba wengi wa wanyama wa jamii ya mamalia hawali pilipili.
Aliwapatia watu pilipili kali sana hadi wealiposhindwa kuhimili ukali tena.
Katika mahojiano, waliokula waliulizwa walipenda zaidi kiungo gani kilichokua na pilipili. Walichagua kiwangi cha juu zaidi ambacho hawakuweza kukistahimili.
"Binadamu sio wanyama pekee wanaofurahia matukio ambayo ni ya hasi ," Rozin anaeleza.
"Akili zetu hujifunza kutambua kwamba hatuko mashakani hata kama miili yetu itajibu kinyume ."
Ni kama tunapenda kula pilipili zenye muwasho mkali kwa sababu sawa na ile ya kupenda kuona filamu za kutisha.

Woman eating chilliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJe tunakula pilipili kwa ajili ya muwasho wake?

Sayansi pia pia inataka kuelewa ni kwa nini watu hupenda pilipili kali zaidi ya wengine .
Mwanasayansi wa chakula Nadia Byrnes alipanga kuvumbua uwezekano kwamnba jinsia pia huchangia katika ulaji wa chakula cha pilipili au la.
Alibaini kuwa wanaume huwa wanapenda kufanya vitu visivyo vya kawaida wakichochewa na haja ya kuwaonyesha watu uwezo wao kula pilipili kali zaidi, huku wanawake wakipenda zaidi ladha za joto linaloumiza.
"INchini Mexico, kwa mfano ,ulaji wa pilipili unahusishwa na nguvu, uwezo wa kujaribu mambo na ni ishara ya kuwa mwanaume kamili," Byrnes alibaini.
Ikiwa utachagua pilipili kwasababu unataka muwasho , au unayechukia chakula kisicho na pilipili, au unafuata mila za kale za kutunza chakula kisiharibike , kuongezeka kwa uzalishaji zaidi na zaidi wa pilipili zenye ukali na ukali zaidi, hatutawahi kukosa kiungo hiki katika chakula chetu kamwe.

Post a Comment

Previous Post Next Post