Mba ni vipande vya ngozi vidogovidogo visivyo hai vinavyobanduka .Hamira
ni jamii ya fangasi ambao hushambulia mwili. Mba ni jamii hiyo. Hali hii
hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa
homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa
kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.
Je, ni vipi hushambulia ngozi?
Maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi wa aina hii
hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni
mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa
nyeupe au nyeusi sana).
Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii
kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi
yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya
ngozi.
Upungufu huo ya rangi ya ngozi si wa kudumu, bali ngozi hurudi
kwenye hali ya kawaida ya rangi yake baada ya muda mrefu kidogo tangu maradhi
halisi yalipokomeshwa. Bila matibabu maradhi haya huchukua muda kupona hivyo
dawa ni muhimu ili mwenye maradhi aweze kupona upesi.
Namna ya kuyatambua
Maradhi haya ni rahisi
kuyagundua ila kutokana na kufanana kwake na maradhi mengine yenye
dalili kama hizi uhakiki wa vimelea vinavyosababisha maradhi haya ni muhimu.
Eneo lililo athiriwa na fangasi wa mba kuwasha.
Nini matibabu yake?
Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi
hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla.
Kutokana na uwezo wake wa kurudia kuambukiza ngozi huwa
inashauriwa kwa aliyewahi kupata maradhi haya kurudia kutumia dawa ya kuua
vimelea vya fangasi mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wowote wa maradhi
kurudia kushambulia.
Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua
vimelea hivi vya fangasi.
Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa
ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za
kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi.
Matokeo baada ya matibabu
Maeneo ya ngozi yaliyobadilika rangi huweza kubaki hivyo
hata baada ya vimelea vya fangasi kuondolewa na dawa.
Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka
yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa
ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi. Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na
kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa
au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa
zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.
Hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi
kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na
madhara huchukua muda mrefu kidogo ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe
basi uvimbe hupotea haraka.
Hali ya kuwashwa kupotea,eneo ambalo limeathiriwa na fangasi waletao mba kuacha kuwasha. kichwani.
Njia ya kuepukana na mba
Utumiapo vifaa vya kunyolea nywele hakikisha vinafutwa vizuri , epuka kuchangia kitu kama chanuo kwa sababu masalia ya mba
huwa yanabaki kwenye vifaa vya nywele endapo vitatumika kwa mtu aliepatwa na
mba.
Tags:
UREMBO