Shida
nyingi zinaweza kuathiri ulimi wako kama vile:
maumivu ,vidonda ,uvimbe ,mabadiliko
katika ladha ,mabadiliko
katika rangi
Dalili
zifuatazo zinaweza kuashiria matatizo ya ulimi:
upotezaji
wa ladha au sehemu kamili au mabadiliko katika uwezo wako wa kuonja tamu,
uchungu,chachu au ladha tamu ,ugumu
wa kusonga ulimi wako ,uvimbe
wa ulimi,
mabadiliko
kutoka kwa rangi ya kawaida ya ulimi wako au viraka vya rangi ambayo ni nyeupe,
rangi nyekundu, nyeusi, au hudhurungi
maumivu
yanaweza kua juu ya ulimi au katika sehemu kadhaa tu za ulimi wako
VIDONDA
VYA ULIMI ni michubuko inayotokea kwenye
mdomo na ulimi. Vidonda hivi husababisha mhusika kupata maumivu kwa maana
kinywa ni moja ya sehemu ya mwili yenye mishipa mingi ya fahamu na wakati
mwingine vidonda katika kinywa husababisha kushindwa kuongea vizuri.
Ingawa
vidonda hukufanya ujisikie vibaya, huwa vinapona vyenyewe ndani ya wiki moja au
mbili. Vidonda vya kinywa hutokea kwenye au ndani ya mashavu, midomo (lips),
ulimi, kingo na kuta za meno pia huweza kusambaa mpaka kwenye koromeo ikiwa
havitatibiwa kwa wakati.
Vidonda
vya mdomo huwa vya duara na hutokea ndani ya kinywa, kwenye ulimi na midomo.
Vinaweza kuvimba na kuwa vyeupe, vyekundu au vya kijivu. Inawezekana kuwa na
kidonda kimoja au zaidi wakati mmoja na kusambaa ndani ya kinywa.
Wakati Gani Unapaswa
Kupata Msaada wa Kitabibu?
Vidonda
mdomoni huwatokea watu wengi kwa kawaida na hupona bila ya matibabu ya daktari
wa kinywa. Ikiwa vidonda vitatudumu zaidi ya wiki tatu, zungumza na daktari.
Ikiwa
vidonda vitauma na vitakufanya ushindwe kula, kunywa au kusukutua meno. Ikiwa
vidonda vinajirudiarudia, au vidonda vinapokuwa na maumivu zaidi au vyekundu
kitu kinachoweza kuashiria maambukizi ya bacteria.
Vidonda
kwenye kinywa vinaweza kuwa moja ya dalili ya ugonjwa unaosababishwa na virusi
unaoathiri mikono, miguu na mdomo. Ugonjwa huathiri zaidi watoto chini ya miaka
10 wakati mwingine huathiri hata watu wazima.
Matibabu yanaweza
kupunguza uvimbe na kuondoa wasiwasi. Vitu unavyoweza kufanya kuharakisha
uponaji wa vidonda ni pamoja na
kupaka dawa kwenye vidonda, kutumia mswaki
laini kusukutua meno, ktumia dawa ya meno isiyo na sodium laryl sulphate ambayo
inaweza kukereketa, kutotumia vyakula vyenye viungo vingi na chumvi nyingi.kula
matunda na mboga za majani.
Nini
Husababisha Vidonda kwenye Kinywa?
Mara
nyingi chanzo cha vidonda kwenye kinywa si cha moja kwa moja. Mara nyingi
kidonda kimoja kwenye kinywa husababishwa na uharibifu wa utando laini ndani ya
kinywa kwa mfano unapojing’ata kwa bahati mbaya au unapokula chakula kigumu.
Haijulikani
wazi ni nini husababisha vidonda kwenye kinywa ambavyo hujirudia mara kwa mara,
lakini vitu vinavyochochea ni pamoja na msongo, wasiwasi, mabadiliko ya homoni,
mfano, baadhi ya wanawake hupatwa na vidonda mdomoni wanapokuwa kwenye siku
zao, ulaji wa baadhi ya vyakula mfano vyenye viungo vingi, kahawa, nyanya na
unga wa ngano.
Kutumia
dawa ya meno yenye sodium lauryl sulphate na kuacha kuvuta sigara ghafla, wengi
wanaoacha kuvuta sigara kwa mara ya kwanza wanaweza kupatwa na vidonda mdomoni.
Chembe za urithi pia zinahusishwa na kupatwa na vidonda mdomoni, angalau asilimia
40 ya watu wanaopatwa na vidonda mdomoni wameripoti kurithi kutoka kwenye
familia zao.
Vidonda
vya kinywa wakati mwingine husababishwa na magonjwa yanayosababishwa na virusi
kama tetekuwanga, magonjwa ya fangasi, magonjwa ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula
(Crohn’s Disease, Coeliac Disease), ugonjwa wa kuvimba sehemu za maungio za
mwili (Reactive Arthritis), ugonjwa wa kuvimba mishipa ya damu (Behcet’s
Disease), kinga ya mwili kudhoofu kutokana na VVU au Lupus, upungufu wa vitamin
B na madini chuma.
Pia,
Vidonda vya Kinywa vinaweza kusababishwa na matumizi ya dawa mbalimbali kama za
kutibu magonjwa mbalimbali mfano kupanda kwa shinikizo la damu na dawa za
kutuliza maumivu mfano ibuprofen.
Ninawezaje Kuzuia
Vidonda vya Kinywa?
Inaweza
kuwa ngumu kuzuia Vidonda vya Kinywa kwa sababu mara nyingi husababishwa na
vitu ambavyo huwezi kuvizuia mfano chembe za urithi na maradhi mbalimbali.
Ingawa kufanya yafuatayo kunaweza kupunguza hatari ya kupata Vidonda vya Kinywa
mfano kuepuka vyakula fulani kama vyenye viungo vingi, kahawa au chokoleti na kula
lishe bora.
Epuka
kula vyakula vya moto au baridi sana ikiwa una vidonda tayari kwa maana
huchelewesha kupona kwa vidonda, kula matunda kwa wingi na mboga za majani ili
kuongeza vitamin na madini chuma vitu vinavyoongeza kinga ya mwili, kutotafuna
chingamu, kusukutua meno yako na mswaki laini, kutumia dawa ya meno isiyo na
sodium lauryl sulphate, kupunguza msongo na wasiwasi.
Tags:
MAGONJWA YA KINYWA