Moyo wako unaweza kuharibika baada ya kupokea taarifa ya kusikitisha na hii inaweza kusababishwa na ubongo, wataalam wanaamini.
Watafiti wa Uswizi wamekuwa wakiwafanyia uchunguzi watu wenye madhara ya kiafya yasiyo ya kawaida na ambayo hujitokeza kwa nadra wakati mtu anapopokea taarifa ama kushuhudia mambo ya kusikitisha yajulikanayo kama 'broken heart syndrome' kwa lugha ya kitaalam.
Hali hii hudhoofisha na kuufanya moyo ushindwe kufanya kazi yake vema hutokea ghafla, mara nyingi baada ya tukio la kusikitisha au lililogusa hisia kama vile msiba.
Ni ugonjwa ambao unafahamika kwa kiwango kidogo, lakini taarifa zilizochapishwa kwenye jarida la afya la afya zinasema ubongo unavyopokea taarifa za kushtua huchangia hali hii.
Kushindwa kuvuta pumzi na maumivu
Yakifahamika pia kama maradhi ya takotsubo -kuelezea umbo la moyo kwa watu wenye hali hii, linalofanana na chungu cha Wajapan chenye jina hilo, tmaradhi ya broken heart yanaweza kusababishwa na mshituko.
Ni tofauti na ugonjwa wa kiharusi ambao husababishwa na kuziba kwa mishiba ya damu, lakini huwa na dalili zinazofanana, ikiwemo ile ya kukosa pumzi na maumivu ya kifua.
Mara kwa mara matukio yasiyo ya kufurahisha husababisha hali hii, lakini matukio makubwa ya kusisimua, kama vile harusi au kazi mpya pia vimehusishwa na maradhi haya.
Baadhi ya watu huwa hawawezi kuyapata, au kuwa na uwezo wa kutambua tukio halisi lililosababisha hali yenyewe.
Inaweza kuwa ni hali ya muda, huku misuli ya moyo ikipona yenyewe taratibu kwa siku kadhaa, wiki au hata miezi, lakini kwa baadhi wanaweza kufa.
inakisiwa kuwaathiri watu wapatao 2500 huathirika na ugonjwa huo kila mwaka nchini Uingereza.
Chanzo hasa cha maradhi hayo hakijajulikana, lakini wataalamu wanasema hali hii inaweza kuwa na uhusiano na kupanda kwa viwango vya homoni za msongo wa mawazo ,kama vile homoni aina ya adrenaline.
Nadharia kuhusu maradhi ya mshituko utokanao na matukio
Daktari Jelena Ghadri na wenzake katika chuo kikuu cha Hospitali ya Zurich alichunguza kile kilichokuwa kukutokea katika ubongo wa wagonjwa 15 wenye hali ya mshituko wa damu utokanao na matukio.
Makovu ya ubongo yaliyoonekana kwenye skaniyalionyesha tofauti za wazi yakilinganisha na picha za skani miongoni mwa watu 39 wenye afya, kulinga na kiyuo cha udhibiti wa wagonjwa.
Kuna mawasiliano machache baina ya maeneo ya ubongo yanayohudika na udhibiti wa hisia za mtu na kutokuwa na ufahamu au uelewa wa mwili wa matukio, kama vile mapigo ya moyo.
Sehemu hizi za ubongo ndizo zinazokisiwa kudhibiti namna tunavyokabiliana na msongo wa mawazo.
Dkt Ghadri alisema: "Hisia hutengenezwa katika ubongo kwa hiyo ni kweli kwamba chanzo cha ugonjwa katika ubongo kinaweza kuuathiri ubongo."
Bado jibu kamili halijapatikana, kwa hiyo kazi kubwa inahitajika kufanyika: Makovu ya mgonjwa ya ubongo ya kabla au wakati yanaposababisha maradhi ya mshituko utokanao ya matukio ya kimaisha hayakupatikana, kwa hiyo watafiti hawawezi kufahamu iwapo kupungua kwa mawasiliano baina ya maeneo ya ubongo kulisababisha matatizo ya moyo ya takotsubo au kinyume chake.
Joel Rose, mkurugenzi mkuu wa taasisi ya magonjwa ya moyo nchini Uingereza ,alisema: " Hii ni sehemu muhimu ya utafiti ambayo itasaidia katika mwongozo wa uelewa wetu wa aina ya matatizo ya afya ya moyo ambayo kwa kawaida yanasahaulika na kubakia kutoeleweka.
" Watu wenye matatizo ya afya ya moyo ya takotsubo ambao tunawasaidia wataafiki juhusu hizi mpya za kuelewa nafasi ya ubongo katika kusababisha hali hii na ni kwanini watu wengi zaidi wana mashaka kuliko wengi juu ya suala hili.
Tunatumai kwamba utafiti huu utawezesha kuangaziwa zaidi kwa eneo hili na ushirikiano baina ya wanasayansi wa upasuaji na madaktari wa moyo "
Muasisi wa Wakfu wa utafiti wa tiba ya moyo nchini Uingereza Prof Dana Dawson, kutoka Chuo kikuu cha Aberdeen, amesema "Matokeo haya yanaunga mkono kitu ambacho kwa muda mrefu tumekuwa tukikishuku - kwamba kuna mawasiliano kati ya moyo na ubongo katika kusababisha maradhi ya takotsubo."
Tags:
MOYO