Fahamu mambo matano usiyoyajua yanayosababisha kiharusi

mwanamke mwenye ugonjwa wa moyoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHuenda kuna mambo yanayoathiri moyo wako usiyo yatambua
Sote tunafahamu kwamba tumbaku ,unene wa mwili kupita kiasi na ukosefu wa mazoezi vinaweza kuongeza uwezekano wako wa kupata kiharusi.
lakini kuna mambo mengine ambayo huenda hujawahi kuyasikia yanayoweza kusababisha maradhi hayo.
Maradhi ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo kwa mujibu wa data zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Tuangalie baadhi ya hatari zilizofichika.
1. Kutosafisha meno
Mwnaamume akisafisha menoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMoyo hushukuru unaposafisha meno yako
Meno yetu na mioyo yetu vina uhusiano mkubwa.
Uchunguzi kadhaa umeonyesha kuwa wenye afya mbaya ya kinywa wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya moyo.
Fizi zenye majeraha huwawezesha bakteria kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.
Zinaweza kusaidia kukwama kwa mafuta kwenye mishipa ya damu.

Zinaweza pia kusababisha ini kutengeneza viwango vikubwa vya aina fulani za protini ambazo hujeruhi mishipa ya damu.
Vidonda hivyo hatimae vinaweza kusababisha mshituko wa moyo au kiharusi.
Je kuna suluhu? piga mswaki na tumia uzi kusafisa mianya iliyopo kati kati ya menona mtembelee daktari wa meno
2. Chuki dhidi ya bosi wako
Mwanamke mwenye msongo wa mawazo unaosababishwa na bosi wakeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchunguzi uliofanyika nchini Uswisi unaonyesha ongezeko kubwa la magonjwa ya moyomiongoni mwa watu wanaopatwa na msongo wa mawazoSwedish study showed a significant increase in heart disease for people stressed at work
Si jambo la mzaha - kumchukia bosi wako kunaweza kukusababishia matatizo ya afya ya moyo.
Utafiti uliofanywa kwa miaka 10 nchini Uswisi na kuchapishwa kwneye jarida la tiba la Uingereza- British Medical Journal ulibaini kwamba uhusiano mbaya na kiongozi wako kazini huongeza uwezekano wa shinikizo la damu kwa asilimia 40% ya watu.
"Kiharusi kinaweza kusababishwa na msongo wa mawazo kazini," anasema Vijay Kumar, daktari bingwa wa moyo katika taasisi ya afya ya moyo ya Orlando nchini Marekani.
Pamoja na sababu nyingine kama vile kutopata usinginzi wa kutosha na chakula kisichofaa husababisha uwezekano wa maradhi hayo hata zaidi.
3. Tukio linaloshitua
Mwanamume ambaye amepokea taarifa mbayaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTukio la kushitua linaweza kukusababishia kiharusi
Taarifa ya ghafla inayokushitua mfano kifo cha mtu wa familia yako inaweza kukusababishia kiharusi.
Kwa mujibu wa shirika la afya ya wanawake waliotimiza umri wa kutoweza kupata ujauzito nchini Marekani , mishipa ya damu miongoni mwa wanawake ambao wamewahikupitia matukio matatu ya kushitua maishani mwao, uwezo wao wa kufanya kazi ni mbaya wakilinganishwa na wanawake ambao hawajawahi kupitia uzoefu huo.
Daktari bingwa wa moyo Jackie Eubany anasema kwamba kiwango cha juu cha msongo wa mawazo kinaweza kuongeza hatari kubwa kwa kusababisha kuongezeka kwa kazi ya mapigo ya moyo na hivyo kusababisha kiharusi.
4. Kujihisi mpweke
Mwanamume mpweke mwenye maumivu ya kifuaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUpweke unaweza kuathiri vibaya moyo wako
Jarida jingine la kitabibu la Uingereza linaonyesha kuwa watu wenye mahusiano ya kijamii na watu wachache wanakabiliwa na uwezekano wa asilimia zaidi ya 29% ya kupatwa na maradhi ya moyona asilimia 32% zaidi ya uwezekano wa kupata kiharusi.
Moja ya sababu za athari za za upweke ni kwamba husababisha msongo wa mawazo na watu walio na upweke hawana mtu wa kuwasaidia kukabiliana na hisia zao.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Oxford na kuchapishwa mwaka 2014 uliowahusisha wanawake zaidi ya 700,000 kwa zaidi ya miaka minane, ulibaini kwamba watu wanaoishi na wenzi wao walikuwa na uwezekano wa chini ya asilimia 28% wa kufa kwa maradhi ya moyo kuliko wanawake wanaoishi peke yake.
5. Msongo wa mawazo
Mwanaume akiwa pamoja na DaktariHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMsongo wa mawazo unaweza pia kuathiri afya yako ya mwili.
Shirika linalojishughulisha na masuala ya afya ya moyo linasema kuwa 33% ya wagonjwa wa shinikizo la damu nchini Marekani hupata ugonjwa huo kutokana na msongo wa mawazo.
Wataalamu wanashuku kwamba watu wenye matatizo ya afya ya akiliwanaweza kuhisi ugumu wa kuchukua maamuzi ya kiafya.
Nieca Goldberg, mkurugenzi katika kituo cha afya ya wanawake cha New York cha Joan H. Tisch, anasema tabia kama ya kula chakula chenye virutubisho vya mwili au kuwa na kikomo cha kiwango cha unywaji wa pombe inaweza kuwa ni jambo gumu kwa watu wenye msongo wa mawazo.
6. Kipindi cha kutoweza kupata ujauzito The menopause
Mwanamke akinywa chaiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionkupungua kwa homoni kunakosababishwa na kipindi cha kutoweza kupata ujauzito huathiri mfumo wa moyo wa mwanamke
Wanawake wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kupata shinikizo la damu katika miaka ya baada ya kipindi cha kutokuwa na uwezo wa kupata ujauzito.
huenda hii ikawa na uhusiano na kupungua kwa homoni asilia za uzazi katika miili yao.
inaaminiwa kuwa homoni aina ya estrogen zina athari chanya kwenye kuta za mishipa ya damuj inayosaidia afya ya mishipa ya damu.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Jackie Eubany anaongeza kuwa umri huifanya mishipa ya damu kukakamaa jambo linalosababisha msukumo wa kiwango kikubwa wa damu.
Hata hivyo, lishe bora na mazoezi ya mwili ya mara kwa mara vinaweza kusaidia kukabiliana na athari hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post