MAUMIVU YA NYONGA.

Watu wengi wamewahi kusumbuliwa na tatizo hili la maumivu ya nyonga kwa kipindi fulani katika maisha yao. Yaweza kuwa ni dalili za matatizo ya hedhi, constipation, kukua kwa tezi dume,na  matatizo ya neva. Kwa watu wachache tatizo linaweza kuwa sugu hadi kupeleka kukwamisha shuguli zao za kimaisha kama kunyanyua mizigo na kutembea vizuri au kufanya tendo la ndoa kwa uzuri.
Asilimia 60 ya watu wanaopata maumivu sugu ya nyonga bado hawajapatiwa ufumbuzi kufahamu nini kinasababisha maumivu haya kitu ambacho kinaleta wasiwasi kwa mgonjwa sababu atashindwa kujua hatima yake. Kwa mgonjwa kufahamu kinachosababisha maumivu haya ni jambo la msingi zaidi ili ujue tiba sahihi ya kukufaa.

Maumivu ya nyonga ni nini?

Kwa ujumla hakuna njia moja inayoweza kuelezea maumivu haya, ni maumivu yanayotokea sehemu katikati ya tumbo na eneo la hips , kwa baadhi ya watu maumivu yanaweza kuanzia kwenye eneo la chini ya mgongo na kusambaa hadi kwenye eneo la nyonga. Kwa upande wa mwanamke maumivu yanaweza kutokana na shida kwenye uzazi sababu mfumo wa uzazi wa mwanamke upo kwenye nyonga. Maumivu haya ya nyonga yanaweza kumpata mwanamke, mwanaume na hata watoto pia.

Dalili za maumivu ya nyonga

Maumivu ya nyonga siyo ugonjwa bali ni dalili ya uwepo wa tatizo la kiafya. Maumivu haya yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na hutokea kweye nyonga na chini ya tumbo.
Dalili za maumivu  ya nyonga hutofautiana kwa wagonjwa, wengine hupata maumivu mepesi na wengine hupata maumivu makali. Kwa baadhi ya watu maumivu huweza kuwa makali hadi kupelekea kukwamisha shughuli za kimaisha kama mazoezi, kutembea na tendo la ndoa. Kwa ujumla maumivu ya nyonga huambatana na matatizo mengine kama kushindwa kufanya tendo la ndoa vizuri.

Nini kinasababisha maumivu ya nyonga?

Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya nyonga kwa wanawake na wanaume. Inaweza kuwa ni maambukizi, ama athari kwenye viungo vya ndani kama kibofu cha mkojo, utumbo mpana, kwa wanawake yaweza kuwa ni shida kwenye uzazi. Hapa chini ni maelezo sababu kuu zinazopelekea maumivu ya nyonga.
  • Constipation: kukosa choo ama kupata choo kigumu kwa muda mrefu husababisha maumivu ya nyonga kutokana na presha na kujaa gesi kwa tumbo. Constipation yaweza kusababishwa na lishe mbaya, msongo wa mawazo, matatizo ya homoni, upungufu wa madini ya magnesium, kupungua kwa bacteria wazuri tumboni na kutoshugulisha mwili. Kwa kutumia package yetu ya digestive care unaweza kupona tatizo lako la constipation na kuimarisha afya ya tumbo. bonyeza hapa kuanza huduma ya virutubisho asili.
  • Matatizo ya kibofu cha mkojo: kibofu kinapopata hitilafu hupelekea kuvimba kwa tishu zake na kusababisha maumivu kwenye eneo la nyonga. Ugonjwa wa kibofu uitwao interstitial cystitis, ambao huletekeza dalili za UTI ni moja ya matatizo yanayosababisha maumivu ya nyonga.
  • Matatizo ya figo: matatizo kama maambukizi kwenye figo au mawe kwenye figo husababisha maumivu ya nyonga. Tatizo la mawe kwenye figo husababisha maumivu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka kwenye eneo la nyonga.
  • Hernia: hernia hutokana na kutofunga kwa eneo la chini ya tumbo na kupelekea kukua kwa tishu kukua kuelekea eneo la uzazi. Hernia husababisha maumivu makali ya nyonga.

    Maumivu ya nyonga kwa wanawake

Maumivu ya nyonga kwa wanawake yanaweza na shida kwenye uzazi. Matatizo haya yanaweza kutokea kwenye viungo kama uke, shingo ya kizazi, mirija ya uzazi, mifuko ya mayai au mfuko wa mimba. Inawezekana pia kupata maumivu kutokana na sababu zaidi ya moja, sababu hizi zinaweza kuwa
  • Endometriosis : endometriosisi ni kitendo cha kukua kwa ukuta wa ndani(endometrium) wa mfuko wa mimba kuelekea nje ya mfuko wa mimba. Pale tishu zinapokua na kuwa nene husababisha dalili kama maumivu ya nyonga, maumivu kpindi cha hedhi, tumbo kujaa gesi na maumivu ya chini ya mgongo.
  • Fibroidsfibroids ni uvimbe usio saratani unaotokea ndani ya kuta za mfuko wa mimba. Tafiti zinasema kwamba karibu asilimia 40 mapaka 80 ya wanawake hupata shida ya fibroids katika uzazi kwenye maisha yao.
  • PIDpid ni maambukizi kwenye njia ya uzazi ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na magonjw aya ngono kama chlamydia au gonorrhea. Dalili kubwa ni maumivu ya nyonga, maumivu wa wa tendo ndoa, maumivu wakati wa kukojoa, na kutokwa na uchafu ukeni kusiko kawaida.
  • Ovarian cysts: ovarian cysts ni mkusanyiko kwa vimbe ndogo ndogo zilizojaa maji kwenye mifuko ya mayai ya mwanamke. Kwa wanawake wengi vimbe hizi hazileti shida na huweza kupotea baada ya muda. Lakini kwa baadhi ya wanawake vimbe zinapokuwa kubwa huleta maumivu ya nyonga na kuvurugika kwa hedhi.
  • Kutoa mimba: dalili kubwa zinazotokea baada ya kutoa mimba ni kama kutokwa na uchafu ukeni usio kawiada, maumivu ya chini ya tumbo, maumivu ya nyonga, kuharisha na wakati mwingine kuzirahi kutokana na kutokwa na damu nyingi.
  • Maumivu kipindi cha hedhi: baadhi ya wanawake hupata maumivu ya nyonga wakati wa hedhi, mumivu haya huitwa dysmenorrhea kwa kitaalamu. Maumivu kipindi cha hedhi ni kutokana na kutanuka kwa misuli ya mfuko wa mimba.Maumivu ya nyonga kwa wanaume
Ukiacha wanawake, wanaume pia hupata tatizo hili la maumivu ya nyonga, hasa wenye tatizo la tezi dume.. kuvimba kwa tezi dume ama maambukizi kwenye tezi dume husababisha maumivu ya nyonga, eneo la haja kubwa, kwenye tumbo la chini na pia maumivu kwenye kibofu. Dalili zingine zinazoonesha kuna shida kwenye tezi dume ni kupata maumivu wakati wa kukojoa ama kupata mkojo kidogo sana . unapoona dalili hizi wahi hospitali mapema ili kupata vipimo na tiba haraka.

ANGALIZO

Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya nyonga na baadhi ya sababu hizi huashiria magonjwa hatari. Weka mihadi na dactari wako ufanye vipimo ili kujua chanzo cha tatizo. Kumbuka maumivu ya nyonga ni dalili na siyo ugonjwa kwahiyo ni lazima kujua ni ugonjwa gani unapelekea maumivu yako ya nyonga. Hivo basi kama unapata maumivu yasiyokwisha pamoja na kutokwa na uchafu ukeni kwa wanawake onana na dactari haraka hasa pale ukiwa mjamzito, maana inaweza kuwa ni dalili ya kutoka kwa mimba.

Post a Comment

Previous Post Next Post