Jinsi ya kuhesabu tarehe ya matazamio ya kujifungua

Picha ya mwanamke aliyetoka kujifungua. Picha na Hubpost

JINSI YA KUHESABU TAREHE YA MATAZAMIO YA KUJIFUNGUA

Kuweza kufahamu tarehe ya makadilio ya mama kujifungua njia tatu zinaweza kutumika kujua umri na kimo cha mimba,
  • Kukokotoa Hesabu
  • Kupima fumbato la mimba.
  • Kipimo cha ultrasound.

KOKOTOA HESABU

Namna ya kuhesabu tarehe ya matazamio

Njia hii ni ya uhakika na inampa mwanamke kujua tarehe ya matazamio ya kujifungua. Mwanamke anatakiwa kujua tarehe yake ili kuweza kupanga mahali pa kujifungulia na kujiweka tayari.

Wastani wa kipindi cha ujauzito ni siku 280 ama wiki 40 kamili

Njia hii hutumika maranyingi kwa mwanamke mwenye mzunguko usio badilika badilika sana na unachukulia mwanamke anaona hedhi baada ya siku 28 ama na katikati ya mzunguko wake ni siku 14. Kwa mwanamke wmenye mzunguko wa siku 35 siku yake ya katikati ni siku ya 21.

Formula inayotumika inaitwa Naegele's rule

Tarehe ya matazamio inagunduliwa,

  • Fahamu tarehe yako ya kuona hedhi yako ya mwisho kabla ya ujauzito.
  • Ongeza 7 kwenye tarehe.
  • Toa 3 kwenye mwezi (ikiwa mwezi ni zaidi ya mwezi wa 3 na kuendelea).
  • Ongeza 9 kwenye mwezi( ikiwa mwezi ni chini ya mwezi wa 4 kushuka chini)
  • Ongeza 1 kwenye mwaka (ikiwa mwezi ni zaidi ya mwezi wa 4)
MFANO
Kama mwanamke mara ya mwisho kuona siku zake ni tarehe 21/3/2018 hivyo tarehe ya matazamio ni,

Siku   mwezi  Mwaka
21           3          2018
+7        +9
28         12          2018

Hivyo tarehe ya matazamio ya mwanamke huyu itakuwa ni 28/12/2018.

Kama siku yake ya mwisho kuona damu ni 21/5/2018

Siku   Mwezi   Mwaka
21           5           2018
+7         -3               +1
28          2            2019.

Hivyo tarehe ya matazamio kwa mwanamke huyu itakuwa 28/2/2019

KUPIMA FUMBATIO

Njia ya Pili ni kupima fumbato la mimba. Wiki ya  20 fumbato huwa usawa wa kitovu.
Hupimwa unapofika kliniki, usijipime nyumbani kwasababu ziko sababu zinazoweza kufanya tumbo kuwa dogo au kubwa na hali hiyo si salama kwa ujauzito wako, kliniki watafanya uchunguzi wa kina na kulitatua.

KIPIMO CHA ULTRASOUND

Njia ya tatu ni kipimo cha ultrasound . Hii ndio njia ambayo huweza kubaini umri wa Ujauzito kwa usahihi zaidi. Hata hivyo mapacha, maji mengi kwenye chupa ya uzazi na uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hufanya namna ya kubaini umri wa Ujauzito kuwa ngumu zaidi.

KUMBUKA

Watoto wengi huzaliwa kati ya wiki 3 kabla hadi wiki 2 baada ya tarehe hii.
Rudia mara nyingi zaidi kujifunza njia hii, kumbuka kufuata hatua na maelekezo, fanya hivyo kulingana na tarehe yako. Kumbuka Muuguzi au mtoa huduma ya afya atakusaidia kukuhesabia tarehe ya makadirio ya kujifungua kwako, usiwe na hofu ukishindwa kukokotoa.

Post a Comment

Previous Post Next Post