Tatizo la kuvimba miguu

KWA WANAOSUMBULIWA NA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU.

Tatizo la kuvimba miguu husababishwa na kujikusanya kwa maji maji ambayo uvuja kutoka katika mishipa ya damu kutoka na sababu mbalimbali zinazosababisha damu ishindwe kurudi kwenye moyo kutoka katika miguu. Hali hii huweza kutokea pia kwenye mapafu, ubongo, tumboni, na kwenye mapaja lakini kutikana na mvuto wa dunia huweza kuonekana zaidi kwenye vifundo vya miguu na bila maumivu.
Mambo yanayochangia na kusababisha tatizo ili mara nyingi huwa ni ujauzito, ugonjwa sugu wa ini, figo, ini na moyo kushindwa kufanya kazi, dawa za kupunguza mfadhaiko na shinikizo la damu. 

MATIBABU YAKE.
Fika hosipitali kama kuvimba miguu inaambatana na kubanwa na kifua, kushindwa kupumua, maumivu makali ya kifua, kuna uvimbe wenye maumivu au joto kali, matatizo ya moyo, ini na figo ambapo dawa za kupunguza majimaji mwilini, kusaidia moyo, ini na figo kufanya kazi zitatolewa kwa kwa maelezo ya wataalamu wa afya.
Unaweza kufanya yafuatayo kujitibu mwenye kabla ya kumuona daktari
Nyanyua miguu yako juu ya usawa wa moyo wakati umelala kwa muda wa dakika 30 ili kuwezesha damu ya kutosha kurudi kwenye moyo. Fanya hivi walau mara 3 kwa siku kupata matokeo bora zaidi
Kufanya mazoezi laini pia itakusaidia kupeleka damu kwenye moyo na hivyo kurekebisha mzunguko wa damu
Wakati unasafiri safari ndefu hakikisha unasimama mara kwa mara.
Epuka kuvaa kwa muda mrefu nguo zinazobana sehemu za mapaja.
Punguza uzito.

Post a Comment

Previous Post Next Post