SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI(CERVICAL CANCER)


Shingo ya kizazi au cervix ni njia ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba. Sehemu hii ina kazi

CERVIX/SHINGO YA KIZAZI

nyingi ikiwemo kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mirija ya uzazi ili kupevusha yai,
kupitisha damu ya hedhi na pia ndio mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa.                       
Kama zilivyo sehemu zingine za mwili, sehemu hii nayo inaweza kupata maradhi ikiwemo kansa.
Ugonjwa huu huwaathiri wanawake wengi wa rika zote walio katika umri wa kuzaa. Miaka ya
nyuma kabla ya maambukizi ya Ukimwi kansa ya shingo ya kizazi ilikuwa ikiwapata zaidi
wanawake wenye umri wa miaka 45 na kuendelea.                       
 Lakini miaka ya hivi karibuni mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa anaweza kupata tatizo hili.
SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI/CERVICAL CANCER
Saratani ya shingo ya kizazi ni mabadiliko ya chembe chembe hai zilizo juu au zinazofanana na shingo ya uzazi ambapo huchukua miaka mingi hadi kujitokeza kwake. Ugonjwa huu huchukua zaidi ya miaka 15 mpaka 20 kugundulika lakini kabla ya kujitokeza bayana hutokea mabadiliko kadhaa
yanayoweza kugundulika mapema na kufanikiwa kuzuilika katika hatua za mwanzoni. Utafiti uliofanywa na timu ya wataalamu wa ugonjwa huo umebainisha mabadiliko ambayo hujitokeza kabla ya maradhi haya katika sehemu ya kizazi  kabla ya kujitokeza saratani yanayoitwa
kitaalamu Precancerous lesion.
 Mabadiko hayoyanaweza kuendelea na kujirudia na mwishowe kuwa ugonjwa. Hata hivyo yapo mambo ambayo yameonekana kusababisha ugonjwa huo kwa wanawake ambapo baada ya kufanyika uchunguzi duniani kote imebainika kuwa ugonjwa huo husababishwa na sababu tofauti.
Uchunguzi huo uligundua kuwa saratani hiyo ya shingo ya kizazi  husababishwa na
kuanza ngono mapema katika umri mdogo chini ya miaka 18,
kuwa na wapenzi wengi na kuvuta sigara.
Pia miongoni mwa mambo yanayochangia kupata saratani ya shingo ya kizazi ni pamoja na
historia ya kubeba mimba nyingi
 unywaji pombe kupindukia huku watu walioathirika na virusi vya Ukimwi wakiwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi hayo.
                      

 SABABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI                       

Ugonjwa huu husababishwa na virusi vinavyoitwa Human papilloma, ambapo mtu anaweza kupatwa na virusi hawa wakati wa kujamiana na mtu mwenye maambukizi.                       
 Watu walio katika hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu ni kwa ujumla wanawake wote lakini zaidi wale wasiokwenda kufanyiwa uchunguzi wa kila mwaka kuhusiana na ugonjwa huu unaojulikana kitaalamu kama pap smear, wanawake walioathirika na virusi vya
human papillomavirus HPV au genital warts,
wanaovuta sigara,
wenye ukimwi na wasiokula vyakula bora hasa wasiozingatia mboga na matunda katika lishe zao uchunguzi huo, timu ya wataalamu wa ugonjwahuo imeeleza sababu zinazochangia kupata
saratani ya shingo ya kizazi na kubainisha dalili ambazo huonekana kwa mtu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo.                       
Kutokana na nuchunguzi huo, timu ya wataalamu wa ugonjwa huo imeeleza sababu zinazochangia kupata saratani ya shingo ya kizazi na kubainisha dalili ambazo huonekana kwa mtu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo.                       
 Kufanyiwa uchunguzi wa pap smear ili kubaini ugonjwa huu kuna nafasi kubwa katika kuzuia
watu kupatwa na saratani ya shingo ya kizazi.
Uchunguzi wa awali wa saratani ya shingo ya kizazi unatakiwa kufanyiwa wanawake walio
katika mahusiano ya ndoa na pia wanatakiwa kupima mara kwa mara hadi wanapofikia umri
wa miaka 69. Mwanzoni uchunguzi huu unatakiwa ufanyike mara kwa mara kwa muda
wa miaka mitatu mfululizo. Ikitokea katika miaka mitatu mfululizo uchunguzi huo haujatoa
dalili zozote za kuwepo saratani basi mwanamke anaweza kuendelea kufanyiwa
uchunguzi mara moja kila baada ya miaka miwili na mitatu hadi pale atakapofikisha umri wa

miaka 69.
VIPIMO VYA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI

Tunapaswa kujua kuwa, uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ni
rahisi na hauna maumivu yoyote tofauti na dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa
huambatana na maumivu yanayotokana na uchunguzi huo na unaweza hufanyika katika
chumba cha daktari au nesi mtaalamu kwa muda wa dakika chache tu.                     

PAP-SMEAR

Pap-Smear ni kipimo ambacho hutumika kuchunguza mabadiliko ya chembe zilizopo katika mlango wa kizazi (cervix) ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo mapema na hivyo kuyakabili mapema, kwani saratani ya shingo ya kizazi inaweza kutibika iwapo itagundulika mapema. Kipimo hicho huangalia shingo ya mfuko wa kizazi kwa kutumia kemikali iitwayo acetic acid, ambayo huwekwa kwa kutumia pamba na mabadiliko ya rangi ya chembe chembe hai zilizopo ndizo zitakazobainisha kuwepo kwa dalili za ugonjwa huo. Endapo kipimo hicho kitaonesha dalili za
mwanzo za ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, kitachukuliwa kipimo kutoka katika sehemu iliyoathirika kwa ajili ya uchunguzi zaidi.                        
Wataalamu wa masuala ya afya wanasema kuwa, asilimia 50 ya wagonjwa wana uwezo mkubwa wa kupona kabisa ugonjwa huu, lakini pengine ikiwa saratani ya shingo ya kizazi haitochukuliwa na
jamii za kimataifa kuwa tatizo kubwa huenda miaka ijayo ukawa ni ugonjwa mkubwa kuliko hata ukimwi na malaria.
JINSI YA KUJIKINGA /PROTECTION FROM CERVICAL CANCER                     
kama wanavyosema wahenga kinga ni bora kuliko tiba, basi tufahamukuwa kwa kujikinga tunaweza kujiepusha na magonjwa mengi na hata ya saratani. Moja ya kinga hizo ni
mke au mume kutokuwa na wapenzi wengi
kulinda tabia zetu na kutofanya ngono zembe.
mke au mume kutokuwa na wapenzi wengi
kutozaa sana na kutovuta sigara
kutoanza tendo la ndoa katika umri mdogo,
 kufanya uchunguzi mara kwa mara,
Tumia neplily pads kwa afya bora ya kizazi  
Kufanya vipimo mara kwa mara 
Pia ugonjwa huu huweza kuzuilikakwa chanjo inayojulikana kana HVP vaccine,ambayo hupunguza hatari ya kutokea mabadilikoya seli na kuwa saratani.                                           

MATATIZO YA KANSA YANATIBIKA UKIWAHI MAPEMA

Kansa ya shingo ya kizazi inatibika iwapo itagundulika mapema ikiwa katika hatua za mwanzo. Hii ni katika hali ambayo ugonjwa huu unapogundulika katika hatua za mwisho, uwezekano wa kutibika huwa mdogo na gharama za matibabu kuwa kubwa. Kuna njia za kutibu saratani ya shingo ya kizazi ambayo haijaanza kuonesha dalili ikiwa ni pamoja na
kutumia barafu maalumu na pia njia ya upasuaji mdogo wa kuondoa uvimbe. Pamoja na njia hiyo ya kutibu saratani ya awali pia ipo tiba maalumu ya saratani ya shingo ya kizazi ambayo ni pamoja na upasuaji katika hatua ya mwanzo ya ugonjwa, mionzi pamoja na njia ya dawa inayohusisha matumizi ya kemikali maalumu za kutibu saratani au chemotherapy.                        
 Matibabu ya mionzi na dawa hutegemea umri, afya na hatua ambayo ugonjwa umefikia. Baadhi ya wakati wagonjwa hutolewa kizazi wakati wa upasuaji ili
kutibu aina hii ya saratani hasa wakati ikiwa imesambaa kwenye kizazi chote.

MATIBABU KWA KUTUMIA DAWA ASILIA

Mmea wa ginseng na pia ganda la nyanya baada ya uchunguzi wa kisayansi yamebainika kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na kansa aina zote kwa kutibu na kukinga seli,dawa zilizotengenezwa kwa mmea huu hazina kemikali kabisa hivyo ni salama kwa afya ya mtumiaji
Tukiangalia ganda la nyanya limefanyiwa uchunguzi kwa uwezo wake mkubwa wa kupambana na kansa shid ikawa ni kwamba mtu anapotumia nyanya halifyonzwi linatoka ndipo ikatumika teknolojia ya hali  ya juu kulifanya katika mfumo ambao litaweza kufyonzwa na mwili
Mmea wa ginseng wenyewe una chembe ndogo sana za kitabibu ambazo zinapenya sehemu zote za mwili hivyo kutoa tiba kwa ugonjwa wa kansa na magonjwa mengine
Mimea hii ikawekwa kitaalam katika mfumo wa vidonge kwa ajili ya matibabu
Na dozi yake ni kwa muda wa miez mitatu mfululizo

chanzo KOROTITZ
REVIEWED

Post a Comment

Previous Post Next Post