Sindano za kuimarisha uume ambazo zimebuniwa kuongeza ukubwa wa uume zimepata umaarufu mkubwa licha ya tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusu madhara ambayo yanaweza kujitokeza mtu anapotumia dawa hizo.
Wanaume wawili waliiambia BBC, kwa nini hawaoni aibu kutumia njia hiyo.
Abdul Hasan, 27,ni mteja mzuri wa sindano hizo za kuimarisha uume na kuufanya uwe na muonekano mzuri.
Kwa sasa ameanza jitihada hizo ili iwe zawadi itakayomstaajabisha rafiki yake wa kike.
Amekuwa na rafiki yake huyo wa kike kwa miaka minane lakini wazo hilo bado liko akilini kama atamridhisha kimwili au la.
Mara ya mwisho kutumia sindano hizo ,mchumba wake alifurahi kwa asilimia 100, mwanaume huyo anayetumia dawa ya kuimarisha uume alieleza katika kipindi cha Victoria Derbyshire.
"Nilifikiri kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuumia kutokana na jambo hilo, kwa sababu kadhaa huwa nafurahia kutumia njia hiyo ", aliongeza.
Dawa ya kuimarisha uume ni mmiminiko wa asidi ambao uko kwenye mfumo wa sindano ambayo huchomwa chini ya ngozi ya uume.
Hakuna upasuaji ambao unafanyika na zoezi hilo linaweza kufanyika kwa masaa tu katika kliniki na hugharimu Euro 3000 tu kwa mara moja.
Dawa hiyo ambayo imebuniwa kuongeza ukubwa wa uume na kuufanya kuwa na muonekano mzuri.
Kwa kawaida huongezeka kwa sentimita moja au mbili na vilevile inategemea na kiasi cha dawa inayochomwa.
Mtu akichoma mara moja inaweza kudumu kwa kipindi cha miezi 18.
Aina hiyo ya matibabu bado ina kanuni chache ambazo zinazoiongoza.
Asif Muneer,kutoka jumuiya ya wapasuaji wa njia ya mkojo Uingereza anasema kuwa hawezi kuwashauri watu kufanya hivyo.
Ongezeko la zoezi hili lipo zaidi katika kuongeza upana wa uume na haiongezi urefu hivyo kiuhalisia haiwezi kuimarisha tendo hilo.
Kama kitu chochote kitapelekea kuleta madhara basi itakuwa baada ya kufanya mapenzi.
Muneer anaamini kuwa kuna wengi ambao wanataka kujua namna ambavyo dawa hizo zinaweza kufanya kazi mara baada ya kuona watu maarufu na wasanii wakitangaza upasuaji wa mapambo katika mtandao.
'Hakuna cha kuficha'
Kwa upande wake Abdul, kutojiamini ndio sababu iliyomfanya atake kupewa kiwango cha miligramu 10 za dawa ya kuimarisha uume.
Uume wake uko katika ukubwa na urefu ulio sawa lakini bado huwa anaona akiwaona wanaume wengine wanapotembea bila nguo katika chumba cha mazoezi.
Anadai kuwa mara ya kwanza kutumia dawa hiyo ya kuimarisha uume, ilimfanya ajiamini zaidi ingawa anakiri kuwa aliogopa kupata madhara,
"Nilipotumia dawa hiyo,nilianza kujiamini tena.Sikuwa na cha kuficha tena" alisema.
Mwanaume huyo aliongeza kuwa baada ya siku kadhaa alijisikia afadhali katika sehemu za mjumuiko.
"Nimebadilika, kama nikiona kundi la watu nnaweza kujumuika nao".
Makampuni mawili makubwa ya vipodozi nchini Uingereza yanayoangazia afya ya ngono yamesema katika kipindi cha Victoria Derbyshire kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la utafiti juu ya sindano zinazoimarisha uume.
Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la utafiti ambapo kunakadiriwa kuwa na tafiti 700 kwa mwezi ukilinganisha na kiwango cha miaka mitatu iliyopita ilikuwa ndogo ndani ya miezi 10.
Vilevile Muneer alidai kuwa kuna wanaume wengine ambao huwa wanajichoma sindano wenyewe ili kuimarisha uume wao kwa kutumia mafuta ya mgando kama Vaseline na hawafahamu juu ya madhara ambayo wanaweza kuyapata.
Wengi huwa wanaenda kwa madaktari lakini baada ya siku chache huwa wanakuja kutaka kutibiwa madhara madogo ambayo hujitokeza.
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 36 ,Stuart anadhani kuwa wanaume wote wanaweza kupata uume mkubwa wakitaka.
"Sidhani kama ninahitaji kutumia dawa hizo ingawa itaweza kuniongezea kujiamini zaidi", alisema.
"Ningejisikia vizuri zaidi kama uume wangu ungekuwa mkubwa zaidi".
Stuart alipenda wazo hilo la kuimarisha uume bila ya kufanyiwa upasuaji baada ya kuona tangazo la biashara kuhusu dawa hiyo.
Imani potofu juu ya uume mkubwa
Utafiti wa mwaka 2015 uliofanywa katika chuo kimoja mjini London iliangalia urefu na upana wa uume kwa wanaume zaidi ya 15,000 duniani kote.
Kitaalamu uume unapaswa kuwa na inchi 5.1 yaani sentimita 13 wakati unaposimama.
Ni 5% peke yake ya wanaume ndio walikuwa na uume wa urefu wa zaidi ya inchi 6.3, wakati 0.14% wakiwa na uume mdogo sana kuliko kawaida ambao ni wa urefu wa chini ya inchi tatu ukisimama.
Kwa upande wa kipimo cha mzingo cha uume (ukubwa wake kwa kuangalia mzunguko ambacho ni kipimo cha kukadiria upana wake), kiwango cha kawaida huwa inchi 3.6 (sentimita 9) ukiwa haujasimama, na inchi 4.6 uume unaposimama.
Stuart aliamua kuweka kimiminika cha milimita 15 ambacho ni kiwango cha mwisho ambacho mtu hupewa katika kliniki.
Mchumba wake Stuart amekiri kuwa ana hofu utakuwa mkubwa sana.
"Nina furaha sana kwa sababu naona kuwa umeongezeka," ameeleza Stuart.
Abdul yeye aliongeza kutoka sentimita 10 mpaka 11.5.
Daktari amewashauri wanaume kusubiri wiki nne kabla ya kufanya mapenzi tena kwa usalama wao kitu ambacho Abdul anakizingatia.
Viambata hivyo vinaweza kutolewa na uume kurudi katika hali yake ya awali kwa malipo ya ziada.