Je unajua usalama wa lipstick upakayo?


Kila uchao baadhi ya wanawake hupakaa rangi za mdomo maarufu kama lipstiki ikiwa ni sehemu ya kuendea urembo na umaridadi wa mwili.


Aina hii ya vipodozi inayopakwa kwenye ngozi ya nje ya mdomo inakuja katika sampuli na rangi tofauti japo maarufu zaidi ni zile za rangi nekundu, na zipo ambazo hung'arisha mdomo bila kuwa na rangi yeyote.
Kuna ambazo huvumilia maji yaani water proof kwa lugha ya kingereza. Zipo za maji, za mafuta na kavu. Baadhi hutoka kila unapokula nyingine hudumu mpaka kwa saa 24.



Gharama za bidhaa hizo hutofautiana na mahali mteja amenunua na pia ubora. Nchini Tanzania, zipo lipstiki za bei nafuu mpaka kuanzia Sh500 ambazo hizi hupatikana mitaani na minadani. Lakini pia zipo za bei ya juu mpaka Sh50,000 na zaidi, ambazo huuzwa kwenye maduka makubwa na hutangazwa kuwa ni halisia.

Kuna kila aina ya Lipstiki, zipo za maji,kavu na za mafuta.
Changamoto kubwa katika bidhaa hizo ni ubora na usalama, kwani zipo ambazo huaminika wazi wazi kuwa si salama yaani sio halisia na ndio hupatikana kwa bei rahisi zaidi. Lakini zile za bei ya juu zaidi hutangazwa kutoka uingereza ndio yasemekana ni halisi zaidi.
Watumiaji wengi wameiambia BBC kuwa bei ndio huwa kigezo kikuu wanachoangalia ili kubaini ubora wa urembo huo.
Lakini je bei ndio kipimo pekee cha ubora?
BBC imezungumza na Gaudensia Simwanza ambaye ni meneja mahusiano na elimu kwa umma kutoka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) juu ya usalama wa bidhaa hizi za urembo wa mdomo ambazo mara nyingi huingia kinywani hasa wakati wa kula au kunywa.
"Bidhaa lazima isajiliwe, kupitia usajili ndo tunaamini kua mtu anaweza tumia bila kupata madhara, kwasababi kuna vitu tunaangalia katika usajili mfano uhalali wa bidhaa, taarifa zilizo wekwa je ni sahihi, iliko toka je imesajiliwa? Pia tunaang alia ubora wa bidhaa yenyewe na vifungashio vyake kwa sababu tuna viwango vyetu. Viungo vilivyo wekwa kwenye bidhaa vimewekwa kwenye lebo na je viungo hivyo ni salama? Kuna wengine husema bidhaa imetoka kwenye kiwanda hiki kumbe kiwanda hicho hakipo. Baada ya hapo lazima bidhaa tupeleke maabara kwaajili ya vipimo."


Hata hivyo ameongeza kuwa zipo baadhi ya bidhaa zina viambata ambavyo haviruhusiwi nchini Tanzania hivyo huzuiliwa. Bi Gaudensia pia ametoa rai kwa watumiaji wa urembo huo kununua bidhaa kwenye maduka yanayoeleweka.
"Tunaangalia sifa za kikemikali na kibaiolojia, katika viambato tunaangalia kama vilivyo tumika ni salama kwa sababu kuna baadhi ya viambato ambavyo havitakiwi kama vile steroid, mercury compound, hydroquinone na vinginevyo. Na bidhaa ambazo tumezisajili unazikuta zipo kwenye tovuti yetu, lakini kikubwakwa mtu wa kawaida tunamwambia nunua kwenye maduka ambayo yana tambulika, kwa sababu unanunua kwenye maduka rasmi inakusaidia hata ukipata tatizo unarudi hapo tofauti na hkununua mtaani au zilizo wekwa chini kesto ukija huta mkuta," Gaudensia anaiambia BBC
Mwaka 2007 ilifanyika tafiti kupitia kampeni ya vipodozi salama huko Marekani iliyo itwa "A poison Kiss" yaani busu lenye sumu. Utafiti huo uligundua kemikali ya lead kwenye asilimia 61 ya lipstick 33 zilizo fanyiwa utafiti.
Wataalamu wa dawa wanasema hakuna kiwango cha kemikali ya lead ambacho ni salama kwenye damu.
Mwanafunzi aliyejilipia karo kwa kumtengenezea Lil Wayne mkufu
Hata hivyo utafiti huo unasema hakuna lipstiki ambayo imeorodhesha kemikali ya lead kuwa sehemu ya kiungo chake. Kiwango chake ni kidogo lakini uwepo wa kemikali hiyo katika lipstiki ama shedo ambayo hupakwa na kunyonywa kupitia ngozi inaleta wasiwasi wa usalama wa bidhaa za urembo ambazo hutumiwa na wanawake wengi duniani.
Hata hivyo katika utafiti uliofanywa na mamlaka ya chakula huko marekani, waligundua kemikali ya ulead katika lipstiki au shedo zote 400 walizo zifanyia utafiti. Kiwango chake kilikuwa kikubwa maranne zaidi ya utafiti wa kampeni ya vipodozi salama.
Lakini pia utafiti wa Chuo kikuu cha Calfonia wao walichunguza lipstiki nane na lipshine 24 na walikuta chemikali zingine ambazo ni sumu kama vile chromium, cadmium, manganese, aluminum na hiyo lead.
Kemikali ya Lead inamadhara gani?
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, kemikali ya lead ina sumu ambayo huathiri mifumo mingi ya mwili wa binadamu. Na zaidi ni sumu kwa watoto. Kemikali hiyo katika mwili wa binadamu husambaa katika ubongo, ini, figo na mifupa. Inatunzwa katika meno na mifupa ambapo hujiongeza kwa muda.
Katika wakati wa mimba sumu hiyo ya kemikali ya lead huenda moja kwa moja kwnye damu na humuathiri mtoto na hakuna kiwango cha kemikali hiyo kinachotajwa kuwa ni salama.
Watafiti wanasema kemikali hiyo huathiri kwa baadhi kupata mzio yaani hu washwa midomo. Madhara mengine ni kuzuia vitundu vya hewa kwenye mwili. Na baadhi ya viungo huleta hatari ya kupata saratani.
BBC imezungumza na Daktari wa Saratani Heri Tungaraza kutoka Hospitali ya Taifa muhimbili anasema kama lipstiki hiyo ina kemikali ya lead basi hatari ya uwezekano wa kupata saratani upo japo kua hakuna tafiti inayoelekeza ni kiasi kipi cha kemikali hiyo ambacho ni salama.


Image caption
Baadhi ya hizi bidhaa kama ukitumia ambayo si salama zinakufanya unapendeza kwa muda, lakini baadae huleta madhara.
"Zipo bidhaa ambazo zina kemikali hiyo na ambazo hazina. Kemikali ya lead imekuwa ikihusishwa sana na saratani ya figo, tumbo na mgongo. Kwa hiyo uhusiano upo lakini hakuna tafiti iliyo fanyika ikaangalia kiasi cha kemikali hiyo iliyopo kwenye lipstiki na kusema moja kwa moja inaleta saratani ya aina gani. Hivyo kama kweli lipstiki imebeba kemikali hiyo basi ni vyema mtumiaji akahoji kabla ya kutumia. Pia watu waache kununua vitu mitaani wanunue bidhaa ambazo zimesajiliwa na zinatambulika vyema zilipo toka, Tungaraza anaiambia BBC
Nae Daktari Romana Malikusema kutoka SANITAS hospitali anasema kweli kuna madhara kuanzia kwenye madhara ya kawaida kama mzio mpaka yale madhara makali kama kuingiza kemikali sumu katika mwili endapo mtu atatulia lipstiki isiyo salama.
"Inategemea na bidhaa imetengenezwa kwa kemikali zipi, baadhi ya hizi bidhaa kama ukitumia ambayo si salama zinakufanya unapendeza kwa muda huo lakini baadae huleta madhara, ni kama vile watu wanavyo jipaka foundation mara nyingi huzeeka haraka inaondoa ule uhalisia inatoa kabisa uhalisia wa ngozi hivyo hata hali ya ngozi kusinyaa inakuja haraka," Dokta Romana anaiambia BBC
Hata hivyo Daktari huyo ameshauri kuwa watu wawe makini na bidhaa za urembo, wasome lebo na kujua ukomo wa kila bidhaa. Pia amesisitiza kuwa ni bora kununua ya gharama ambayo ni bora kuliko ya bei rahisi ambayo huenda ni si salama.

Post a Comment

Previous Post Next Post