Kusinzia kupita kiasi wakati wa mchana ni ugonjwa

Lucy sleeping
Wengi wetu huwa wanahangaika kuamka asubuhi wakati mwingine.
Wengi hudhani kuwa walikuwa na usingizi mzuri wakati kengele inapoita na kufikiri kwamba wanaweza kulala dakika tano zaidi.
Lakini kwa upande wake Lucy Taylor kutoka Wales ambaye ana umri wa miaka 42, kushindwa kuamka vizuri ni sehemu ya maisha yake kila siku.
Ili Lucy aweze kuamka vizuri lazima anywe dawa, na uweka kengele kwenye saa kwa sauti kubwa ili iweze kumuasha au ndugu zake kumuamsha.
Hali hii ya kuwa na tatizo la kupata usingizi kupita kiasi wakati wa mchana na kushindwa kuamka kwa shida asubuhi.

Tatizo la kushindwa kuamka asubuhi na kuwa na usingizi kila mara wakati wa mchana

Ugonjwa huu huwatokea watu mara chache sana na hutokana na usingizi wa kupindukia
"Ni hali ambayo inanifanya nilale kwa muda mrefu sana na hiyo ni sehemu ya ugonjwa huo," Lucy alieleza.
Chanzo cha hali hiyo hakijafahamika bado.
"Huwa nnachoka sana wakati wa mchana. Kulala huwa hakunifanyi kuwa na nguvu mpya na ninapata wakati mgumu sana kuamka ninapolala".
"Muda mrefu ambao niliwahi kulala ni kuanzia ijumaa baada ya chai ya jioni mpaka jumapili mchana."
Lucy Taylor
Image captionLucy andai kwamba hali ya kupata usingizi wa kupindukia ni mateso kwake
"Hakukuwa na mtu yeyote wa kuniamsha. Nilipomaliza kazi siku ya ijumaa nilirudi nyumbani na kulala mida ya jioni na kuamka jumapili mchana."
Lucy lazima anywe dawa 12 mpaka 15 kwa siku, kila siku ili ziweze kumsaidia aweze kuamka asubuhi na kumfanya ashinde vizuri siku nzima.

Dalili zake ni zipi?

Wataalam wanasema kwamba watu wawili kati ya 100,000 huwa wanaathirika na kusinzia kulikopitiliza lakini chanzo chake hakijulikani.
Dalili zake:
  • Usingizi wa kila wakati majira ya mchana na bado kuendelea kutojisikia vizuri
  • Kusinzia wakati wa kula na kuongea
  • Kulala kwa muda mrefu usiku hata kama mtu amelala muda mrefu wakati wa mchana
Lucy alielezea namna ambavyo hali yake inavyomuathiri.
"Ni kama vile nnaishi chini ya maji na nnajaribu kutoka. Ninataka kuachwa mwenyewa na nnataka kulala."
"Huwa inaniwia vigumu sana kupata usingizi wa kutosha na kuamka kuendelea na kazi vizuri."

Kutegemea wanafamilia

Ingawa hali yake huwa inawapa wakati mgumu familia yake.
Mama yake(Sue) huwa analala kwake siku za kazi ili aweze kumpa dawa na kumuamsha kuwahi kazini.
"Huwa nnaumia sana kumuona katika hali hii, kabla ya kupata ugonjwa huu alikuwa anaishi maisha mazuri tu", Sue alieleza.
Lucy's mother Sue
Image captionMama yake Lucy analazimika kukaa na Lucy siku tano katika wiki
Kwa sasa anapanga kufanya vitu na mwanae lakini haamki, na hiyo inamkatisha tamaa binti yake.
Nikiwa hapa nnaweza kumuasha na tunaweza kufanya vitu kwa pamoja. Inashangaza lakini bila kuamshwa hawezi kuamka.
'Sio Uvivu'
Hakuna mtu anayeelewa, wengi huwa wanadhani kuwa huwa ni mvivu au hataki tu kuamka. Hawaelewi ni changamoto gani anazipitia katika maisha yake.
Sue anakubali kuwa Lucy huwa anapata wakati mgumu sana kuamka. "Lucy akilala hakuna kitu kinachoweza kumuasha", Sue alisema.
Sue huweka kengele za sauti kubwa kwa ajili ya Lucy na kama hiyo haitoshi huwa anamuita kwa sauti mpaka aamke.
"Huwa inaniwia vigumu sana kumuona mwanangu anaishi hivi. Inauzunisha sana kiukweli. Hakuna utafiti ambao uliwahi kufanywa kuhusu hii hali.
Ingawa maisha ni mapambano ya kila siku", Sue aliongeza kwa kumsifia binti yake kuweza kuimudu hali hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post