Dawa za kuua bakteria zimekuwa zikipungua ufanisi siku hadi siku kutokana na bakteria kuwa na mabadiliko katika usikivu wa dawa izo.
kutokana na takwimu inasemekana miaka kumi baadae Afrika itakuwa ba vifo vingi zaidi vitokanavyo na bakteria wasiosikia dawa.
sababu za bakteria kutosikia dawa
sababu kubwa ya bakteria kutosikia dawa ni kutokana na wagonjwa kutomaliza dozi.sababu hii watu huwa hawaiwekei maanani lakini ina maana kubwa katika bakteria kutosikia dawa.
Hebu fikiria kama mtu akiwa anakuvamia kila siku bila kukua anakupiga na kukuacha mzima kwa mara kadhaa. Baadae utajua ni namna gani ya kupambana nae baada ya mda na kuanza kumshinda. Hivyo ndivyo bakteria hufanya endapo hawatauliwa kikamilifu kwa mgonjwa wataunda njia ya kupambana na dawa husika na baadae hawatasikia dawa kabisa. Bakteria huwa wanafanya mabadiliko ya haraka(evolution) katika genome zao(viini seli) kuliko binadamu kwani genome zao sio complicated kama za mwanadamu.
kwa maana hiyo ni rahisi sana kwa bakteria kubadilisha vipokeaji vya dawa husika kwenye mwili wao.
Sababu nyingine ni matumizi ya dawa bila kuumwa au bila majaribio na uchunguzi wa maabara.
Kutumia dawa za bakteria kwa wanyama waliwao bila kuwa na dozi sahihi pia huweza kusababisha.
Kumbuka
matumizi sahihi ya dawa ni lazima kwa maisha bora ya baadae