Kwa nini ubongo wa mlevi unashindwa kunakili kumbukumbu ya mambo yanapotendeka?

Mtu akishikilia glasi ya pombe
Kupoteza fahamu kutokana na unywaji wa pombe kupita kiasi ni hali ambayo watu wengi wameshawahi kushuhudia japo mara moja maishani.
Suala la kusahau au kupoteza kumbu kumbu baada ya kunywa pombe nyingi limezua gumzo nchini Marekani kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili jaji Brett Kavanaugh aliyeteuliwa na rais Trump.
Mmoja wa wale wanaomtuhumu Jaji Kavanaugh, anadai kuwa alimnyanyasa kingono akiwa mlevi miaka, 36 aliyopita.
Mwanamke mwingine anadai kuwa jaji huyu alijitupa kwake akiwa mlevi wakati wa michezo wakiwa chuoni.
Bwana Kavanaugh amekanusha madai hayo huku baadhi ya watu wakisema huenda alipoteza fahamu kutokana na ulevi kupindukia japo amepinga dhana hiyo pia.

Kupoteza fahamu kutokana na unyaji wa pombe ni nini?

Hii ni hali ya ubongo kushindwa kunakili kumbukumbu ya mambo yanayofanyika katika mazingira ya mtu anapokua mlevi.
Kwa mujibu wa taasisi ya kitaifa ya kukabiliana na matumizi mabaya ya vileo, hali hiyo hutokea kwa sababu mzunguko katika eneo la ubongo uliyo na jukumu muhimu la kuimarisha kumbukumbu za maisha yetu ya kila siku, imefungwa na pombe.
Dr Kate Carey, profesa wa sayansi ya tabia ya watu katika jamii kutoka Chuo Kikuu cha Brown huko Providence, Rhode Island,"Kati ya 30% na 50% ya vijanaambao wanakunywa pombe wameripoti hali ya kupoteza fahamu kutokana na ulevi.
Mwanamke akinywa mvinyoHaki miliki ya pichaPA
Ni watu gani wako katika hatari ya kupoteza fahamu kutokana na unywaji wa pombe?
Utafiti umebaini kuwa watu waliyo na miili midogo hukabiliwa na hali ya kupoteza fahamu hasa wanapokunywa pombe kupindukia.
Wanawake pia hukabiliwa na hali hiyo kwa sababu viwango vya pombe hupanda haraka kwa wanawake kadiri wanavyokunywa pombe bila kunywa maji.
Geni ya mtu pia inaelezea ni kwa nini watu wengine hupoteza fahamu wanapokunywa pombe kupindukia na wengine hawajipati katika hali hiyo.
Baadhi ya wataalamu pia wanasema wale watu wanao vuta sigara huku wakinywa pombe wako katika hatari ya kupoteza fahamu kutokana na ulevi.
Je kuna dalili zozote hujitokeza?
Dr Kate Carey, profesa wa sayansi ya tabia ya watu katika jamii , mtu anaweza kujieleza vizuri akiwa mlevi na hata kujua njia ya kuenda nyumbani akiwa mlevi.
Dr. Carey anasema ''Ukimuuliza mtu aliyekuwa mlevi jinsi alivyofika nyumbani hakumbuki nini kilichofanyika alipokuwa mlevi.
Mlevi wakati mwingine huchanganyikiwa kadri kiwango cha kileo kinavyoongezeka mwilini mwake kwa mfano na hawezi kuendelea na mazungumzo.
Madhara ya unywaji pombe ni yapi?
Kwa mujibu wa kituo cha marekani cha masuala ya ulevi na madhara yake, watu wanaweza kujiingiza katika tabia ambazo hawana wakiwa katika hali za kawaida
Ukiwa mlevi, inakuwa rahisi kwako kudhulumiwa kwa njia mbalimbali. Wakati huohuo, unaweza kuhatarisha maisha ya wengine, kwa kufanya mambo ambayo hungefikiria kufanya ukiwa na akili timamu.
Mara nyingi mlevi huwa hakumbuki yale yaliyojiri siku iliyotangulia alipokua amelewa chakari. Hii inatokana na hali ya yeye kupoteza fahamu.
Hata hivyo hali ya kupoteza fahamu mara kwa mara mtu akinywa pombe huenda ni ishara ya tatizo la kiafya ambalo huenda likasababisha maradhi ya ini.
Mwanamume analala baada ya kunywa pombe

Post a Comment

Previous Post Next Post