Canada imekuwa nchi ya pili baada ya Uruguay kuhalilisha matumizi ya bangi kwa starehe

Bendera ya Canada ikiwa na nembo ya bangiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Saa kadhaa baada ya Canada kuhalilisha uuzaji, umiliki na matumizi ya bangi kwa starehe kumekua na mjadala kuhusu madhara ya kiafya ya bangi kwa mtumiaji.
Mengi pia yameandikwa kuhusiana na madhara ya kiafya ya bangi kwa mtumiaji, japo kumekua na baadhi ya tafiti zinazoruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kwamba inasaidia wagonjwa walio na msongo wa mawazo.
Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.
Katika mataifa mengi duniani ni kosa la jinai kutumia bangi, kuuza, kusafirisha, kuhifadhi au kujihusisha nayo kwa namna yoyote .
Adhabu kwa makosa hayo hufikia hadi kifungo cha maisha.
Katika baadhi ya nchi ikiwemo Afrika mashariki - ni makosa kuilima lakini kila kukicha shehena kadha wa kadha zinakamatwa zikisafirshwa kimagendo.

Marufuku ya bangi Afrika mashariki

Tanzania ina mfano wa eneo huko Makeke Iringa ambapo jamii huitumia bangi kama mboga na kwa manufaa ya afya...hakuna sheria ya kuidhibiti.
Katika Pwani ya Kenya kumeshuhudiwa janga kubwa la vijana kutumia mihadarati mkiwemo hiyo bangi.
Swali ni je kuhalalisha bangi ni suluhisho kwa tatizo la vijana kujiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya?
Musa Ali aliwahi kuwa mraibu wa dawa za kulevya na sasa anawahamasisha vijana kuhusu madhara yakeHaki miliki ya picha@MUSA ALI
Image captionMusa Ali aliwahi kuwa mraibu wa dawa za kulevya na sasa anawahamasisha vijana kuhusu madhara yake
Musa Ali ambaye ni mwanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya mjini Mombasa pwani ya Kenya anasema, '' Kuhalaisha bangi itakua mwanzo wa vijana kujiingiza zaidi katika dawa za kulevya kwa sababu sasa watakua wanaona sasa ni kitu kimehalaishwa''.
Anaongeza kuwa vijana wamekua wakitumia bangi licha ya kuwa ni hatia na imeharamishwa kisheria.
Watafiti wamegundua kuwa zaidi ya vijana 3,100 walio katika umri wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji wakubwa wa bangi.
Utafiti pia umebaini kwamba asilimia 18 ya vijana hao ni wale waliojiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya kwa muda wa miaka miwili au mitatu.
Bwana Musa anasema yeye binafisi alianza kutumia bangi kabla ya kujiingiza katika utumizi wa dawa zingine za kulevya, ''Utumiaji wa bangi ulinisukuma mpaka nikaanza kuingilia mihadarati mingine mikwubwa, nikaanza kutumia Heroine, Cocaine kwa hiyo bangi inakushawishi kutumia dawa nyingine na nyingine''
Anasema baada ya kutumia dawa zote hizo za kulevya akajiona kuwa amepoteza malengo yake yote maishani na ndiposa akaanza kutafuta ushauri.
Wanasayansi wamebaini kuwa matatizo makubwa yanaanza kupatikana kutokana na bangi kuingia kwenye ubongo wa mtumiaji na huathiri mfumo mzima wa akili.
Kwa mujibu wa Dk. John McGrath, wa kituo cha uchunguzi wa afya ya wagonjwa wenye mtindio wa ubongo cha Queensland, nchini Marekani, anasema: Wengi wa wagonjwa ambao wamekumbwa na matatizo hayo tumegundua ni wale waliowahi kutumia bangi kwa muda mrefu na hatimaye kujikuta wakipata tatizo la akili
Daktari huyo anasema kuwa ni nadra sana kukutana na wagonjwa wa akili ambao hawajawahi kutumia bangi, iwe mwaka mmoja au zaidi.
Anasema kuwa iwapo matumizi ya bangi yatakomeshwa tatizo la vijana kupata matatizo ya utaahira yatapungua kwa kiasi kikubwa duniani.
bangiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKumekuwa na harakati za kutaka kuhalilishwa matumizi ya bangi katika baadhi ya mataifa Afrika mashariki

Madhara ya Bangi

  • Kuchanganyikiwa,ukatili,ukorofi,uhalifu,n.k.
  • Kuona,kusikia na kuhisi vitu visivyokuwepo.
  • Kupoteza kumbukumbu
  • Utegemezi na usugu
  • Moshi wa bangi unapoingia kwenye mapafu hutengeneza kitu kama lami ambayo huganda na kuathiri utendaji kazi wa mapafu.
  • Bangi ni kemikali (sumu) inayosababisha (saratani) zaidi ya tumbaku (sigara).
  • Kupunguza kinga ya mwili
  • Mtumiaji kuridhika na hali duni aliyonayo hivyo kukosa mwamko wa maendeleo huku akijihisi ni mwenye mafanikio makubwa.
  • Kuumwa koo,kupata kikohozi na saratani ya mapafu.
  • Kuathirika kwa mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na mabadiliko ya hedhi kwa wanawake.
  • Kuharibika mimba
  • Kuzaa mtoto njiti
Licha ya hofu ya wataalamu kuhusiana na madhara ya bangi juhudi za kuhalalisha utumizi wakezinaendelea kushika kasi katika baadhi ya mataifa ya Afrika.
bangiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBangi
Zimbabwe imehalalisha uzalishaji wa bangi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi ikiwa ndiyo nchi ya pili kufanya hivyo barani Afrika baada ya Lesotho iliyotoa leseni yake ya kwanza kwa kilimo cha mmea huo mwaka uliopita.
Hata hivyo, ni haramu kupanda, kumiliki au kutumia bangi nchini Zimbabwe ambapo yeyote ambaye atakutwa na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 12 jela.
Mwezi uliyopita mahakama ya Kikatiba nchini Afrika kusini ilihalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha.
Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.
Mtafiti mmoja nchini Kenya - Simon Mwaura - amewasilisha ombi kwa kamati ya afya katika bunge nchini kenya kutaka bangi ihalalishwe akieleza kuwa serikali inapoteza Shilingi trilioni 1.5 kila mwaka. Anataka sasa bangi ihalalishwe kwa manufaa yake ya kiuchumi

Post a Comment

Previous Post Next Post