Jinsi ya kuondoa michirizi mwilini bila gharama



michirizi.jpg
Uwapo wa michirizi mwilini ni tatizo linalowasumbua wengi. Michirizi hii huweza kutokea shingoni,tumboni,mikononi,mapajani na hata kiunoni.
Watu wengi huhaha kutafuta dawa ya kuondoa tatizo hilo bila mafanikio. Ni tatizo linaloleta muenekano mbaya hasa mhusika akivaa nguo za wazi. Mtaalamu wa masuala ya vipodozi Mandeep Singh anabaanisha dondoo za kukabiliana na tatizo hilo.
Miongoni mwa dondoo hizo ni unywaji wa maji mengi angalau glasi kumi kwa siku,ulaji wa mboga za majani na vyakula vyenye wingi wa vitamin C na E sambamba na madini ya Zinc na Silica ikiwamo karoti,spinachi na maharage mabichi.
Vilevile matumizi ya juisi ya limao ambayo unaweza kuipaka kwenye maeneo yenye michirizi. Unapotumia njia hii hakikisha limeingia vizuri kwenye ngozi yenye michirizi kwa angalau dakika 15 halafu nawa na maji ya uvuguvugu.
Njia nyingine ni matumizi ya viazi mduara. Katakata vipande vyembamba na kisha jipake kwenye maeneo yaliyoathirika

Post a Comment

Previous Post Next Post