Mpiga picha wa Reuters Clodagh Kilcoyne ametengeneza mfululizo wa picha za waislamu wa Rohingya wasichana na wanawake katika kambi mbalimbali za kusini mwa Bangladesh, akipata picha za urembo wao wa asili
Zaidi ya watu wa jamii ya Rohingya 700,000 wamekimbia makwao na kukimbia kushtakiwa katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar na kukimbilia nchini Bangladesh tangu mwezi Agosti mwaka 2017.
Idadi ya warohingya wanaokaribia milioni moja nchini Myanmar ni moja kati ya jamii ya watu wachache waishio nchini humo.
Jeshi la Myanmar limesema linapambana na wanamgambo wa Rohingya wakikana kuwalenga raia.
Picha za wasichana waislamu wa Rohingya na wanawake kwenye kambi za Cox Bazaar, mji ukio kusini mwa pwani ya mashariki mwa Bangladesh zilipigwa na Kilcoyne.
Poda hii iliyo mithili ya tope pia husaidia kuzuia miale mikali ya jua, kuifanya ngozi kupoa.
Poda hii ya manjano hukauka na kuwa kavu usoni, huzuia pia kuumwa na wadudu.
Poda hii, imekuwa ni kawaida miongoni mwa jamii ya wasichana na wanawake wa kiislamu jamii ya Rohingya.
Juhara Begum mwenye miaka 13 hapo chini anamwambia Kilcoyne kuwa'' ninapenda sana kujiremba, ni utamaduni wetu''.
''Jeshi lilifyatua risasi na kutuchinja.Niliishi milimani, ambako kuna joto kutokana na jua kali''.
Begun aliwasili Cox's Bazar mwezi Septemba mwaka jana baada ya kukmbia mashambulizi ya kijeshi katika kijiji chake kilicho katika jimbo la Rakhine.
Alilazimika kutembea kwa siku tano kufikia eneo la mpaka lililo salama na kambi iliyokuwa na watu wengi ya Jamtoli.
''Ninaweza kuishi bila kula wali lakini si bila poda'', alisema Begum.
Zannat Ara, mwenye miaka tisa kutoka kambi ya wakimbizi ya Kutupalong alisema: ''Ninapaka poda kuuweka uso wangu kuwa safi na kuna wadudu wanauma usoni lakini poda hii huwafukuza''.
Picha na Clodagh Kilcoyne.