Fahamu kwa nini mafuta ya mgando si mazuri kutibu vidonda

Watu wana maoni kuwa mafuta ya mgando huponya vidonda
Utafiti mpya unaeleza kuwa kuweka mafuta ya mgando haraka kwenye jeraha lililotokana na kukatwa,michubuko au kuungua ni maamuzi mabaya
Wanasayansi wamegundua kuwa ngozi hujitengenezea ''plasta ya asili'' ili kusaidia kuponya majeraha.
Vitu vilivyo na mafuta, kama vile mafuta ya mgando, huvuruga mchakato huu muhimu, na inaweza kuleta athari za kwenye jeraha, wameeleza wanasayansi hao kwenye jarida lao la kitabibu.
Taasisi inayohusika na tiba za ngozi inasema kuwa mafuta ya mgando husaidia kukiweka kidonda kisiwe kikavu kwa kuwa huchukua muda mrefu kupona.Pia husaidia kuzuia kovu lisiwe kubwa sana, kuchimbika na kuzuia muwasho.
Kwakuwa kidonda husafishwa kila siku, si lazima kutumia mafuta.
Baadhi ya hospitali huwaambia wagonjwa wenye vidonda vinavyotokana na upasuaji ambavyo viamenza kupona kutumia mafuta.
Hata hivyo, Profesa Robert Ariens na wenziwe kutoka chuo kikuu cha Leeds wanasema hii huenda si njia nzuri ya kufanya kuelekea uponyaji wa kidonda.
Wamegundua kuwa kidonda hujiponya chenyewe bila kuwekwa mafuta.

Kidonda hujitengenezea plasta yake yenyewe ambayo huzuia maambukiziHaki miliki ya pichaUNIVERSITY OF LEEDS
Image captionKidonda hujitengenezea plasta yake yenyewe ambayo huzuia maambukizi

Wataalamu wanasema ngozi ambayo huota kwenye kidonda kina matundu madogo madogo ambayo hufanya hewa iweze kupenya lakini ni vidogo sana kuruhusu vijidudu na virusi kupenya.
Ariens amesema ngozi hiyo ''inaweza kuzuia madhara ya bakteria kwa angalau saa 12, na pia husaidia kuupa mfumo wa kinga kupeleka chembechembe nyeupe za damu kwenda kwenye kidonda kupambana na maambukizi''.
Profesa Ariens anasema ''kama umepata mchubuko au umejikata ni bora kuacha kikaganda kwa nusu saa ili kujitengenezea plasta yake yenyewe.baada ya hapo haitakuwa vibaya kama utapaka mafuta juu yake,lakini ukiweka mafuta kabla unaharibu mchakato wa plasta kujitengeneza''.
Mtaalamu wa maswala ya afya ya vidonda, Jacqui Fletcher, ambaye ni mhariri wa jarida la Wound UK anasema: kuna hatari ya matumizi ya mafuta ya mgando ambayo yamekaa kabatini kwa muda mrefu.
''Watu huacha makopo ya mafuta wazi kwa muda mrefu na kutumbukiza kidole, hivyo hayawezi kuwa masafi.

Post a Comment

Previous Post Next Post