Kutokana na maswali mengi kwenye ukurasa wetu wa facebook kuhusu mwanamke kutoshika mimba na matatizo mengine ya uzazi hii post inaweza kuwa jibu la maswali yako
Uchunguzi uliofanyika nchini Marekani mwaka 1990 ulionyesha kuwa tatizo la kutokupata mimba au kutokuzaa hugharimu mamilioni ya dola. Mtiririko wa upataji ujauzito ni kama ifuatavyo:
Baada ya mwezi mmoja wa ndoa uwezo wa kushika ujauzito ni asilimia 20, baada ya miezi mitatu ya ndoa ni asilimia 50, baada ya miezi sita ya ndoa ni asilimia 75 na baada ya miezi 12 ni asilimia 90 mwanamke huweza kupata ujauzito.
Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito ni kama zifuatazo:
Matatizo katika homoni, hii ni kutokana na kwamba, mzunguko (Menstrual cycle) katika mwili wa mwanamke hutawaliwa na hizi kemikali asilia ndani ya mwili ambapo mabadiliko madogo yakitokea katika uzalishaji wa hizi homoni au homoni kuzalishwa katika wakati ambao siyo muafaka huweza kupelekea mwanamke akashindwa kupata ujauzito, pia tatizo la kuwa na uzito wa mwili mdogo sana au mkubwa sana pia huathiri hali nzima ya homoni na kupelekea kushindwa kupata ujauzito.
Umri, kwa wanawake uwezo wa kupata ujauzito unapungua kwa kadri umri unavyoongezeka, hii inatokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni husika wakati umri unavyoongezeka. Kuanzia miaka 35 na kuendelea huwa kunakuwa na tatizo la kushindwa kupata ujauzito kwa wanawake wengi.
Kuziba kwa mirija (fallopian tubes), hii husababisha mbegu za kiume (sperms) zishindwe kulifikia yai na kulirutubisha ili ujauzito utokee. Kuziba kwa mirija huweza kusababishwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, matatizo katika kizazi au upasuaji. Mara nyingi wanawake ambao mirija yao imeziba, hawahisi dalili zozote.
Ute ute katika kizazi (mucus problems), ute unaopatikana katika kizazi cha mwanamke huwa na sifa ya kuruhusu mbegu za kiume ziweze kusafiri kwa urahisi na kulifikia yai ili kulirutubisha. Kwa baadhi ya wanawake ute huu unakuwa na uzito na kemikali ambazo ni vigumu kwa mbegu za kiume kuweza kupita, na wakati mwingine mwili wa mwanamke huzalisha sumu ambazo huziua mbegu za kiume, haya yote husababisha kukutana kwa yai na mbegu za kiume kusitokee na hivyo ujauzito kutopatikana.
Uvimbe katika kizazi (fibroids), hii huchangia asilimia tatu (3%) katika mwanamke kutopata ujauzito. Uvimbe huu ambao hutokea katika kuta za mji wa mimba, kwa namna moja au nyingine huweza kuzuia yai lililorutubishwa lisikae sehemu yake na hivyo kuathiri kizazi.
- soma zaidi kuhusu dalili na mambo mengine kuhusu uvimbe wa kizazi bofya hapa
Matibabu ya kansa, kwa kutegemeana na aina ya matibabu, aina ya dawa au njia ya mionzi, hizi huweza kumuathiri mwanamke na kumsababishia kushindwa kupata ujauzito.
Ukomavu katika kizazi, kwa baadhi ya wanawake wanayo matatizo ambayo kizazi chao huwa hakijakomaa vizuri au katika kuzaliwa kwao walizaliwa na tatizo hili ambalo, kizazi hakiko sawa (abnormally developed uterus).
Asilimia kubwa ya matatizo ya mwanamke kushindwa kupata ujauzito yanayo tiba, kama unalo tatizo katika kupata ujauzito usikate tamaa, onana na wataalamu wa afya ili uweze kujua chanzo cha tatizo lako na kupatiwa msaada unaostahili.
- soma kuhusu hedhi kwa mwanamke kwani inaweza kuwa sababu ya mwanamke kuopata mimba.bofya hapa
Kwa mwanaume; kutoweza kumpa mimba mwanamke
Wanaume wengi wanashindwa kumpa mimba mwanamke kutokana na kutumia dawa hovyohovyo au kuwa na matatizo ya tezi za thyroid, kuwa na ugonjwa wa kansa na matumizi ya kahawa na matatizo mengine ya kimwili.
Pia matatizo ya utokaji mbegu (manii), maumbile yasiyo rasmi na muonekano wa mbegu za kiume, upungufu wa mbegu za kiume, mbegu kutokuwa imara, tezi la kende kupanda juu tumboni, tatizo la vichocheo vya testosterone kupungua mwilini na kuwa na maambukizi ya vijidudu ndani ya viungo vya uzazi wa mwanaume.
Mwanaume pia anaweza kuwa na matatizo ya kurithi kama tatizo la kupeleka mbegu vizuri ukeni kama upungufu wa nguvu za kiume (sexual essues), kumwaga nje mbegu za kiume, kuziba kwa mishipa ya uzazi ya mwanaume kutotengenezwa mbegu (no semen) na kadhalika.
Matatizo ya kimaisha kwa mwanaume kama vile mfadhaiko (stress) au msongo wa mawazo, utapiamlo, ulevi wa kupindukia na matumizi ya madawa ya kulevya, umri kuwa mkubwa zaidi ya miaka 70.
Matatizo ya mazingira mabaya kwa mwanaume kama matumizi ya dawa za kuua wadudu watambao viungo vya uzazi wa mwanaume, kupata joto kupita kiasi kama kuendesha magari ya mizigo ambapo dereva hukaa kitini kwa zaidi ya saa 10 na kufanya sehemu aliyokalia kupata joto sana pia matumizi ya tumbaku na sigara kwa wingi.
Kuchanganua mtu mwenye tatizo la kutopata ujauzito huhitaji kwanza, mama na baba wote kwenda hospitali kuonana na daktari ili apate maelezo sahihi na waweze kupata mafunzo sahihi.
Vipimo kwa upande wa wanawake
Vipimo kwa upande wa wanawake
Kipimo cha upevushaji wa mayai kupima mirija ya uzazi, upasuaji mdogo kwenye tumbo na kumulika ndani ya mwili wake ultrasound ya kizazi na vinginevyo.
Vipimo kwa upande wa wanaume
Baada ya kuchukua historia ya mgonjwa kwa urefu kinachofuata ni vipimo vya kuangalia kama yupo kawaida au kama kuna hitilafu. Vipimo hivyo ni kumchunguza mwanaume kwa ujumla hali ya afya yake kwa kumpima kuanzia kichwani hadi miguuni.
Baada ya kuchukua historia ya mgonjwa kwa urefu kinachofuata ni vipimo vya kuangalia kama yupo kawaida au kama kuna hitilafu. Vipimo hivyo ni kumchunguza mwanaume kwa ujumla hali ya afya yake kwa kumpima kuanzia kichwani hadi miguuni.
Kupima mbegu zake, kupima vichocheo vyake vya uzazi, kupima na ultrasound kwenye korodani zake.
Ushauri Muda wa kufanya tendo la ndoa kabla ya upevukaji wa mayai huzingatiwa kuhesabu vizuri kwa kutumia kalenda kuanzia siku ya kwanza ya kutoka hedhi ambapo mtu mwenye mzunguuko mfupi ni siku 28 hivyo hutoa siku 14 na kubaki zingine 14 ambazo ndiyo siku ya kuweza kuwa yai limepevuka.
Ushauri Muda wa kufanya tendo la ndoa kabla ya upevukaji wa mayai huzingatiwa kuhesabu vizuri kwa kutumia kalenda kuanzia siku ya kwanza ya kutoka hedhi ambapo mtu mwenye mzunguuko mfupi ni siku 28 hivyo hutoa siku 14 na kubaki zingine 14 ambazo ndiyo siku ya kuweza kuwa yai limepevuka.
Kwa hiyo, tunashauri kufanya tendo la ndoa kuanzia siku ya nne hadi ya tano kabla siku ya kupevuka kwa yai.Mwanamke anashauriwa kulalia mgongo huku umeinua magoti baada ya kufanya tendo la ndoa kwa muda wa dakika 20.
Kutotumia mafuta yoyote ya kulainisha uke kwani baadhi ya mafuta huuwa mbegu za kiume.
Kuacha kuvuta sigara kwa mwanaume na mwanamke kwani uchunguzi huonyesha kuwa uvutaji wa sigara unasababisha ugumba na utasa.
Kuacha kuvuta sigara kwa mwanaume na mwanamke kwani uchunguzi huonyesha kuwa uvutaji wa sigara unasababisha ugumba na utasa.
Kupunguza uzito kwa mwanamke na mwanaume na kutumia vidonge vya madini ya foric acid kwa ushauri wa daktari kumeonyesha msaada mkubwa kwa akina mama wanaopata shida ya kupata mimba.
Upimaji wa mbegu za kiume
Upimaji wa mbegu za kiume
Mbegu za kiume baada ya kutolewa zinatakiwa kufikishwa maabara kabla ya dakika 30 kwa upimaji.
Mwanaume anashauriwa kukaa siku 3 bila kuwa amefanya tendo la ndoa na ndipo atoe mbegu zake. Ujazo au wingi wa mbegu kawaida ziwe zaidi ya milioni mbili. Kwa kawaida wingi wa mbegu ni zaidi ya milioni 25.
Mwanaume anashauriwa kukaa siku 3 bila kuwa amefanya tendo la ndoa na ndipo atoe mbegu zake. Ujazo au wingi wa mbegu kawaida ziwe zaidi ya milioni mbili. Kwa kawaida wingi wa mbegu ni zaidi ya milioni 25.
Mbegu zenye afya zinazoweza kuogelea vizuri na kukimbia zinafanya zaidi ya asilimia 40 kuwa na uwezo wa kutembea vizuri.
Wakati wa kupimwa, wataalamu huangalia jinsi mbegu zinavyofanana umbo. Vitu vingine tunavyoangalia kwenye mbegu ni kama PH ya mbegu ambapo kawaida ni 7.2 hadi 8.0. Ikiwa kwenye mbegu kuna chembechembe nyingi nyeupe za damu na kipimo kinaonesha hivyo basi hali hiyo huashiria kuwa kuna maambukizi ya vijidudu kwenye hizo mbegu za kiume.
KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI (MENOPAUSE)
Wataalamu wa afya wanasema kwamba mwanamke amekoma hedhi anapokosa kupata hedhi kwa miezi 12 mfululizo. Ni wanawake wachache hukoma kupata hedhi ghafula, yaani, wanakosa hedhi mwezi mmoja unakuwa mwisho wa kuipata.
Wanawake wengi huanza kipindi hiki wakiwa na umri wa miaka 40 na kitu, lakini kwa wengine huanza wakiwa wamechelewa wakiwa na miaka 60 na kitu.
Kutokana na mabadiliko ya kiwango cha homoni kinachotokezwa, huenda mwanamke akakosa kupata hedhi pindi kwa pindi, akapata hedhi wakati ambao hakutarajia au akavuja damu nyingi isivyo kawaida wakati wa hedhi. Pia huenda mwanamke akashuka moyo, hisia zake zikabadilikabadilika na hilo linaweza kumfanya alielie bila sababu, na pia asiwe makini sana na asahau mambo.
Kipindi cha kukoma hedhi huwa tofauti kwa kila mwanamke. Dalili zinaweza kuonekana kipindi hicho ni pamoja na joto la ghafula mwilini, ambalo huenda likafuatiwa na kuhisi baridi. Dalili hizo zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na kuishiwa na nguvu.
Baadhi ya wanawake hupatwa na joto la ghafla mwilini kwa mwaka mmoja au miaka miwili wakati wa kipindi hicho cha kukoma hedhi.
Wengine hupatwa na hali hiyo kwa miaka mingi na wachache sana husema kwamba wao hupatwa na joto la ghafla mara kwa mara maisha yao yote.
Ni busara mtu afanyiwe uchunguzi wa kiafya kabla ya kuamua kwamba joto la ghafula linasababishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa kuwa kuna matatizo mengine ya kiafya yanaweza kuleta joto la ghafula mfano ugonjwa wa dudumio, malaria, homa ya matumbo n.k
JINSI YA KUISHI VIZURI KIPINDI HICHO
Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kupunguza baadhi ya matatizo hayo mfano kuacha kuvuta sigara, kupunguza au hata kuacha kunywa vileo, vinywaji vyenye kafeini na vyakula vyenye sukari au vikolezo ambavyo vinaweza kusababisha joto la ghafula mwilini.
Kufanya mazoezi husaidia sana kupunguza matatizo yanayohusianishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kupunguza kukosa usongizi na kusaidia kuboresha hali ya kihisia na pia huimarisha mifipa na afya ya mtu kwa ujumla.
Ili kumsaidia mwanamke kukabiliana vizuri na kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi, huenda madaktari wakampa homoni, vitamini na madini, na dawa za kutibu kushuka moyo.
Pia ni jambo la busara kuwaambia uwapendao hali unayokabili ili wakuonyeshe upendo na wakupe msaada unaouhitaji wakati wa hali yako.
Kipindi hicho kinapokwisha, wanawake ambao hutunza afya yao, wanapata tena nguvu na kuendelea kufurahia maisha.
Sababu tajwa hapo juu zaweza kuwa moja ya sababu za mwanamke na mwanaume kutopata mtoto
Ushauri waone wataalam wa matatizo ya wanawake kwa
Uchunguzi na Tiba ya Tatizo
Uchunguzi na Tiba ya Tatizo