Je tunapaswa kulala na kuamka mapema kuimarisha afya yetu?

Je tunastahili kurauka ili tuimarishe afya yetu?
Wakati utafiti wa hivi karibuni ulipokagua tofuati za kiafya kati ya watu wanaoamka kuchelewa na wanaorauka, ulikonekana kuonyesha hali sio nzuri sana kwa wanaoamka kuchelewa.
Hatari ya kifo cha mapema, matatizo ya akili na magonjwa yanayotokana na kupumua ndio mambo yaliogunduliwa katika utaifiti huo, uliounga mkono tafiti nyingine zinazoashiria watu wanaolala kuchelewa wamo katika hatari ya kuugua magonjwa hayo.
Lakini je kulala na kuamka kuchelewa kuna hatari gani kwako na je ina maana kuwa baadhi yetu tunapaswa kulala mapema na kuamka mapema ili tuziimarishe afya zetu.
Uchofu wa wiki nzima'
Ni taswira inayofahamika vizuri na wafanyakazi wengi katika wiki.
Baada ya kuutafuta usingizi kwa saa nyingi na kuishia kulala kuchelewa, ghafla unaamshwa na kengele ya saa ya kukuamsha.
Ikifika mwishoni mwa juma unakuwa taabani na unaishia kulala saa zaidi ya kawaida yako unavyolala Jumatatu hadi Ijumaa ili kupatiliza usingizi ulio ukosa.
Huenda unaona hili ni jambo la kawaida, lakini ni ishara sio tu ya kwamba hupati usingizi wa kutosha lakini pia una uchofu wa wiki nzima.
Tofuati ya saa unayo lala katika wiki nzima ikilinganishwa na unavyo lala wakati wa wikendi ndio kigezo kikuu wakati tuna uhuru wa kulala na kuamka kwa wakati tunaotaka.


Utafiti unaonyesha watu walio na uchofu mkubwa wa wiki huishia kuwa katika hatari zaidi ya kuvuta sigara na kulewa.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUtafiti unaonyesha watu walio na uchofu mkubwa wa wiki huishia kuwa katika hatari zaidi ya kuvuta sigara na kulewa.

Kila unapokuwa na uchofu zaidi ndio unajiweka katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa kama ya moyo na mengine yanayohusu mfumo wako wa kusaga chakula.
Hayo ndiyo yanayotoa msukumo wa utafiti huo hususan kwa watu wanaoamka kuchelewa - wanaoonekana kuwa katika hatari zaidi ya kuwa na afya mbaya ikilinganishwa na watu wanaorauka asubuhi, kwa mujibu wa Till Roenneberg, mhadhiri katika kitengo cha utafiti wa afya wa magonjwa ya akili katika chuo kikuu cha Ludwig-Maximilian mjini Munich.
Na iwapo utawalazimisha watu wanaorauka kufanya kazi na kuishia kulala kuchelewa pia watakabiliwa na matatizo ya afya anasema Russell Foster, mkuu wa maabara ya Nuffield katika taasisi ya Circadian Neuroscience.
'Ni biolojia ya binaadamu'
Basi wafanye nini watu wanaoamka kuchelewa?
Je wanastahili kuamka mapema wikendi badala ya kulala kupita saa yao ya kawaida?
Hilo sio jambo jema," anasema Mhadhiri Roenneberg, anayeamini kwamba hakuna kitu kilicho na hatari kwa afya kuhusu kuamka kuchelewa.
"Kama hujalala kutosha kwa siku tano , ni afadhali upatilize uzingizi wako kwa wakati muafaka kwako."


Je watu wanaomka kuchelewa wanastahili kuamka mapema wikendi?Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJe watu wanaomka kuchelewa wanastahili kuamka mapema wikendi?

Hii ni kwasababu muda tunaotaka kuala au kuamka sio tabia tu wala maadili. badala yake inatokana na shinikizo la jinsi miili yetu ilivyoundwa, ambapo 50% inatokana na jini zilizomo ndani ya miili.
Mengine yanatokana na mazingira, umri 
Huenda uziweze kugeuza mienendo inayotokan an jini zako mwilini ka kuamua tu kuamka mapema ,badala yake unaweza kujinyima usingizi ambao tayari huupati wa kutosha katia wiki, wataalamu wanasema.

Post a Comment

Previous Post Next Post