Kwa miaka mingi sana wanadamu hasa katika nchi masikini wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la funza amabao huchimba ndani ya miili yao na kusababisha usaha na maumivu makali.Kwa kitaalamu tatizo hili huitwa myiasis yaani myia stand for tissue(tishu) na sis stand for inflamation(kuharibiwa).
FUNZA NI NINI?
Funza hawa ni moja tu kati ya hatua za ukuaji za wadudu walukao, watu wengi hufikili hao funza hubaki kuwa funza mpaka mwisho jambo ambalo si la kweli hawa funza ni larval stage ya ukuaji wa wadudu ambapo wadudu hao wapepelukao hutua na kutaga mayai yao katika ngozi au kidonda chako.
Je funza hawa huathiri vidonda tu?
si kweli, kwani baadhi ya funza wanaoitwa screw worms wanaweza kupenyeza hata kwenye ngozi isiyo na jeraha.
Watu walio katika hatari ya kuathirika ni wapi?
- watu wenye kisukari
- wasio na usafi wa miili yao
- wanaoishi karibu na sehemu za taka
- wenye vidonda
- watoto(soma kisukari kwa watoto)
Jinsi ya kuepuka funza hao
- oga mara kwa mara
- usikae sehemu iliyo karibu na uchafu
- epuka mambo yatakayo pelekea upate kisukari
- usiwaache watoto kucheza sehemu chafu
Tags:
WADUDU NA MAGONJWA