Tohara ya Wanaume inaweza kuzuia 200,000 kupata Ukimwi

Tohara ya Wanaume inaweza kuzuia 200,000 kupata Ukimwi TanzaniaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionSherehe ya Tohara
Viongozi wa dini Tanzania wameombwa kusaidia katika kampeini ya kuhamasisha wanaume kuitikia tohara . Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya jarida la Kitabibu la Lancet. Watalaamu wa matibabu wanasema tohara ya wanaume husaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kwa kuitikia wito huu huenda maambukizi laki mbili yakaweza kuzuia.
Asili mia 90 ya Watanzania wanafuata dini moja au nyingine hivyo viongozi wa kidini wametajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika kubadilisha imani potofu juu ya tohara ya wanaume.Baadhi wanaamini tohara ya wanaume ni sawa na kubadilisha imani ya mtu.
Taarifa ya Lancet imesema viongozi wa dini wanaweza kuchangia katika kuhamamisha jamii umuhimu wa tohara ya wanaume katika kukabiliana na maambukizi ya ukimwi.Lancet ilifanya utafiti waake katika vijiji 16 ulioambatana na kampeini ya kuhamamsiha wanaume kukubali kutahiriwa.
Kampeini inayohusisha viongozi wa dini imewezesha asili mia 23 ya wanaume kujitokeza kwa hiari na kupashwa tohara.Ni kutokana na mafanikio haya ambapo viongozi wa dini Tanzania wameombwa kusaidia katika kampeini hii. Aidha wadadisi wa ripoti hii wanasema kampeini hii ya kuwajumuisha viongozi wa dini ifanyike Barani Afrika hususan maeneo yote ya kusini mwa Jangwa la sahara.

Post a Comment

Previous Post Next Post