Taasisi za kujitegemea zilizofanya utafiti maeneo kadha wa kadha hasa mikoa ya morogoro na mikoa jirani na huo zimethibitisha uwepo wa virusi hao wa zika waliojipatia umaarufu mkubwa miaka ya karibuni.
LAKINI
Wizara ambayo ina dhamana na hayo imeendelea kutupilia mbali utafiti huo kwani hakuna mgonjwa aliyeonekana amepata madhara ya uzao wake
HEBU TUMJUE HUYU ZIKA NI NANI
Virusi vya zika kwa mara ya kwanza viligundulika nchini uganda mwaka1947 katika nyani na baadae mwaka 1952 viligundulika kwa binadamu huko huko nchini UGANDA.Virusi hivyo vilisababisha madhara makubwa mwaka2007 huko ISLAND na baadae kurejesha umaarufu wake mwaka 2015 huko BRAZILI
NJIA ZA KUENEZWAvirusi hawa huenezwa na mbu jamii ya aedes genus ambao mara nyingi huwa ni ae.aegypti au ae.albopictus ambao pia ndio wanaoeneza vimelea vya magonjwa kama dengue,homa ya manjano na chikungunya
DALILI
- Maumivu ya kichwa
- maumivu ya mifupa na viungo
- uchovu
- vijipele vidogodogo
NINI MADHARA YAKE
Madhara makubwa ya zika ni kusababisha mtoto kuzaliwa na kichwa kidogo
KUJIKINGA
tutajikinga na ugonjwa huu kwa kuwazuia mbu hao waenezao vimelea
TIBA
kiuharisia hamna tiba yake zaidi mgonjwa atapewa dawa za kawaida za kupunguza maumivu na apumzike