Wenza wa asili ya Asia wapata watoto waliopandikizwa kimakosa

Picha ya mbegu ya kiume kabla ya mchakato wa kupandikizaHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY
Wenza wenye asili ya Asia ambao walijaribu kupata watoto kwa njia ya kupandikiza (IVF) wamedai kuwa kumetokea mkanganyiko katika hospitali ya mjini California mkanganyiko uliofanywa wapate watoto wasio wao.
Mashtaka yaliyofunguliwa na wenza hao katika mji wa New York yanasema wawili hao walipata mshtuko baada ya kuzaa watoto wawili wa kiume ambao hawakuwa na chembe yeyote ya Asili ya Asia kama ilivyo kwa wazazi hao.Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti.
Vipimo vya nasaba, DNA vinathibitisha kuwa watoto hao hawakuwa na uhusiano wowote na wapenzi hao.
Kliniki hiyo haijasema chochote kuhusu shutuma hizo.
Wanasayansi wakaribia kupata dawa ya Ukimwi?
Wapenzi hao ambao wamepewa majina ya AP na YZ wamesema kwa muda mrefu walikuwa wakitafuta watoto kisha wakatumia kiasi cha pauni 80,000 kama gharama za hospitali na kupandikiza.
Inaripotiwa kuwa baada ya kujifungua tarehe 30 mwezi Machi, wapenzi hao walishtuka kuona watoto ambao waliambiwa walipandikizwa kwa kutumia jeni (genes) zao hawakuwa waliowatazamia.
Tumbo la ujauzito
Kulikua na dalili awali kuwa vitu havikuwa sawa baada ya kufanyiwa uchunguzi wakati wa ujauzito na kuambiwa kuwa walitegemea watoto wa kiume, ingawa madaktari waliwaambia hawakupandikiza viinitete vya kiume wakati wa matibabu yao.
Madaktari wameripotiwa wakiwaambia wapenzi hao kuwa uchunguzi huo umetoa majibu yasiyo sahihi,kabla ya kwenda kujifungua watoto wawili wa kiume mwezi Aprili.Mbali na kuwa watoto hawakufanana na wazazi hao, watoto wenyewe pia hawakufanana.
Kwenye tovuti ya kliniki hiyo ya uzazi, iitwayo CHA imesema inatoa huduma hizo kwa umakini wa hali ya juu na huduma zilizo bora kabisa.
BBC imeitafuta Kampuni hiyo kujibu shutuma hizo.

1 Comments

  1. karibu na soma tena machapisho yangu. i will visit your blog.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post