KUHARIBIKA KWA MIMBA(MISCARAGE)

Image result for miscarriage
Kuharibika kwa mimba ni  hali ya mwanamke kupata ujauzito na ukatoka kabla ya muda wake ambapo tatizo hili huangaliwa kabla ya kutimiza wiki 20 tangu kutungwa kwake.Hali hiyo inapotokea huitwa kuwa mimba imetoka au imeharibika (Miscarriage).
Hali hii ya mimba kuharibika inakuwa tofauti kabisa na utoaji mimba ambapo kitendo cha kutoa mimba kinafanywa na binadamu kwa makusudi na huwa amedhamiria kufanya hivyo.
Mimba kuharibika au kutoka ni hali ya mimba yenye wiki 28 au chini ya hapo kuharibika au kutoka. Hali hujulikana kama miscarriage au spontaneous abortion kwa kiingereza. Mtoto aliye tumboni katika umri huu hataweza kuishi nje ya tumbo la mama. Katika nchi zilizoendelea huchukuliwa mimba iliyo chini ya kipindi cha wiki 24.
Image result for miscarriage
SABABU ZA MIMBA KUTOKA
umri mkubwa ambapo kwa kawaida mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi misuli(sphencters) ya mji wa uzazi hulegea na kupunguza nguvu za kuweza kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji wa uzazi, hivyo kusababisha mimba kutoka.
Hitilafu katika kizazi ambayo huwa katika mfuko wa mimba(uterus) ambao muundo wake siyo wa kawaida.Wanawake wenye tatizo kama hili huwa na hatari kubwa ya mimba kuharibika kabla ya miezi tisa.
Aidha maambukizi ya fangasi au bakteria husababisha misuli ya kizazi kushambuliwa hivyo kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi ujauzito hivyo mimba kuharibika. Miongoni mwa sababu zinazosababisha mimba kuharibika ni matatizo ya vinasaba(genetic factors)
Hali hiyo hutokana na hitilafu katika kromosomu(cromosomal abnormalities) ambayo husababisha vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida ambayo hali hiyo ni miongoni mwa sababu kubwa zinazosababisha mimba kutoka kabla ya kutimiza wiki 13.
Hii husababisha damu ya mama kushindwa kuendana na damu ya mtoto hivyo kutokea kwa madhara ambayo humdhuru mtoto na kumfanya ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama hivyo kutoka nje.
Pia ukosefu wa homoni ya progesterone ambayo hufanya kazi kubwa tangu kutungwa kwa mimba hadi mtoto kuzaliwa  ambayo huchochea uimara wa ukuta wa placenta ambao mtoto hujishikiza.
Upungufu wa homoni hii husababisha ukuta wa mji wa mimba kushindwa kuhimili uzito wa mtoto, hali ambayo husababisha ujauzito kuharibika kabla ya muda wake.
Sababu nyingine ni utumiaji wa pombe kali, sigara na dawa za kulevya. Utumiaji wa vitu hivi huchangia mimba kutoka kutokana na kemikali nyingi zilizomo. Hivyo mwanamke mjamzito hushauriwa kutotumia  vitu vyenye kemikali, ili kulinda afya yake na mtoto aliyeko tumboni.
Pia baadhi ya vyakula na vipodozi huwa vina kemikali ambazo hupelekea shingo ya kizazi kulegea na kadiri mimba inavyozidi kukua huendelea kuachia na kusababisha mimba kushuka,hali inayosababisha mimba kuharibika.
Chromosome abnormalities, mimba nyingi ambazo huharibika hadi wiki ya ishirini husababishwa na tatizo hili la chromosomes, na chromosomes huwa zinabeba genes ambazo huyatambulisha maumbile ya mwanadamu kwa nje, yaani jinsia yake, ngozi yake itakuaje, macho yake na vitu vingine vingi nisingependa tuingie ndani sana lakini matatizo haya ya chromosomes huchangia sana kuharibika kwa mimba.

Maambukizi katika mji wa uzazi wa mwanamke {Infections}, kuna kitu kinaitwa Pelvic Inflammatory Diseases {PID} yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi nayo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba kwa mwanamke, lakini pia Candida au fangasi nazo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba. 

Chanzo kingine kikubwa ni utoaji wa mimba za mara kwa mara, wanawakie au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao pia hukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwani uingizaji wa vyuma ndani huweza kuharibu shingo ya kizazi ya mwanamke na pia kukumbwa na tatizo hili la miscarriage au kuharibika kwa mimba.


Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}, magonjwa kama gonorrhea, kaswende mara nyingi sana huathili mfumo wa uzazi wa mwanamke na hasa hasa kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kwa haraka zaidi na hivyo kusababisha tatizo hili la kutoka kwa mimba {Miscarriage}.

Chanzo kingine cha mimba kuharibika ni tatizo la kisukari kwa mwanamke, hii nayo huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibika kwa mimba na mtu ambaye hafanyi uangalizi wa karibu wa tatizo la sukari basi husababisha glucose isitumike kama energy na hivyo kuleta madhara katika kizazi hasa ujauzito.

Kitu kingine ni hormones {homoni} kuvurugika, kwa mfano hormone ya progesterone mara nyingi hufanya ile kazi ya kutunza mimba iendelee kukuwa, na kama kunatokea unbalance au kuvurugika kwa homoni hii basi mara nyingi tatizo hili la mimba kuharibika hutokea

DALILI ZA MIMBA KUHARIBIKA(SYMPTOMS OF A MISCARRIAGE)
kutokwa na damu sehemu za siri. Hiyo ni dalili kubwa ya mimba kuharibika ambapo damu hiyo hutoka sawa na  mwanamke anayekuwa kwenye siku zake.
Maumivu katika viungo ambayo huwa makali katika kiuno, nyonga na tumbo chini ya kitovu ambapo maumivu hayo huanza taratibu, lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele ambapo hali hiyo huambatana na kutokwa damu sehemu za siri.
Dalili nyingine ni kutokwa na uchafu sehemu za siri. Hii ni dalili kubwa ya mimba kutoka. Mama mjamzito kuanza kutokwa na uchafu mwingi wenye rangi sambamba na mabonge ya damu.
Kupata maumivu ya kiuno huku ukisikia maumivu hayo yanashuka chini kwa nguvu fahamu fika mimba yako inaweza kutoka muda wowote.
 Homa. Unaweza kupata homa kama mji wa uzazi ukipata maambukizi wakti mimba inaharibika.


MADHARA YATOKANAYO NA KUHARIBIKA KWA MIMBA
Iwapo mama mjamzito amepata tatizo hili  na hajapata tiba sahihi kama kuna mabaki tumboni yanaweza kusababisha madhara mengine ikiwemo kizazi kuoza au kusababisha matatizo mengine kwenye mji wa mimba.
Miongoni mwa madhara yanayoweza kumpata mama ambaye mimba imeharibika ni pamoja na kizazi kuharibika ikiwa mama hatasafishwa vizuri tumboni baada ya mimba kuharibika.
Madhara mengine ni kuugua mfululizo baada ya ujauzito kuharibika pamoja na kushambuliwa na madhara mfululizo baada ya ujauzito kuharibika.
Pia mama anaweza kupata madhara ya kisaikolojia ambayo yanachukua muda mrefu kusahaulika hasa pale wanapokutana na wanawake wajawazito au wenye watoto.

USHAURI
Endapo mama huyo atachelewa atakuwa anajiweka katika hali mbaya kutokana na sumu inayotokana na kiumbe kilichoharibika  na kusababisha matatizo kwenye mfuko wa uzazi ikiwemo ugumba.
Mwanamke yeyote ambaye hajapata tatizo hilo anashauriwa kula vyakula kama maboga,  mboga za majani na vyakula vyote vinavyojenga mwili.Pia wanatakiwa kuacha matumizi ya vipodozi vyenye kemikali  pamoja na uvutaji wa sigara  na dawa za kulevya ili kujikinga na tatizo la kuharibika kwa mimba.

1 Comments

Previous Post Next Post