Ute sehemu za siri na maana zake


Image result for vaginal discharge
Kila mwanamke katika maisha yake kuna muda anatokwa na ute katika viungo vyake vya uzazi,ute huu unaweza kuwa wa kawaida au ute unasababishwa na magonjwa.


Ute wa kawaida ni ule ute unaotokea kwa sababu ya mifumo mbali mbali mwilini(physiological processes) Mara nyingi ute wa kawaida huwa hauambatani na muwasho sehemu za siri.Ute unaosababishwa na magonjwa huu mara nyingi huambatana na muwasho sehemu za siri na saa nyingine harufu kali,japo yapo magonjwa mengine yanayopelekea kutokwa na ute usioambatana na muwasho.

Asilimia kubwa ya wanawake hawajui jinsi ya kupambanua ute upi ni wa kawaida na upi ni sababu ya magonjwa.Leo nitazungumzia kuhusu ute wa kawaida.

  UTE USIOKUWA NA MUWASHO UNAWEZA KUWA SABABU YA MIFUMO YA UTENDAJI KAZI WA MWILI AU UNAWEZA KUWA SABABU YA MAGONJWA


UTE WA KAWAIDA


Kama tunavyojua uke ni kama njia inayounganisha kati ya viungo vya ndani vya uzazi mfano mji wa mimba na viungo vya nje. Kuta za uke huwa zinazalisha ute ute au majimaji,kuna kipindi maji haya yanaweza kutoka nje ya uke hali inayowafanya watu wasiojua kupambanua aina ya ute kuhisi labda ni wagonjwa nk.

Ute huu unaozalishwa na kuta za uke unasaidia kuondoa au kutoa nje wadudu waletao magonjwa, Kuufanya uke kuwa na unyevunyevu muda wote,kufanya kiwango cha asidi au tindikali(PH) kuwa katika kiwango ambacho mbegu za kiume zinaweza kuvumilia endapo zitaingia zisife. Kikawaida PH ya uke ni ACIDIC ili kuzuia wadudu waletao magonjwa wasiweze kuingia na hali hii inasababishwa na wadudu wenye faida(normal flora) wanopatikana ndani ya uke kwa kila mwanamke.wadudu hawa ni kama Lactobacilli na candida albicans.

Ute huu ndani yake unakua pia na majimaji ya tishu, seli zilizokufa,protini na seli nyeupe za damu.

Normal Vaginal Organisms 

Ute huu wa kawaida unakua kama maji,hauna rangi na saa nyingine unaweza kuwa na kama mawingu(cloudy),ute huu ubadilika na kuwa na rangi inayoelekea kuwa kama njano pale unapokauka. Wingi wa ute huu huwa sio sana,unakua katika kiasi cha kulowanisha sehemu ya nje ya uke na kidogo nguo ya ndani na hauna harufu kali.

Ute huweza kuongezeka kwa kipindi fulani.Unaweza kuzalishwa kwa wingi katika hali zifatazo.


1.Siku za hatari ya kupata  mimba(ovulation) 

Kipindi hiki ndipo yai huachiliwa kutoka kwenye mfuko wa yai(ovary),kipindi hiki hormone ya estrogen inayozalishwa hufanya tezi zilizoko kwenye uke kuzalisha ute mwingi kwa lengo la kusaidia mbegu za kiume zinapoingia ziweze kusafiri kwa urahisi kulifata yai lililoachiliwa.Ute huu unakua hauna rangi,mzito na unaovutika,uko kama ute wa yai bichi.

Image result for ovulation vaginal discharge


KARIBIA NA HEDHI

Siku mbili au moja kabla ya kuanza bleed (Hedhi) wanawake hupata ute ambao unakua mzito kidogo na rangi yake inakua Inaelekea kuwa kama ya damu ya mzee(Brown), Siku unapoanza kupata kupata ute wa rangi hii ndo inakua siku ya kwanza kwenye mzunguko wako.
Hivyo unopata ute wenye rangi ya Brown siku unapokalibia siku za bleed ni kawaida.

Related imageWAKATI WA UJAUZITO

Kipindi cha ujauzito pia hormone ya estrogen inazalishwa kwa wingi ili kuimarisha mji wa mimba,hormone hii inafanya tezi za kuta za uke kuzalisha ute ute mwingi.ute wa kipindi hiki unakua hauna rangi au unakua na rangi kama mawingu na hauna harufu kali.ute huu huzalishwa kwa wingi kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito

Image result for leukorrhea discharge


WAKATI WA TENDO LA NDOA

Wakati wa ashiki ya tendo la ndoa uke huzalisha ute mwepesi ulio kama maji na unakua hauna harufu kali.


WAKATI WA BAREHE

Kipindi binti anavunja ungo anapata ute mwingi,kutokana na kuongezeka kwa uzalishwaji wa hormone za uzazi hasa hormone ya estrogen.


DAWA ZA UZAZI WA MPANGO

Pia matumizi ya dawa za uzazi wa mpango,hasa vidonge husababisha kuzalishwa kwa wingi ute.Ila unakua hauna rangi,harufu wala muwasho.


Bila shaka umeelewa jinsi gani ute wa kawaida unakuwa.Ute wowote unaoambatana na muwasho sehemu za siri na harufu kali ni dalili ya ugonjwa,upatapo hali hiyo vyema ukawahi hospitali ili kufanyiwa vipimo na kupata matibabu mapema.

1 Comments

  1. You must be conversant with all of the on line casino bonus phrases and circumstances. Deposit Bonus | This promotion is normally triggered when players make their first actual cash deposit on the on line casino website. Casinos usually supply deposit bonuses to motivate users to deposit extra 점보카지노 money into the account. Welcome Bonus| The welcome bonus is one of the|is among the|is probably one of the} greatest on line casino bonuses in online playing. Most of the time, it additionally has first rate wagering necessities.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post