Serikali ya Tanzania haitaongeza muda wa likizo ya uzazi , limeripoti gazeti la binafsi la The Citizen nchini humo.

Serikali ya Tanzania inasedma kuwa wanawake wanaojifungua mtoto mmoja wataendela kupewa 84 za likizo ya uzazi na wanaojifungua mapacha wakipata likizo ya siku 100
Serikali ya Tanzania haitaongeza muda wa likizo ya uzazi , limeripoti gazeti la binafsi la The Citizen nchini humo.
Naibu waziri wa afya Faustin Ndugulile ameliambia bunge kuwa wanawake wanaojifungua mtoto mmoja wataendela kupewa 84 za likizo ya uzazi huku wanaojifungua watoto mapacha wakipata likizo ya siku 100, limeeleza gazeti hilo.
Dr Ndugulile alikuwa akijibu swali kutoka kwa Mbunge wa chama kikuu cha upinzani Chadema Grace Tendega Jumanne ambaye aliiuliza serikali iwapo ina mipango ya kuongeza siku za likizo kwa akinamamawanaojifungua watoto njiti, linasema gazeti hilo linalochapishwa kiola siku.
Naibu waziri alisema kuwa wanawake wanaonyonyesha watapewa saa mbili kwa siku na kwamba serikali itaendelea kutekeleza sera yake ya afya ya mwaka 2007 juu ya vipengele vya huduma bure za afya kwa makundi maalumu, wakiwemo wanawake wajawazito , limesema The Citizens.
"Serikali inajitahidi kuboresha huduma mbali mbali za kujifungua. Kwa sasa tunatekeleza awamu ya pili ya mkakati wa kuinua afya ya watoto wachanga wakiwemo njiti," Dr Ndugulile alinukuliwa akisema.
Lakini wizara ya hiyo imekiri kuwa matibabu kwa watoto njiti nji ghali na kwamba maafisa watashughulikia suala hilo.

Je gharama ya uzazi katika baadhi ya mataifa Afrika mashariki ikoje?

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, takriban wanawake 830 hufariki kutokana na sababu zinazoweza kuepukika zinazohusiana na uja uzito na kujifungua ikiwemo gharama za kupokea hudumu za afya.
99% ya vifo hivyo vyote hutokea katika mataifa yanayoendelea. Je hali iko vipi kwa baadhi ya maatifa ya Afrika mashariki?

Kenya:

Kenya imekuwa ikishuhudia kiwango kikubwa cha vifo vya akina mama waja wazito. Kutokana na hilo serikali iliidhinisha sera ya utoaji huduma za bure kwa kina mama wanaojifungua katika taasisi za umma tagu Juni 2013.
Sera hii imekuwa ikiwawezesha wanawake waja wazito kupata huduma za bure wakati wa kujifungua katika vituo vya afya vya umma.
Mpango uliopo ni kwamba vituo hivyo vya afya hutoa huduma ya bure na baadaye serikali inavilipa kupitia wizara ya afya kulingana na idadi ya akina mama waliozalishwa.
Pia hakuna malipo yanayotolewa kwa huduma za kabla na baada ya kujifungua kwa akina mama na watoto kwa hadi wiki sita.
Licha ya huduma hiyo ya bure,kiwango cha hudumu zinazotolewa bado kinazusha maswali mengi huku baadhi ya wazazi katika hospitali hizo za umma wakiishia kujifungua katika hali duni na wengine hata kuishia kulala kitanda kimoja na wazazi wenzao.
Sio wengi wanaoweza kumudu gharama za hospitali za kibinafsi nchini.

Uganda:

Suala moja kubwa linalohusiana na afya ya uzazi ni nafasi ya akina mama kufikia huduma za dharura na za kiwango bora za uzazi na changamoto nyinginezo kwa wanawake nchini Uganda kufikia huduma hizi, zikiwemo gharama kubwa. Kama nchi nyingine nyingi zinazoendelea, Uganda inashuhudia kiwango kikubwa cha akina mama wanaofariki wakati wa kujifungua - jambo linalodhihirisha ufikiwaji wa huduma hizo za afya.
Hata wakati huduma hizo zinapatikana, kwa kawaida idadi ya wahudumu, dawa na vifaa hospitalini inakuwa ndogo ikilinganishwana idadi ya akina mama wanaohitaji hudumu hiyo.
Muongozo uliotolewa na shirika la Afya duniani ni kwamba mkunga mmoja anastahili kuwazalisha takriban wanawake 175 kwa mwaka, lakini wakunga nchini Uganda huwazalisha kati ya akina mama 350 hadi 500 kwa mwaka.
Upungufu na usambazaji mbovu wa wahudumu wa afya unaathiri kwa jumla gharama ya huduma ya afya ya uzazi na watoto.

Tanzania:

Idadi ya wanawake wanaofariki wakati wa uja uzito na kujifungua nchini Tanzania, kati ya 454 kwa kila visa 100,000 vya kujifungua - ni miongoni mwa zilizo kubwa duniani.
Licha ya kwamba serikali imeahidi kuisaidia hali, idadi hiyo ya vifo haijapungua.

Zaidi ya 70% ya raia Tanzania wanaoishi katika maeneo ya mashambani wana tatizo kufikia huduma za afyaHaki miliki ya pichaWATERAID/ELIZA DEACON
Image captionZaidi ya 70% ya raia Tanzania wanaoishi katika maeneo ya mashambani wana tatizo kufikia huduma za afya

Na zaidi ya asilimia 70 ya idadi jumla ya raia nchini wanaoishi katika maeneo ya mashamabani ambako wanatatizo kufikia huduma za afya.
Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya magonjwa katika maeno ya joto na afya ya umma kutoka chuo kikuu cha Heidelberg, Ujerumani kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Muhimbili, kwa jumla wazazi wanaopokea huduma hizo hugharamia malazi, madawa pamoja na usafiri.
Na usafiri hugharimu nusu ya kiwango jumla cha gharama nzima. Malipo yasiyo rasmi hayajumuishwi katika hesabu, na gharama nzima hutegemea huduma inayotolewa kutoka taasisi hata taasisi.

DRC:

Licha ya ufadhili wa kimataifa, kiwango cha huduma za uzazi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imezongwa na miongo kadhaa ya vita vya kiraia nchini pamoja na kudorora kwa hali za kijamii na kiuchumi na miundo mbinu duni.
Kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni ya serikali, takriba 40% ya akina mama waliojifungua Kinshasa hawakujifungua katika hospitali za umma hali inayoashiria kuwa kiwango fulani walipokea huduam hizo katikataasisi zisizo chini ya wizara ya afya nchini.
Eneo la Ulaya ambapo wanawake 'hubeba mimba za biashara'
Miongoni mwa mambo yanayozingatiwa na mzazi kabla ya kutafuta huduma za uzazi asilimia 21 wanasema wamezingatia gharama za huduma hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post