Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.
Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa
Mwaka jana Ephraim Kibonde alimpoteza mkewe mama Sara Kibonde