Unywaji wa pombe kupitia kiasi sio mzuri kwa afya yako kitu kilichothibitishwa kisayansi miaka kadhaa iliopita.
Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni , utafiti umeonyesha kuwa imani za zamani kwamba glasi moja ya mvinyo wakati wa chakula ni muhimu ni potofu.
Tukiongezea athari za unyawaji wa pombe zinazidi kujulikana.
Na sasa kundi moja la wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Rutgers nchini Marekani pamoja na watafiti kutoka chuo cha Yale nchini Marekani wamegundua kwamba unywaji wa pombe unaweza kuathiri chembechembe zetu za DNA na kutufanya tuhisi kutaka kubugia pombe zaidi.
Wengi pia wanahoji kwamba kinywaji kimoja kina athari mbaya kwa afya yetu.
Ukinywa unazidi kuwa na hamu ya kuendelea.
Kufikia hapo kundi hilo la watafiti liliamua kuangazia uchanganuzi wake katika jeni mbili zinazohusiana na kudhibiti tabia wakati tunapokuwa chini ya shinikizo la pombe.
Moja ni ile ya PER2 inayoshawishi maisha ya miili yetu na nyengine ya POMC, ambayo inadhibiti utaratibu wetu wa kukabiliana na dhiki.
Ukilinganisha wanywaji wa kadri na wale wanaobugia pombe kwa wingi, wanasayansi wamegundua kwamba jeni za watu wanaokunywa pombe kwa wingi hubadilika.
Kwa wale wanaobugia kwa wingi, jeni zao hutoa protini polepole na hupata hamu ya kunywa wakati wanapokumbwa na matatizo
Kwa nini watu hupendelea kunywa ili kukabiliana na matatizo?
Mabadiliko ya jeni huongezeka kutokana na vinywaji zaidi.
Unapobugia pombe zaidi unazidi kuharibu jeni hatua inayotufanya kuwa na hamu ya kunywa pombe zaidi na zaidi.
"Tumegudua kwamba watu wanaokunywa pombe nyingi wanabadilisha chembechembe zao za DNA katika njia inayowafanya kutaka kunywa zaidi'', alisema Profesa Dipak K Sarkar, mwanzilishi wa utafiti huo unoaongozwa na chuo kikuu cha Rutgers.
"Hii inaweza kusaidia kuthibitisha kwa nini pombe ina mvuto mkubwa'', aliongezea
Watafiti wanatumai kwamba ugunduzi wao utawaruhusu kutambua viashiria vinavyoweza kupimwa kama vile protini au jeni zilizobadilishwa kutabiri hatari ya mtu anayekuwa na unyawaji wa kiwango cha juu mna vile atavyolindwa asiweze kunywa zaidi.