Matibabu ya macho kwa kutumia antibiotiki (viua vijasumu)
Watoto Wachanga na Unyonyeshaji: Madawa
Dawa ya antibiotiki ya aina ya mafuta na ya matone hutumika kulinda macho ya mtoto mchanga dhidi ya maambukizi makali na hata upofu ambao unaweza kutokea wakati wakuzaliwa iwapo mama yake atakuwa na maambukizi ya kisonono, ugonjwa unaoambukizwa kupitia ngono. Hutumika pia kutibu maambukizi ya macho yanayosababishwa na bakteria.
Jinsi ya kutumia
Tumia moja wapo ya dawa ya antibotiki ya mafuta (ointment):
Asilimia 1 ya dawa ya mafuta ya tetrasaikilini AU asilimia 0.5 hadi asilimia 1 ya erithromaisini h Weka mchirizi mwembamba wa dawa kwenye kila jicho mara moja tu, ndani ya saa 2 baada ya kuzaliwa. Polepole vuta chini kigubiko cha chini na kukamuliwa kwenye jicho mchirizi mwembamba wa dawa ukianzia kwenye kona ya ndani na kuelekea nje. Usiruhusu ncha ya tyubu ya dawa kugusa jicho la mtoto.

Mchanganyiko wa asilimia 2.5 wa povidoni na aidini (povidone-iodine) au tone 1 la asilimia 1 ya mchanganyiko wa silva naitreti (silver nitrate). Weka tone moja katika kila jicho, mara 1 tu ndani ya saa 2 baada ya kuzaliwa. Vuta nje kigubiko cha chini na kukamulia ndani ya jicho tone 1 la dawa. Usiruhusu bomba la dawa au chupa kugusa jicho.
Silva naitreti huzidi kukolea kupitia mvukizo inapokaa sana– hivyo usitumie silva naitreti ya zamani. Inaweza kumuunguza mtoto machoni. Kama huna uhakika, ni bora kuepuka kabisa kutumia silva naitreti.