Kwa nini watu wengi wanazidi kufariki kutokana na majeraha ya kuumwa na nyoka

Mtumbuizaji wa nyoka nchini India
Makumi ya maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka.
Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika.
Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya.
Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu.
Waathiriwa huwa hawapati dawa kwa wakati ufaao. Katika matukio mengine, hupewa dawa ili kutibu jeraha lililosababishwa na nyoka tofauti.
Takriban watu 11,000 kila mwezi hudaiwa kufariki kutokana na kung'atwa na nyoka -ikiwa ni sawa na idadi ya watu waliofariki na ebola katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016.
Watu wengine 450,000 zaidi kwa mwaka hudaiwa kupata majeraha yanayobadili maisha yao kama vile kukatwa mguu ama hata kupata ulemavu.
Kiwango hicho cha matatizo kinamaanisha kwamba majeraha yanayosababishwa na kuumwa na nyoka sasa yanafaa kupewa kipao mbele baada ya kusahaulika kwa muda mrefu.

Ni nani anayeumwa na nyoka?

Watoto wanaoelekea shule huenda wako hatarainiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatoto wanaoelekea shule huenda wako hataraini
Katika maeneo yalioendelea kama vile Ulaya, Australia na Marekani kaskazini, ni watu wachache wanaoifariki kutokana na majeraha ya kuumwa na nyoka , licha ya kuwa na nyoka wengi tofauti wenye sumu kali zaidi.
Hiyo inalinganishwa na vifo 32,000 katika eneo la jangwa la Sahara na mara mbili ya kusini mwa bara Asia.
Jamii nyingi zilizopo maeneo ya tropiki ziko katika hatari ya kuumwa na nyoka uwanjani, wakiwa wanatembea na hata usiku wakiwa wanalala nyumbani kwao.
Wakulima vijana ndio walio katika hatari kubwa zaidi, wakifuatiwa na watoto.
Huku idadi kubwa ya watu wanaoishi mashambani wakiwa hatarini, mbinu za kiafya zinazotumiwa katika maeneo ya bara Afrika na Asia haziwezi kukabiliana na janga hilo.
Mafunzo ya kiliniki , usafiri wa dharura na dawa za bei nafuuhuwa havipatikani mtu anapoumwa na nyoka.
Takimu muhimu za kuumwa na nyoka

Dawa ghali.

Kung'atwa na nyoka kunasababisha dalili zinazoweza kuhatarisha maisha yako ikiwemo kutokwa na damu, kupooza na uharibifu wa tishu zisizoweza kurekebishwa.
Ni muhimu kwa waathiriwa wa majeraha ya nyoka kupata dawa zinazohitajika haraka iwezekanavyo baada ya kuumwa.
Antivenom ama dawa ya kukabiliana na sumu ya nyoka ndio inayohitajika kutibu majeraha ya kung'atwa na nyoka.
Dawa hiyo hutengenezwa kwa kutumia sumu ya nyoka aliyesababisha jeraha.
Hatua hiyo inamaanisha kwamba dawa tofauti inahitajika , kwa sababu kuna nyoka wenye sumu kali tofauti kama vile, Cobra, mambas, Kraits, Vipers na Pi Vipers kwa uchache.
Sumu zinazopatikana katika sumu hiyo ya nyoka huwa tofauti kutokana na maeneo.
Hiyo inamaanisha kwamba dawa ya kutibu majeraha ya kuumwa na nyoka ni vigumu kupatikana na inaweza kuwa ghali mno.
Presentational grey line

Jinsi dawa za sumu ya nyoka zinavyoundwa.

Kiwango kidogo cha sumu ya nyoka hudungwa katika mnyama kama vile farasi ama punda.
Hatua hiyo huchochea kinga ambayo hupigana na sumu hiyo ndani ya mwili wa mnyama.
Kinga hiyo hutolewa katika damu ya wanayama hao , kusafishwa na kufanywa kuwa dawa ya kukabiliana na sumu hiyo.
Dawa hizo zinapaswa kutumiwa ndani ya hospitali kwa huwa na madhara makali kwa mgonjwa.
Presentational grey line
Katika maeneo ya Latin Amerika , dawa za kukabiliana na sumu kali ya nyoka hutengenezwa na kugharamiwa na serikali.
Viwango vya vifo viko juu katika maeneo ya jangwa la Sahara barani Afrika ambapo dawa ya kukabiliana na sumu ya nyoka huuzwa kwa kati ya $140 hadi $300 (£108 to £233) kwa chupa, huku kati ya chupa tatu hadi 10 zikihitajika kuokoa maisha ya mwathiriwa.
Kwa mkulima wa Kiswazi anayepokea mshahara wa $600 kwa mwaka, hawezi kugharamia dawa hiyo.

Dawa ya sumu ya nyoka isio sahihi

Nyoka mdogo aina ya pit viperHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNyoka mdogo aina ya pit viper
Hali hiyo imesababisha kupatikana kwa dawa hafifu ama zile zisizo sahihi katika soko katika kipindi cha muongo mmoja ulioipita hususan barani Afrika.
Dawa hizo huuzwa kwa dola 30 kwa chupa.
Bidhaa hizo zilianza kutumika katika hospitali katika maeneo mbali mbali ya bara Afrika.
Hatahivyo kuna ripoti nyengine kwamba baadhi ya dawa hizo huenda hazina uwezo wa kutibu sumu ya nyoka.
Tafiti ndogo ndogo kutoka hospitali nchini Ghana na Jamhuri ya Afrika ya kati CAR zinasema kuwa wakati dawa hizo za bei rahisi zilipotumiwa vifo viliongezeka kutoka asilimia 2 hadi asilimia 10.
Mara nyingi dawa hizi za nyoka hutengenezwa kwa kutumia sumu za nyoka kutoka maeneo tofauti ikilinganishwa na mahali ambapo dawa hizo huuzwa- kwa mfano dawa ya nyoka ilioundwa na sumu ya nyoka wa India inauzwa Afrika.
Nyengine hutengezwa kwa kutumia sumu sahihi lakini ikiwa na kiwango kidogo cha kinga mwilini hatua inayofanya dawa hiyo kuwa hafifu kutibu mtu aliyeng'atwa.
Hii inamaanisha kwamba idadi ya chupa za dawa hiyo zinazohitajika ili kufanikiwa kutibu mgonjwa zinaongezeka kutoka 10 hadi 20 ama hata 30.
Ukosefu wa kufanya majaribio.
Eyelash viperHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEyelash viper
Matatizo haya yamesababaishwa na ukosefu wa kufanyia majaribio dawa hiyo.
Dawa nyingi lazima zifanyiwe vipimo ili kuthibitisha zinaweza kutibu. Lakini hili halifanyiki na dawa za kutibu sumu ya nyoka.
Mamlaka ya kusimamia dawa mara nyingi huidhinisha dawa hizi bila kuwa na ushahidi wa iwapi zinaweza kutibu ama hata kulinganisha na matibabu mengine.
Ili kukabiliana na tatizo hilo, Shirika la Afya Duniani WHO limezindua mpango wa kujaribu dawa hiyo huku matokeo yake yakitarajiwa kuchapishwa baadaye mwaka huu.
Mpango huo utarahusu wizara za afya , wauzaji dawa kuelewa ni dawa gani za kukabiliana na sumu ya nyoka zinazohitajika katika eneo hili, mbali na kutafuta watengenezaji wanaoweza kutengeneza dawa hizo kwa bei rahisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post