Sababu za muwasho ukeni

Kuwasha na kuchoma choma kwa uke mithili ya moto ni tatizo linalowaumiza sana wanawake na kuleta usumbufu mkubwa. dalili hizi zinaweza kuwa ni matokeo ya tatizo kubwa la kiafya ndio maana kuna umuhimu wa kumwona dactari mapema pale unapoona hali imezidi kuwa mbaya. Kwenye makala yetu ya leo tutajifunza
  • Nini husababisha Muwasho ukeni, kuchomachoma na kuvimba
  • Namna tatizo linavotibiwa na
  • Tiba ya nyumbani unayoweza kutumia kupunguza makali ya tatizo na kuzuia

Nini Husababisha Uke Kuwasha, kuchomachoma na kuvimba

Kuna sababu nyingi zinazopelekea muwasho ukeni ambazo ni pamoja na
  1. Maambukizi ya bacteria ukeni (bacterial vaginosis)

    Maambukizi ya bacteria ukeni ni moja ya maambukizi yanayowatokea mara kwa mara wanawake. Wengi wanaoathirika ni wale wanaojihusisha na ngono zaidi, wenye kinga dhaifu na wajawazito. Watafiti wanasema kinachosababisha Bacterial vaginosisi ni kuvurugika kwa uwiano wa viumbe kwenye mazingira ya uke (vaginal microflora) ambayo inahusisha uwepo wa bacteria na fangasi pia.
    Kuvurugika huku kwa mazingira ya uke kunaweza kuletekekezwa na sababu nyingi ikiwemo, kudhoofika kwa kinga ya mwili na mabadiliko ya pH- kikawaida uke una tindikali zaidi 3.8-4.2 ni kawaida na pH zaidi ya 4.5 siyo salama kwa afya ya uke.
  2. Magonjwa ya Ngono (Sexual transmitted Diseases)

    Magonjwa haya ni pamoja na Chlamydia, genital herps, genital warts, trichomoniasis, na gonorrhea yote huletekeza dalili za kuwasha ukeni na kuchomachoma.
  3. Fangasi Ukeni (Vaginal Candidiasis)

    Kila mwanamke yupo kwenye hatari ya kuugua fangasi ukeni na tafiti zinasema kwamba karibu kila mwanamke hupata fangasi ukeni katika kipindi fulani kwenye maisha yake. tatizo hutokea pale fangasi wa candida wanavokuwa kupita kiasi kwenye uke na mashavu ya uke. Makundi yaliyopo kwenye hatari ya kupata fangasi ukeni ni pamoja na wajawazito, wanaofanya ngono mara kwa mara, wanaotumia zaidi madawa na wenye kinga hafifu.
  4. Kukoma Hedhi-Menopause

    Wanawake waliokoma hedhi hupata shida ya uke kukauka, misuli ya uke kulegea na kuwasha kutokana na kupungua uzalishaji wa homoni ya estrogen.
  5. Matumizi ya Vifaa Vyenye Kemikali

    Vitu vingi vinavyotumika kila siku mfano sabauni, condom, toilet paper, wipes, na cream zina madhara makubwa kwa afya ya mwanamke, kwani huvuruga homoni na kuleta matatizo kama ugumba na kuwasha kwa uke.

Vipimo ili Kugundua Uwepo wa Tatizo

Mara nyingi tatizo ua kuwasha ukeni huisha ndani ya siku chache baada ya kuanza. Kama tatizo litaendelea na dalili kuwa kali zaidi wek apointment uonane na dactari kupata vipimo na tiba. Dactari atafanya pelvic examnation ambapo atangalia dalili anazopata mgonjwa kwenye via vya uzazi (eneo la nje la uke, mfuko wa mimba, mlango wa kizazi, mirija ya uzazi, kibofu cha mkojo na mifuko ya mayai, ) Dactari pia anaweza kuchukua sampuli ya uchafu unaotoka na kuufanyia vipimo ili kugundua chanzo cha tatizo.
Kwa hivo tiba ya tatizo hili la kuwasha kwa uke itategemea na chanzo ama ugonjwa unaosababisha kama ugonjwa ni
  • Maambukizi ya bacteria (Bacterial vagoniosis): mgonjwa hupewa antibitics na antiparastis ili kuua vimelea vya ugonjwa
  • Yeast infection (candidiasis): mgonjwa hupewa daw za kuua fangasi, antifungal ambazo humeza na zingine kuweka ukeni.
  • Menopause: kama chanzo ni kukoma hedhi basi mgonjwaanaweza kupata dawa na virutubisho vya kuongeza uzalishaji wa homoni ya estrogen.

Ushauri wa Kufuata na Tiba Mbadala kama Unapata Shida ya Muwasho Ukeni.

Zifuatazo ni hatua za kuchuka ili kuzuia na kutibu muwasho ukeni.
  • Epuka kuvaa pedi, kutumia cream na spray zenye harufu kali tabia hizi zinaharibu mazingira ya ukeni na kutoa mwanya wa fangasi na bacteria kukua.
  • Tumia maji na sabuni zisizo na kemikali kujisahfisha ukeni na usioshe uke zaidi ya mara moja kwa siku.
  • Siku zote unapojisafisha ukeni ama ehemu ya haja kubwa basi jifute kuanzia mbele kwenda nyuma. kufanya hizi inazuia kusambaa kwa bacteria walioko mkunduni kwenda ukeni.
  • Vaa nguo za ndani za pamba ambazo huruhusu hewa kupita na kukausha unyevu ambao ni mbolea kwa fangasi na bacteria wabaya.
  • Epuka kufanya douching
  • Kwa watoto wadogo, wabadilishiwe diepers zao mara kwa mara
  • Tumia condom ili kujikinga na magonjwa ya zinaa
  • Usifanye ngono mpaka pale uatakapopona ugonjwa unaosababisha upate muwasho ukeni.
  • Onana na Daktari haraka pale unapoona dalili zisizo za kawaida kama kutokwa na uchafu unaonuka mfululizo, kuwasha kwa uke, kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya nyonga na mabadiliko kwenye hedhi.

Post a Comment

Previous Post Next Post