Kwanini wanawake hulewa haraka kuliko wanaume?

Watu wanaokunywa pombe
Wanaume walikuwa wakiheshimika kuwa wanywaji wa pombe wa kupindukia katika jamii ya nchi za Magharibi - walijulikana katika utamaduni wa Don Draper kuwa wanaume wenda wazimu waliobugia pombe kwa wingi baada ya kazi katika kilabu ambazo wanawake wengi wasingethubutu kuingia.
Lakini wataalam wa magonjwa wamedai kwamba ongezeko la matangazo ya pombe miongoni mwa wanawake mbali na mabadiliko ya majukumu ya kijinsia yameleta usawa miongoni mwa watu wa jinsia tofauti wanaobugia bidhaa hiyo.
Kwa jumla, wanaume bado ni mara mbili zaidi ya wanawake katika ubugiaji wa pombe, lakini hiyo si ukweli miongoni mwa vijana.
Ukweli ni kwamba wanawake waliozaliwa kati ya 1991 na 2000 wanakunywa pombe nyingi sawa na wenzao wanaume na viwango vya ubugiaji pombe huenda vikapita vile vya wanaume.
Hatahivyo miili ya wanawake huathiriwa na pombe tofauti na ile ya wanaume.
Wanawake wanaendelea kuathirika kutokana na athari mbaya za pombe.
PombeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Data ya kitaifa inaonyesha kwamba viwango vya vifo asilimia 57 miongoni mwa wanawake vinatokana na ini lililoathirika kutokana na pombe ama hepatitis miongoni mwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 45-64 kutoka 2000 hadi 2015 nchini Marekani ikilinganishwa na asilimia 21 ya wanaume.
Na ilipanda kwa asilimia 18 miongoni mwa wanawake walio na umri kati ya 25-44, licha ya kuongezeka kwa asilimia 10 miongoni mwa mwanaume wenye umri kama huo.
Viwango vya wanawake watu wazima vinavyozuru hospitalini kwa dharura baada ya kubugia pombe kupitia kiasi vimeongezeka. Ubugiaji wa pombe wa kiwango cha hatari umeongezeka miongoni mwa wanawake.
Lakini tatizo sio kwamba wanawake wanakunywa sana, watafiti wamegundua kwamba miili ya wanawake inaathirika tofauti ikilinganishwa na miili ya wanaume.
Viwango vyao vya mafuta mwilini vinamaanisha kwamba wanawake huathirika tofauti na pombe ikilinganishwa na wanaume.
Wanasayansi wamegundua kwamba huzalisha viwango vya chini vya enzyme kwa jina alcohol dehydrogenase (ADH), ambavyo hutoka ndani ya ini na kuvunja vunja pombe mwilini.
Tafiti zote za pombe zilifanyiwa wanaumeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wakati huohuo mafuta huzuia pombe huku maji yakitumika kuitoa mwilini. Wanawake wanaokunywa kupitia kiasi hupatikana na matatizo ya kiafya kwa haraka ikilinganishwa na wanaume.
Wanawake walio na tatizo la unywaji pombe hujipata wakinywa pombe tena katika miaka ya uzeeni zaidi ya wanaume , lakini huchukua muda mfupi kupenda pombe.
Wanawake pia hupata ugonjwa wa ini ule wa moyo na kuathirika neva zao ikilinganishwa na wenzao wa kiume.
Tofauti hii kubwa ya kijinsia kuhusu athari ya pombe mwilini hazikugundulika hadi miongo ya hivi majuzi.
Utafiti wa mapema kuhusu tofauti za kijinsia ulifanyika 1990.
Na kwa sababu tatizo la unywaji wa pombe lilionekana kuwa la wanaume, hakuna mtu aliyejali kwamba kuna kitu wanakosa kutoka kwa wanawake.
Hilo lilibadilika wakati taasisi za serikali kama vile taasisi ya kitaifa ya afya nchini Marekani ilipoagiza kwamba wanawake na wasio wengi walifaa kushirikishwa ili kufanyiwa utafiti , hatua iliolazimu tofauti za kijinsia katika tafiti za matibabu kuanzishwa.
''Wanasayansi walidhani kwamba unapowafanyia wanaume utafiti, matokeo yake pia yatawaathiri wanawake'', alisema Sharon Wilsnack. watu hawakuwafikiria wanawake , alisema Sharon Wilsnack .
Mwanamke anayekunywa pombeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Akisomea shahada yake ya uzamivu katika chuo kikuu cha Havard nchini Marekani mapema miaka ya 70 , Wilsnack aliandika kuhusu wanawake na pombe: huku akiruhusiwa kufanya tafiti saba katika chuo hicho.
Akiwa na mumewe, mwanasosholojia Wilsnack aliongoza utafiti wa kitaifa kuhusu tabia za wanawake za unywaji pombe.
Miongoni mwa matokeo ya utafiti wake ni ugunduzi kwamba wanawake wanaotumia pombe hunyanyaswa kijinsia kama vile watoto , tofauti ya kijinsia ambayo sasa imeonekana kuwa muhimu katika kuwasaidia wanawake wanaobugia pombe kupitia kiasi.
Tafiti nyengine za kijinsia tangu wakati huo zimetoa matokeo mengine ya kingono.
Kufikia mwaka 2000, uchunguzi wa ubongo wa watu wanaokunywa pombe sana , ulibaini kwamba ubongo wa wanawake walevi huathirika zaidi na pombe zaidi ya ule wa wanaume.
Baadhi ya wanawake walikuwa wamekunywa pombe mara tano , sita na hata mara kumi na walikuwa wakisema vitu kama vile , huu ni ujumbe ambao sijawahi kuusikia, na sikujua kwamba ninaathirika zaidi ya wanaume ninapokunywa pombe ama bidhaa hiyo huniathiri tofauti.

Post a Comment

Previous Post Next Post