Faida za ukwaju kwenye ngozi

Image result for sabuni ya ukwaju
Warembo wengi wakitanzania wamekuwa wakihangaika sana hadi wanatia huruma.
Wanatumia gharama nyingi, muda mwingi na mpaka kuhatarisha afya zao katika harakati za kujaribu kujirembesha…..
lakini wapi!
Warembo hao wamekuwa wakitumia sabuni (na vipodozi vyengine) ambazo zinatangazwa na kuaminika na watu wengi kuwa na faida nzuri kwenye ngozi na miili yao kwa ujumla lakini ni chache zenye kufanya hivyo.
Japokuwa sabuni za urembo wanazonunua ni za kisasa, zenye kunukia na kuvutia machoni,  wingi wa sabuni hizo zina madini ya mercury pamoja na hydroquinone  ambazo husababisha athari mwilini ikiwemo magonjwa ya ini pamoja na figo.
Vile vile kemikali hiyo ya hydroquinone husababisha ngozi kukunjana kama mzee, kutokwa na michirizi na mabaka mwilini ( hivyo ngozi kupoteza uhalisia wake) na mpaka kusababisha kwa namna moja au nyengine kansa ya ngozi (melanoma).
Hydroquinone ni nini?
Hydroquinone ni kemikali inayopatikana kwenye sabuni na vipodozi vingi venye za kuondoa mabaka na kufanya ngozi kuwe nyeupe.
Kwa hivyo kabla ya kununua sabuni au kipodozi chochote chenye kusifika kufanya ngozi yako kuwa nyeupe, hakikisha unasoma ina virutubisho gani. Kama ina hydroquinone, basi ni vyema kujiepusha nayo kwani utakuwa unacheza kamari na ngozi na mwili wako kwa ujumla.
Usihofu lakini…..
Sina lengo la kukutisha kwa kukwambia maneno haya,
….. hapana.
Lengo langu ni kukuelimishia na kukujuza kuwa
sio kila kinachong’ara ni dhahabu“.
Na vile vile kukujuza kuwa zipo sabuni (na vipodozi) vyengine visivyong’ara venye kuleta faida kubwa kuliko hizo za kisasa na kukufanya uwe na afya nzuri kwenye ngozi na mwili wako kwa ujumla.
Na leo nataka nizungumze na wewe kuhusu …..

Sabuni ya Asilia Ya Tunda la Ukwaju na faida zakeFaida Za Sabuzi Ya Ukwaju

Tunda la ukwaji (kwa kiingereza tamarind) ni tunda linalopatikana kila kona huku Tanzania.
Wengi wetu tumelizoea tunda hilo katika ice cream (za kibongo) hususan tulivyokuwa watototo.
Mbali na kuwa juisi na ice cream tamu kuna faida nyingi zinazopatikana kutokana na tunda hili.
Baadhi ya faidi ni:

1.Kupambana na Saratani ya Ngozi.

Tunda la ukwaju ni chanzo kikuu cha vitamini C.
Moja ya kazi kubwa ya vitamini C ni kupambana na vimelea vya kansa kwa kukausha uvimbe wa kansa ile na kuyageuza na kuyafanya magamba yenye kubambuka ndani ya wiki 2 (inaweza kuzidi au kupungua kidogo kutegemea na ukubwa wa uvimbe). [Chanzo: Cancer Tutor]
Vitamin C vile vile ni anti-oxidant (molekuli zinazozuia molekuli nyenginezo kupoteza elektroni) ambayo huzuia madhara yanayosababishwa na free radicals (molekuli zilizokuwa hazijashikana na molekuli nyengine) yenye kuharibu chembe chembe za mwili.

2.Hutibu Madhara Yanayotokana na Vipodozi vya kemikali.

Warembo wengi wanapenda kuwa weupe kwa kutumia vipodozi au sabuni bila ya kufahamu kuwa vipodozi hivyo vina kemikali ya hydroquinone.
Hydroquinone inasababisha kansa kwa kuuwa melanin (chembe chembe za rangi kwenye ngozi) kama nilivyoeleza hapo awali.
Mbali na kansa, sabuni hizo (na vipodozi) vyenye kemikali ya hydroquinone husababisha:
  1. mwili kutoka mabaka na michirizi
  2. Ngozi kuwasha na kuvimba
Sabuni ya asilia iliyotengenezwa kwa ukwaju inaweza kuondoa madhara hayo ndani ya muda mfupi sana kwa (eleza jinsi gani inafanya hivyo).

3. Hutakatisha ngozi yako.

Tunda la ukwaju lina kiungo kiitwacho  AHA (Alfa Hydroxy Acid) ambayo husafisha ngozi kwa kuondoa seli zilizokufa.
Japokuwa sabuni za viwandani zina kiunga hicho cha AHA, kiungo hicho si asilia (yaani kinatengenezwa kiwandani (synthetic)) na mara nyingi hufanya ngozi iwe inachonyota.
Matumizi ya vipodozi vya kemikali, kuchomwa na jua muda mrefu, madhara ya madawa ya hosipitali pamoja na mziho husababisha ngozi kuchafuka na kuwa na mabaka meusi. (hapa sijaelewa ulikuwa unataka kusema nini. Irekebisha, au kama unaona haina haja ifute)

4.Hupunguza makunyanzi usoni.

Kwa msaada wa vitamin B na AHA zilizopo ndani ya tunda la ukwaju vitundu vya hewa kwenye ngozi hufunguka na kuruhusu mpishano mzuri wa hewa hivyo ngozi huwa na unyevu masaa yote na makunyanzi kutoweka.

5. Husawazisha ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye kidonda.

Kama nilivyoeleza hapo awali tunda la ukwaju lina kiungo cha AHA yenye faida ya kuondoa seli za ngozi zilizokufa, kitu ambacho husaidia kuondoa makovu mwilini inayosabaishwa na vidonda, majibu na kuungua kwa moto.

6.Huondoa chunusi na harara.

Tunda la ukwaju limo katika orodha ya matunda yaitwavyo “Anti Inflammatory Fruits yenye sifa ya kuponesha vidonda, majibu na kuungua kwa moto.
Hufanya hivyo kwa acid iliyonayo kufyonza mafuta ya ziada katika ngozi hivyo huzuia chunusi (ambazo hutokana na mafuta yaliojirundika chini ya ngozi yasiyo na kazi kwenye ngozi) na harara.

7.Hutibu vivimbe vinavyosababishwa na kuumwa na wadudu.

Kwa vile tunda la ukwaju ina sifa ya kuwa ni ‘Anti-Inflammatory‘ vile vile ina uwezo wa kufyonza sumu kwenye ngozi iliyoachwa na mdudu baada ya kukuuma.

8.Hung’arisha na kulainisha ngozi kwa muda mfupi sana.

Kwa vile ukwaju una kirutubisho cha AHA, chembe chembe za ngozi zilizokufa na uchafu huondolewa haraka na kufanya ngozi yako kuwa laini na kung’ara mara moja.

9.Husaidia kuzibua matundu ya jasho na kuifanya ngozi iwe na unyevunyevu siku nzima.

Matundu ya jasho yanaruhusu majasho kutoka mwilini endapo joto la mwili litazidi. Ikiwa matundu hayo yataziba, bacteria watakusanyika na kusababisha majibu na uvimbe.
AHA iliyokuwemo ndani ya ukwaju husaidia kuzibua matundu hayo na kuruhusu majasho kutoka bila ya matatizo yoyote

Post a Comment

Previous Post Next Post