Kundi la kwanza la madaktari kutoka Cuba ambao wameombwa na serikali ya Kenya kuanza kufanya kazi nchini humo kupunguza uhaba wa madaktari wamewasili nchini humo.
Madaktari hao 50 waliowasili Nairobi wengi wao ni wanawake.
Walilakiwa na Gavana wa jimbo la Kisumu ambaye zamani alihudumu kama waziri wa afya Prof Anyang' Nyong'o na Dkt Rashid Aman, afisa mkuu msimamizi katika wizara ya afya katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Jumanne usiku.
Tanzania kuisaidia Kenya na madaktari
Madaktari wa Tanzania wakataa kwenda Kenya
Tanzania kuajiri madaktari waliofaa kutumwa Kenya
Madaktari hao kutoka Cuba wamewasili huku bado kukiwa na utata kuhusu mazingira yao yakikazi na malipo, ikiwa ni pamoja na huduma watakazopokea kutoka kwa serikali kwa mfano malazi.
Chama cha madaktari nchini Kenya kimelalamika kwamba madaktari hao wanathaminiwa na kulipwa mishahara ya juu kuliko madaktari wazawa wa Kenya.
Dkt Aman amesema madaktari wengine 50 watawasili nchini humo Alhamisi jioni.
"Tutawaandalia mafunzo ya kina, kuwafahamisha kuhusu Kenya, mfumo wetu na jinsi mambo huendeshwa hapa na pia kuhusu sekta ya afya humu nchini," alisema Dkt Aman.
Madaktari hao wataunganishwa na madaktari wenyeji kwa matumaini kwamba wataongezana maarifa.
Pacha walioshikana watenganishwa hospitali ya Kenyatta
Miongoni mwa madaktari wataalamu walio kwenye kundi hilo kutoka Cuba ni wataalamu watano wa figo, wataalamu wa x-ray, wataalamu wa mifupa na maungio na wataalamu wa mfumo wa neva.
Wizara ya afya imesema madaktari 50 kutoka Kenya wanatarajiwa kwenda Cuba kwa mafunzo zaidi Septemba mwaka huu.