
Madaktari kwenye hospitali moja iliyo jimbo la magharibi mwa Inida ya Gujarat wamefanikiwa kutoa meno saba kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja.
"Kwa sasa mtoto yuko sawa," daktari ambaye alifanya upasuaji huo Meet Ramatri alisema.Alisema kuwa upasuiji huo ulifanya kwa njia mbili. Kwanza walitoa meno manne, na baadaye matatu.
- Mtoto azaliwa kutoka kwa wazazi tasa
- Mtoto azaliwa kutoka kwa wazazi watatu
- Mtoto mchanga 'azaliwa' mara mbili
Wazazi wake walimpeleka kwa daktari wakati alipata matatizo ya kunyonya,

"Wakati nilimfanyia uchunguzi aligundua meno saba," Dr Ramatri aliambia BBC.
- Janet Jackson, 50, ajifungua mtoto wa kiume
- Mtoto aliyezaliwa ndani ya ndege atunukiwa safari za bure maishani
"Sasa mtoto huyo anaweza kunyonya," dakatari alisema, lakini aliongeza kuwa ni vigumu kujua ikiwa upasuaji huo utatatiza ukuaji wa meno ya mtoto huyo siku za usoni