Kichwa maji au hydrocephalus

Kichwa maji au hydrocephalus (kwa lugha ya  kitaalamu) ni mkusanyiko usio wa kawaida wa maji yanayojulikana kitaalamu kama (cerebral spinal fluid) kwenye ventrikali (ventricles) au nafasi zilizo wazi (cavities) kwenye ubongo.
Hali hii huweza kusababisha kuongezeka kwa shinikizo katika fuvu (increased intracranial pressure).  Hydrocephalus limetokana na lugha ya kigiriki ambalo humaanisha: Hudro - Maji , na Kephalos - Kichwa
Kichwa Maji (Hydrocephalus)
Kwa kawaida kwa kila mtu huwa na maji yanayoitwa kitaalamu cerebral spinal fluid kifupi CSF ambayo huzunguka ndani ya ventrikali za ubongo, nje na ndani ya ubongo na kuelekea kwenye uti wa mgongo (spinal cord) ambapo hufyonzwa na kurudi kwenye damu. Kichwa maji husababishwa na uzuiwaji wa mzunguko wa CSF, au kufyonzwa kwake au uzalishwaji wa CSF kwa wingi kupita kiasi kama kwenye papilloma of choroid plexus. Ikumbukwe ya kwamba kichwa maji huweza hata kusababisha kifo.
Kuna aina mbili za kichwa maji ambazo ni
Communicating hydrocephalus (Non obstructive hydrocephalus)
Aina hii husababishwa na kutokufyonzwa kwa maji ya CSF ingawa hakuna uzuiwaji wake wa mzunguko baina ya ventrikali na nafasi iliyopo kwenye ubongo inayojulikana kama Subarachnoid space. Hii inaweza kuleta madhara kama uvujaji wa damu baina ya ventrikali au kwenye Subarachnoid space, ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis) nk. Aina hii ya kichwa maji nayo imegawanyika katika sehemu mbili, ambazo ni
  • Normal Pressure Hydrocephalus (NPH) – Katika aina hii ventrikali za kwenye ubongo zimeongezeka ukubwa na kuongeza pressure ya CSF.
  • Hydrocephalus ex vacuo – Katika aina hii, pia kuna kuongezeka ukubwa kwa vetrikali za ubongo na subarachnoid space kutokana na kusinyaa kwa ubongo ambapo kunaweza kusababishwa na ugonjwa wa dementia, baada ya kupata ajali ya kichwa au matatizo ya akili kama Schizophrenia.
Non communicating hydrocephalus (Obstructive hydrocephalus)
Aina hii husababishwa na uzuiwaji wa mzunguko wa CSF kwenda kwenye Subarachnoid space kutokana na uvimbe wa kwenye ventrikali.
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na kichwa maji kutokana na kuzaliwa nacho (congenital) au akakipata baadae maishani (acquired) baada ya kupata maradhi kwenye mfumo wa neva mwilini (CNS infections), ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), uvimbe kwenye ubongo, ajali ya kichwa, kuvuja damu kwenye ventrikali nk. Kichwa maji anachopata mtu baadae maishani huwa kinaambatana na maumivu makali sana.
Kichwa maji husababishwa na nini?
Tatizo hili huathiri zaidi watoto, ingawa inaweza kutokea kwa watu wa rika zote.
  • Maambukizi ya mfumo mkuu wa neva (ugonjwa wa uti wa mgongo na maambukizi katika ubongo), hasa kwa watoto chini ya mwaka mmoja.
  • Kuvuja damu katika ubongo wakati wa kujifungua au mara tu baada ya kujifungua hasa kwa Njiti.
  • Kuumia kabla ya kujifungua ,wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua
  • Kansa za mfumo mkuu wa neva ikihusisha ubongo na uti wa mgongo.
Dalili
Dalili hutegemea na sababu, umri, na kiasi cha ubongo kilichaathiriwa.
Kwa watoto chini ya mwaka mmoja
  • Kichwa huwa kikubwa kupita kiasi
  • Utosi kuvimba
  • Macho ambayo huonekana kwa nadhari kuangalia chini
  • Mtoto hukereka haraka (irritability)
  • Dege dege
  • Fuvu kutofunga vizuri
  • Kutapika
  • Kuwa na usingizi kila wakati
Dalili kwa watoto wa kubwa (zaidi ya mwaka)
  • Kulia kwa sauti kubwa sana kwa muda mfupi
  • Kupungua kumbukumbu, na uwezo wa kufikiri
  • Kubadilika kwa muonekano wa sura na nafasi kati ya macho
  • Macho huzunguka zunguka yenyewe
  • Kushindwa kula vizuri
  • Kulala kupita kiasi
  • Kichwa kuuma
  • Hasira na kukereka haraka
  • Kujikojolea
  • Wanaweza kushindwa kutembea vizuri
  • Kutapika
  • Ukuaji wa kusuasua
  • Ishara nyingine ni macho kutumbukia ndani, na kuwa na muonekano mwingine ambao sehemu nyeupe ya ndani ya macho huwa juu ya ile sehemu nyeusi na kitaalamu huitwa “sun setting appearance”
Kwa watu wazima
  • Maumivu ya kichwa
  • Kusahausahau
  • Kutapika
  • Kifafa
  • Kujikojolea
  • Miguu na mikono kuwa legevu
Vipimo na uchunguzi
  • X-ray ya kichwa
  • Kupima ukubwa wa kichwa (head circumference)
  • Cranial ultra sound..(ultrasound ya kichwa)
  • Head CT-scan – ambayo ndio kipimo kizuri na muafaka kwa tatizo hili
  • Head MRI-scan
  • Brain scan using radioisotopes
  • Lumbar puncture kuangalia ili kuchunguza zaidi Maji (CSF)
  • Radionuclide scan- hiki ni kipimo cha kichwa kinachoangalia mzunguko wa maji ya uti wa mgongo kwa kutumia madini ya nyuklia yanayotumika kwenye tiba. Mgonjwa huchomwa sindano kwenye uti wa mgongo iliyo na madini haya ya nyuklia na baada ya masaa 4 hadi 6 hupigwa picha ya Scan ambayo itaonyesha mzunguko wa maji ya uti wa mgongo. Picha hurudiwa tena baada ya masaa 24, 48 na hata baada ya masaa 72. Umuhimu wa kipimo hiki ni kwamba kinaweza kugundua wapi kuna uzuiwaji wa maji ya CSF, wapi yanapovuja kutoka kwenye uti wa mgongo, kama kuna kichwa maji, kugundua kichwa maji aina ya NPH, na hata baada ya operesheni ya kichwa maji kipimo hiki kinatumika kuangalia kama shunt zilizowekwa zimeziba au zipo wazi.
  • Kipimo cha kutumia mwanga (Transillumination) – Kinatumika kugundua kichwa maji kwa watoto wachanga au wale wa chini ya mwaka mmoja.
  • Picha za CT SCAN ya kichwa ambapo ya kushoto inaonesha dalili za kichwa maji – kuongezeka ukubwa wa ventrikali, nafasi zilizo wazi kuziba (sulcus), kutoonekana kwa choroid fissures, kupungua nafasi zinazozunguka ubongo (reduced subarachnoid space), kuongezeka ukubwa wa kichwa, kupungua kwa nafasi baina ya sehemu mbili za ubongo (reduced interhemispheric fissures) na kulia ni picha ya kawaida (normal).
Matibabu
Matibabu ya mwanzo
  • Tibu tatizo lililosababisha mfano kwa maambukizi toa Antibiotic
  • Matibabu tiba: Mannitol, hyperventilation, loop diuretics, steroid, acetazolamide.
  • Njia nyingine ni Cauterization kuunguza baadhi ya sehemu za ubongo zitengenezazo CSF, ili kupunguza utengenezwaji wa CSF
Matibabu kwa njia ya upasuaji
  • Ventriculo-peritoneal shunt
  • Lumbar peritoneal shunt
  • Endoscopic third ventriculostomy (ETV)
NA DR MAYANJA

Post a Comment

Previous Post Next Post