Uingereza: Daktari wa upasuaji matiti afungwa jela miaka 15 kwa upasuaji usiofaa

Daktari wa upasuajia wa matiti Ian Paterson amefungwa jela miaka 15 kwa kufanya upasuaji usio muhimu.
Daktari Ian PatersonHaki miliki ya pichaSWNS
Image captionDaktari Ian Paterson amefungwa jela miaka 15
Paterson, mwenye umri wa miaka 59, aliwafanyia upasuaji wanawake tisa na mwanamume mmoja baada ya kuwadanganya kuwa walikuwa na saratani ya matiti.
Amepatikana na hatia ya mashtaka 17 ya kujeruhi kwa makusudi, baada ya kesi iliyodumu kwa mwezi mmoja uliopita.
mwanamke anayechunguza saratani ya matitiHaki miliki ya pichaTHINKSTOCK
Image captionJopo la mahakama ya Nottingham liliambiwa kuwa Paterson alizidisha ama kubuni hatari ya saratani
Jopo la mahakama ya Nottingham liliambiwa kuwa Paterson alizidisha ama kubuni hatari ya saratani.
Mahakama iliambiwa kuwa alifanya upasuaji wa matiti kwa "sababu zisizojulikana" ambazo ni pamoja na shauku ya "kupata pesa za ziada"

1 Comments

Previous Post Next Post