Faida ya Tunda la Zabibu katika Kutibu Magonjwa ya Moyo

Faida ya Tunda la Zabibu katika Kutibu Magonjwa ya Moyo
Zabibu hutumika kutengeneza divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda. Tunda hili huweza kuwa katika rangi mbalimbali na katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.


Matunda haya inaelezwa kwamba yalianza kulimwa huko nchini Uturuki, lakini kwa hapa nchini kwetu Tanzania yanapatikana sana mkoani Dodoma.

Matunda haya huwa na rangi ya nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza , njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba hapa kwetu Tanzania wengi tumezoea zabibu za rangi nyeusi

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula  na Kilimo Duniani (FAO) linaeleza kuwa asilimia 71 ya zabibu yote duniani hutumika kutengenezea  mvinyo na asilimia 27 huliwa kama matunda ya kawaida, huku asilimia 2 ikifanywa kukaushwa.

Zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Aidha, inaeleza kwamba zabibu pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo kutokana  na sababu hii hupunguza hatari ya kukumbwa na kiharusi (stroke). Kunywa juisi ya zabibu nyekundu (red grapes) kuzuia damu kuganda ili kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

Utafiti uliofanyika mwaka 2005 kwa watu 1000 wenye matatizo ya magonjwa ya moyo ulibaini kwamba asilimia 50 ya watu hao matatizo yao ya shambulio la moyo (heart attack) au kurudiwa na kiharusi yalipungua kwa kunywa divai nyekundu (red wine) kiasi cha glasi moja kila siku wakati wa kula chakula.

Kwamba zabibu pia inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu na pia kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasiri (Hemorrhoids).

Kadhalika matunda hayo husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Zabibu pia husaidia kuimarisha afya ya figo na kuifanya kuwa na uwezo zaidi katika katika kuondosha sumu ndani ya damu .
Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari ya asili aina ya fructose na glucose hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.


Sambamba na hayo, watalaam wa afya hueleza kuwa juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng;enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Divai pia husaidia bacteria rafiki kwa binadamu wanaoishi ndani ya tumbo (normal flora) kukua vizuri na kusababisha umeng’enyaji wa chakula ndani ya tumbo kuwa rahisi.

Kutokana na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect).

Kwa wale wanaotaka kupunguza miili yao (slimming) na kuimarisha afya ya miili yao wanashauriwa kunywa juisi ya zabibu siku moja kila juma bila kula chakula kingine chochote siku hiyo. Na siku zingine za wiki wanapaswa kula mlo kamili (balanced diet).

Wataalam hushauri kwamba ni vizuri ukatumia kila siku japo punje za zabibu zisizopunguwa tano kwa ajili ya kulinda afya ya mfumo wa damu na nyama za moyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post