Umbo la figo/structure
Figoni miongoni mwa viungo muhimu vya mwili wa binadamu. Kukosa kufanya kwake kazi kunaweza kusababisha magonjwa mazito na hata mauti. Figo limejengwa kwa viungo vingi na kazi zake ni nyingi.
Kazi zake mbili muhimu ni: kutoa uchafu unaoathiri mwili na wenye sumu na kuweko usawa wa maji (fluids), madini and kemikali.
Umbo la figo/structure
Figo hutoa mkojo kwa kutoa uchafu wenye sumu na maji zaidi kutoka mwilini. Mkojo unaotengenezwa katika figo hupitia kwenye mrija uitwao” ureta, na huteremka hadi kwenye kibofu (bladder) na mwisho hutoka kupitia mrija wa urethra.
- Watu wengi (waume kwa wake) wana figo mbili.
- Figo ziko sehemu ya juu na nyuma ya tumbo, pande zote za uti wa mgongo (tazama mchoro) zinakingwa zisiathiriwe na mbavu za chini.
- Figo huwa ndani kabisa mwa tumbo kwa kawaida mtu hawezi kuzihisi.
- Figo ni viungo jozi ya umbo la aragwe lenye urefu wa sentimita 10, upande wa sentimita 6 na wembamba wa sentimita 4. Uzito wake ni kati ya gramu 150 – 170.
- Mkojo unaotengenezwa kwenye figo huteremka hadi kwenye kibofu kupitia kwenye ureta.
- Ureta ina urefu wa karibu sentimita 25 umbo la mrija uliotengenezwa kwa misuli ya kipekee.
Muundo na kazi ya figo ni sawa katika sehemu ya viungo vya kiume na kike.
- Kibofu ni kiungo chenye mwanya kilichoundwa kutokana na misuli inayolala.Kibofu kipo chini na mbele ya tumbo na ni stoo ya mkojo kwa muda. Chini na ndani mwa tumbo. Huwa kama mbwawa la mkojo.
- Kibofu cha mtu mzima huweza kubeba 400 – 500 mililita ya mkojo na iwapo kimejaa karibu pomoni, mtu, hujisikia kwenda kukojoa.
- Mkojo kwenye kibofu hutolewa kupitia urethra wakati wa kukojoa. Kwa wanawake, urethra yao ni fupi ilihali ni ndefu kwa wanaume.
Kwa nini figo ni muhimu kwa mwili?
- Sisi hula vyakula vingi na tofauti kila siku.
- Kiwango cha maji, chumvi na tindi kali (acids) katika miili yetu hutofautiana.
- Ile hali inayoendelea ya kubadilisha chakula ili kilete nguvu hutoa vitu/sumu mwilini.
Kazi za figo ni zipi
- Vitu hivi husababisha utofauti wa kiwango c tindi kali (acids) mwilini. Huu mkusanyi isiyohitajika huweza kuhatarisha maisha.
- Figo hubeba kazi muhimu sana ya kusafish vyenye sumu, tindi kali(acid) ya sumu na vi materials) hufanya hivyo wakati huo huo i kuhakikisha usawa wa kiwango cha maji, el cha tindi kali (acid base).
Kazi za figo ni zipi?
Kazimuhimu ya figo ni kutengeneza mkojo na huondoa vitu visivyofaa, chumvi chumvi ya ziad mwilini.
Kazi muhimu za figo zimeelezwa hapa chini.
1. Kutoa uchafu Kusafisha damu kwa kutoa uchafu ni kazi muhimu sana ya figo. Vyakula tunavyokula huwa na protini. Protini ni muhimu kwa kukua na kurekebisha mwili. Lakini jinsi protini invyotumika na mwili hutoa uchafu. Mkusanyiko wa uchafu huu ni kama sumu kwenye mwili. Figo huchuja damu na uchafu hatari (wa sumu) na hutolewa katika mkojo.
Creatinine na urea ni aina mbili muhimu ya uchafu ambao kiwango chake katika mwili wa binadamu huweza kupimika.Kiwango chake katika damu huonyesha jinsi figo zinavyofanya kazi Iwapo figo zote mbili
zimeshindwa, kiwango cha creatine na urea kitakuwa juu katika uchunguzi wa damu.
2. Kutoa maji(fluid) mengi
Kazi ya pili muhimu ya figo ni kulinganisha fluid kwa kutoa maji zaidi kama mkojo na kubakiza kiwango muhimu cha maji katika mwili. Kwa hivyo figo huweka kiwango kamili cha maji yanayohitajika katika mwili.
Figo zinaposhindwa, hushindwa kutoa maji zaidi kama mkojo. Maji mengi mwilini huchangia kuvimba kwa mwili.
3. Kusawazisha madini na kemikali
Figo hufanya kazi nyingine muhimu ya kusawazisha madini na kemikali kama sodium, potassium, hydrogen, calcium, phosphorus, magnesium na bicarbonate na husawazisha kiwango kamili cha fluid kwenye mwili. Kubadilika kwa kiwango cha sodium uweza athiri fahamu ilhali kubadilika kwa kiwango cha potassium huweza kuwa na madhara makubwa kwa mapigo ya moyo na kufanya kazi kwa mishipa. Kuweka kiwango sawa cha calcium na phosphorus ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno.
4. Kuchunga Shinikizo la damu
Figo hutoa hormoni mbalimbali (rennin, angiotensin, aldosterone , prostaglandin ….nk) na kusawazisha maji na chumvi kwenye mwili ambayo hufanya kazi muhimu kwa kulinda msukumo wa moyo. Usumbufu wa kutoa hormoni na kusawazisha chumvi na maji kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa figo uongeza msukumo wa damu kwenye moyo ( shinikizo la damu / high blood pressure).
5. Uzalishaji wa chembechembe za damu nyekundu
Erythropoietin inayotolewa kwenye figo hufanya kazi muhimu katika kutoa chembechembe za damu nyekundu (RBC).Figo likishindwa husababisha figo hilo kutoa erythropoietin kidogo ambayo baadaye husababisha kupungua kwa RBC na matokeo yake huwa hemoglobin kidogo (anemia).
Kwa sababu ya kutoa erythropoietin kidogo kwa wagonjwa ambao wana shida ya kushindwa kwa figo, hemoglobin haiwezi kuongezeka hata kama itaongezewa kwa madini ya chuma na vitamin.
6. Kuendeleza mifupa yenye afya
Figo hubadilisha vitamin D katika hali yake ya kutumika, ambayo n muhimu kwa kunyonya calcium kutoka kwenye chakula, kukua kwa mifupa na meno na kuweka mifupa yenye afya. Katika hali ya figo kushindwa kufanya kazi,na kwa sababu ya upungufu wa vitamin D kunafanya kukua kwa mifupa kunapunguzwa na kuwa hafifu. Kushindwa kukua inaweza kuwa ishara ya kwanza kwa watoto walio na shida ya kushindwa kwa figo.
Damu inasafishwa vipi na mkojo kutengenezwa?
Katika harakati ya kusafisha damu, figo husalia na vitu muhimu na kwa huchagua kutoa maji yaliyozidi zaidi, madini na uchafu wowote Ni muhimu tuelewe mbinu muhimu na ya kushangaza ya kutengeneza mkojo.
- Je wajua? Kila dakika ml 1200 ya damu huingia katika figo zote kwa kusafishwa, ambayo ni asilimia 20% ya damu yote inayosukumwa na moyo. Kwa hiyo kwa siku lita1700 ya damu inasafishwa!
Kazi kuu ya figo ni kutoa uchafu na vitu hatari na maji yakupindukia kutengeneza mkojo.
- Njia hii ya kusafisha mwili hutokea katika vitu vidogo vya kuchuja vinavyojulikana kama nephron.
- Kila figo huwa na karibu na nephron million moja. Kila nephron imeundwa na glomerulus and tubules.
- Glomeruli ni vichungi na mashimo madogo madogo sana yenye sifa ya kuchuja kwa kuchagua. Maji na vitu vidogo huwa rahisi kuchujwa. Lakini chembechembe kubwa za damu nyekundu, chembechembe za damu nyeupe, platelets, protini n.k haviwezi kupita katika mianya hii. Kwa hivyo katika mkojo wa watu wenye afya hakuna vitu vikubwa katika mkojo wao.
- Hatua ya kwanza ya kutengeneza mkojo hufanyika katika glomeruli, ambapo 125 ml za mkojo hutolewa kwa dakika. Ni jambo la kushangaza kuwa kwa saa 24, lita 180 ya mkojo imetengenezwa! Haina uchafu pekee, madini na sumu lakini hata glucose na vitu vingine muhimu.
- Figo hufanya kazi ya kunyonya kwa uerevu mkubwa mno. Kutokana na lita180 za maji ambayo huingia kwenye tubules asilimia 99% ya maji hunyonywa na asilimia 1% tu hutolewa kama mkojo.
- Katika njia hii erevu vitu vyote muhimu na lita 178 ya maji yananyonywa na vijishipa na kati ya lita1-2 ya maji, vitu vichafu, madini zaidi na vitu vingine hatari hutolewa.
- Mkojo uliotengenezwa kwenye figo huteremka kupitia ureta hadi kibofu cha mkojo (urinary bladder) na baadaye kutoka nje kupitia urethra.
- Je kunaweza kuwa na tofauti ya kipimo cha ujazo cha mkojo kwa mtu mwenye figo lenye afya?
- Ndio. Kiwango cha kunywa maji na hali ya hewa (atmospheric
Kiwango kidogo sana au kingi sana cha mkojo kutengenezwa, huashiria kuwa figo yataka kuangaliwa na kuchunguzwa.
temperature) ni sababu kuu ambazo huamua kiwango cha mkojo kwa mtu mzima.
- Iwapo kiwango cha maji yaliyonywewa ni kidogo,huwa kidogo, mkojo huwa na vitu vingi vya chumvichumvi (concentrated), na kiwango cha chinihuwa karibu 500ml. Lakini maji mengi yakinywewa, mkojo mwingi unatengenezeka.
- Wakati wa jua (summer) kwa sababu ya joto na kutoa jasho nyingi kipimo cha mkojo hupungua. Wakati wa baridi (winter) hali ni tofauti – kiwango cha joto ni cha chini,hakuna kutokwa na jasho, mkojo huwa mwingi.
- Kwa mtu anayekunywa kiwango cha maji kinachofaa, na iwapo kipimo (volume) cha mkojo anaokojoa ni chini ya 500ml lakini zaidi ya 300ml ni ishara tosha kuwa figo inahitaji uchunguzi.wa haraka.
Tags:
FIGO