Dawa tano za asili zaidhinishwa Tanzania

Dawa za asili maarufu kama 'miti shamba'
Hivi karibuni nchini Tanzania kumeshamiri kwa uwepo wa matangazo mbalimbali ambayo mengine ni rasmi na mengine sio rasmi kuhusiana na dawa za asili haswa za kuongeza nguvu za kiume lakini sasa serikali ya nchi hiyo imethibitisha matumizi ya dawa tano za asili.
Huku miongoni mwa dawa hizo ni dawa ya 'Ujana' ambayo kazi yake ni kusaidia kuongeza nguvu za kiume wakati dawa nyingine zikiwa Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver ambazo kazi yake ni kukemea vimelea mbalimbali.
Dawa za kiume za vidonge maarufu, ViagraHaki miliki ya pichaPA
Image captionDawa za kiume za vidonge maarufu, Viagra
Baraza la dawa nchini humo limesema hatua hii imekuja baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na kubaini kuwa dawa hizo hazina madhara kwa afya ya binadamu hivyo hawana budi kuzikubali.
Aidha Paul Muhame ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa za asili nchini Tanzania anasema baada ya baraza kupitisha vigezo vyote vilivyohitajika kutoka katika dawa hizo na mamlaka ya dawa na chakula wamethibitisha hilo.
"Suala la muhimu ambalo tumeliangalia zaidi ni usalama wa mtumiaji lakini katika upande wa kuthibitisha kuwa dawa hizo zinaponyesha au la, linabaki kwa mnunuaji na mtumiaji wa dawa hiyo''.
Aina ya kuvu fulani nchini Nepal inayotambuliwa kwa uwezo wake wa kuongeza nguvu za kiume.
Image captionAina ya kuvu fulani nchini Nepal inayotambuliwa kwa uwezo wake wa kuongeza nguvu za kiume.
Aliongeza kwa kusema kwamba jukumu lao zaidi ni kuangalia usalama lakini sio dawa inatibu kwa kiwango gani.
Uthibitisho wa dawa hizo umeleta mijadala mbalimbali katika vipindi vya radio nchini humo haswa katika upande wa serikali kuthibitisha dawa ya nguvu za kiume kuuzwa kihalali .
BBC iliweza kupata maoni mbalimbali kutoka kwa Watanzania kuhusiana na uthibitisho wa dawa hizo:
Maoni
Image captionMaoni
'Watu watazinunua lakini hakuna mtu atakuwa na uhakika kwamba dawa hizi zinatibu sana sana atabahatisha tu,"
" inaweza isilete madhara lakini huwezi kujua baadae lakini kiukweli inabidi ziangaliwe kwa watu maalum kwa watu wanaouza ili mtu akidhurika ajue ataenda kwa nani?" Thomas Hemed ,mkazi wa Dar es salaam amesema
Maoni
Image captionMaoni
Sababu za kukosa nguvu za kiume:
  • Magonjwa (kisukari, saratani)
  • Msongo wa mawazo
  • Kutumia aina fulani ya dawa kwa mfano dawa za kudhibiti msukumo wa damu (BP)
  • Umri mkubwa
  • Kukosa usingizi wa kutosha
  • Matatizo ya kihomoni

Post a Comment

Previous Post Next Post