Matatizo ya kimaumbile kwa watoto

Matatizo ya kimaumbile

Mtindio wa ubongo

Mtindio wa ubongo ni upungufu katika utendaji wa ubongo ambao huathiri jinsi mtoto anavyotembeza au kuuhimili mwili wake.
  • Katika kuzaliwa, mtoto anaweza kuwa teketeke na mwenye viungo visivyo imara (lakini wakati mwingine huonekana kuwa katika hali ya kawaida mwanzoni).
  • Mtoto anavyokua, huendelea polepole kuliko watoto wengine. Anaweza kuchukua muda mrefu zaidi kufikia hatua ya kuinua kichwa chake, kukaa, au kutambaa.
  • Mtoto anaweza kupata shida wakati wa kula.
  • Anaweza kuhangaika na kulia sana. Au anaweza kuwa mkimya kuliko kawaida.
  • Kadri anavyokua, mwendo wake huwa wenye kukakamaa na kutikisika.
Karibu watoto wote wenye mtindio wa ubongo hufikiria na kujifunza polepole kuliko kawaida, lakini hawachukulii jambo hili kuwa kweli. Watoto wenye tatizo la kupooza ubongo wanaweza kucheza, kujifunza, na kwenda shule.
Mtoto mwenye miguu iliyokingamana, mkono uliopinda, na kichwa chake kikiwa kimelalia upande mmoja akiwa ameshikiliwa na mtu mzima
Uso, shingo au mwili hujigeuza na kutua kwa mshtuko. Misuli ndani ya miguu iliyokaza husababisha miguu kukingamana kama mkasi.
Mtindio wa ubongo hauwezi kutibika. Lakini unaweza kumsaidia mtoto mwenye ulemavu huu kutembea zaidi akijitegemea, kuwasiliana, na kujihudumia mwenyewe na watu wengine. Tafuta msaada kutoka kituo chochote kinachotoa tiba au huduma ya fiziotherapi. Pia soma Watoto Wenye Ulemavu Vijijini kwa taarifa zaidi juu ya kumhudumia mtoto mwenye mtindio wa ubongo.
Mtoto mwenye kitovu kilichojitokeza nje kidogo
Mtoto mwenye kitovu ambacho kimejitokeza nje sana

Henia ya kitovu (kitovu kilichojitokeza nje)

Kitovu ambacho hujitokeza nje husababishwa na misuli ya tumbo kuachana kidogo. Kawaida misuli hufungamana yenyewe na tatizo hili halihitaji dawa. Kufunga kitambaa au kamba kukizunguka kitovu pia haitasaidia.
Hata henia ya kitovu kama hii siyo hatari na mara nyingi hutoweka yenyewe. Kama itaendelea kuwepo mtoto anapofikisha miaka 5, tafuta ushauri wa daktari. Huenda operesheni ikahitajika.

Korodani kuvimba, busha, na henia

Mtoto mwenye mfuko wa korodani uliovimba upande mmoja
Mfuko wa korodani unaweza kujaa majimaji au na pindo la utumbo. Hii husababisha uvimbe sehemu iliyoathiriwa.
Unaweza kugundua chanzo cha tatizo. Mulika na tochi nyuma ya mfuko wa korodani.
  • Kama mwanga wa tochi utapita hadi upande wa pili, mfuko wa korodani umejaa majimaji. Tatizo hili hujulikana kama busha na kawaida hutoweka lenyewe. Kama litaendelea kwa zaidi ya mwaka 1, tafuta ushauri wa daktari.
  • Kama mwanga wa tochi hautapita hadi kuonekana upande mwingine na uvimbe ukazidi kuongezeka mtoto anapokohoa au kulia, pindo la utumbo litakuwa limejipenyeza ndani. Tatizo hili hujulikana kama henia.
Kinena cha mtoto, kikiwa na uvimbe upande mmoja juu ya ume
Henia inaweza kusababisha uvimbe sehemu ilioelekezwa na mshale kwa msichana au mvulana (kwenye mchoro). Kama uvimbe utazidi kuongezeka mtoto anapokohoa au kulia, huenda ikawa henia. (Kama utabaki vilevile, huenda ni uvimbe tu wa tezi la limfu (lymph node), angalia Kumchunguza mgonjwa (kinaadaliwa).

Henia inaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hospitalini. Unaweza kusukuma na kuirudisha ndani kwanza:
  1. Kama inawezekana mpatie mtoto dawa ya diazipamu ili kumtuliza.
  2. Mtoto miguu yake ikiwa imetanuliwa na kupinda kwenye goti, na mtu mzima akisukuma henia yake ili kuirudisha sehemu yake
  3. Tumia miito, au inua sehemu ya chini ya kitanda au mkeka ili kiuno cha mtoto kiwe kimeinuka juu zaidi ya kichwa chake.
  4. Mwezeshe kupinda goti lake na kutanua mguu wa upande wenye henia – kama chura.
  5. Weka kitu baridi cha kusukumizia mfano barafu ikiwa imefungwa kwenye kitambaa juu ya henia ili kupunguza uvimbe. Subiri kwa dakika 10 au zaidi.
  6. Kama hii haitasaidia, unaweza taratibu na polepole kujaribu kubonyeza henia kuirudisha katika nafasi yake.
Mtoto atahitaji kufanyiwa upasuaji, hata kama utakuwa umeirudisha henia katika nafasi yake.
Maumivu makali kwenye mfuko wa korodani, hasa yakianza ghafla, kawaida hutokana na tishu kujisokota ndani ya mwili. Mvulana mwenye msokoto wa tishu ndani ya korodani atahitaji kufanyiwa upasuaji mara moja ili kuinusuru korodani hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post